#COVID19 Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amechanjwa chanjo ya COVID-19

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
MTATIRO ACHANJWA

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amechanjwa chanjo ya korona.

Mtatiro ametekeleza wajibu huo binafsi katika hafla ya uzinduzi wa chanjo wilayani Tunduru huku akifuatiwa na mamia ya wananchi.

Mtatiro ameiomba wizara ya Afya na Rais Samia Suluhu Hassan waharakishe kuongeza chanjo nyingine kwani zilizopo tayari zinagombaniwa na wananchi wengi ambao wameanza kujiandikisha tangu wiki iliyoisha.

Mtatiro amewataka wananchi wa Tunduru kuchanja wa hiari, kujifunza na kujua maana ya chanjo na umuhimu wa kuimarisha kinga ya mwili ili usivamiwe na virusi vya korona kirahisi, na hata inapotokea mwili ukavamiwa basi kusiwe na madhara makubwa.

Idd Mohamed
Tunduru,
05 Agosti 2021

 
Back
Top Bottom