Habari wanabodi,
Mimi ni mtumishi wa umma, idarani kwetu tumebahatika kupata mkuu mpya yapata mwaka sasa.Tatizo la boss huyu anasikiliza maneno ya majungu ya watumishi wenzangu, yani akisikia shutuma kukuhusu hafanyi uchunguzi,anaziamini direct na kuanza kukuongelea vibaya kwenye vikao na kwa wafanyakazi wengine.
Binafsi nimekuwa muhanga wake baada ya wanoko kumpelekea maneno kunihusu,basi sina amani kazini,anaishia kunizungumzia vibaya kwa watendaji wenzangu.
Tabia hii nimeipuuzia kwa muda ila naona kadri siku zinavyosonga naanza kuichukia ofisi na kutotamani hata kufika kazini.Suala la bajeti ya idara ameliacha kwa watumishi wachache wanao jiandikia posho afu watumishi wengine tunawekwa kando.
Niliwahi kumuomba kiasi fulani cha matumizi ya internet kwaajili ya mfumo wa idara akanitoa resi ofisini kwake,ila kwa fungu hilohilo nililoomba nipewe kiasi cha mtandao walikomba watu wengine tena bila kufanya lolote ila iliporudi hoja ya matumizi ya pesa hizo akaning'ang'aniza mie nijibu.
Kuna mengi ambayo siwezi yaanika hapa, naomba ushauri wenu nifanyeje??kwani nafikiria kuhama kituo cha kazi.