Mlalamikaji kesi ya jerry muro akiri kutoa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlalamikaji kesi ya jerry muro akiri kutoa rushwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lokissa, Jan 25, 2011.

 1. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  January 24, 2011 at 5:25pm


  [​IMG]Michael Wage akiondoka mahakamani baada ya kukiri kutoa rushwa ya shilingi milioni 10.
  Na Richard Bukos
  ALIYEKUWA Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage, ambaye kwa sasa ni mlalamikaji na shahidi wa kwanza katika kesi ya kutaka kupokea rushwa ya shilingi milioni 10 inayomkabili mtangazaji wa kituo cha luninga cha Taifa (TBC1), Jerry Muro, amekiri kutoa rushwa ya kiasi hicho cha pesa.

  Wage alisema hayo baada ya kubanwa na wakili wa upande wa utetezi, Majura Magafu, aliyemtaka kuelezea lengo la kutoa shilingi milioni moja alizodai kuwapa Jerry Muro na wenzake.

  Mlalamikaji huyo alisema aliwapa Jerry Muro na wenzake kiasi hicho fedha ili wasirushe hewani kwenye kipindi cha ‘Usiku wa Habari’ tuhuma za matumizi mabaya fedha kwenye Halmashauri ya Bagamoyo.

  Magafu alimueleza Wage kuwa kitendo chake cha kueleza mahakamani kuwa alitoa rushwa ili tuhuma zake zisirushwe kwenye luninga kinathibitisha kuwa mlalamikaji huyo ana kesi ya kutoa rushwa, hivyo kosa hilo linaweza kumpeleka jela.

  Kesi hiyo iliyounguruma leo inatarajiwa kuendelea tena mahakamani hapo kesho, Jumanne, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Mirumbe.HAPA MWANDISHI KACHEMSHA.HUYU HAKIMU SI MFAWIDHI,ILA UJUMBE UKO SAWA​

  [​IMG]Jerry Muro, akiondoka mahakamani.
  [​IMG] ...​
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hivi hili sakata bado halijaisha tu..? na huyu Jerry anafanya kazi wapi sasa au ni Freelance?
   
Loading...