Mkuu wa Wilaya ya Mwanga amsimamisha kazi mwenyekiti wa kijiji kwa kumtapeli Mkorea milioni 19

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,880
6,366
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Kivulini Yusuf Semvua na wajumbe wanne wa Serikali yake wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wamesimamisha uongozi kwa tuhuma za kumtapeli raia wa Korea Bw.Byung Yai Lee sh 19mil/= za ununuzi wa ekari tisa za ardhi ambazo alitaka ajenge chuo cha ufundi katika kijiji hicho.

Mkuu wa wilaya ya Mwanga Bw.Shayibu Ndemanga amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha na kitendo cha viongozi hao ambao wamekiri na kukubali kupokea fedha hizo ambazo waligawana kwa viwango tofauti akiwemo mchungaji wa kanisa la Pentekoste.

Bw.Ndemanga amesema, ingawa viongozi hao ambao walipigwa picha na wakorea wakiwa na mfuko mweusi wenye fedha hizo baada ya kuzipokea wamekubali kuzirejesha kupitia jeshi la polisi lakini hatua za kisheria lazima zichukuliwe dhidi yao.

Katika mgawo huo mchungaji huyo alipewa shs. 7mil= kwa madai anaenda kugawana na wachungaji wenzake wakati si kweli, mwenyekiti wa kijiji shs 3.5mil/= na wajumbe wengine shs. 1.7mil/= kila mmoja..

Wananchi wa kijiji hicho wamesema, viongozi hao hawana budi kuchunguzwa zaidi kwa kuwa wana tuhuma nyingi za ubadhilifu ikiwa ni pamoja na kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati.

Kwa upande wao wanawake wa kijiji hicho wamesema wamekuwa wakinyanyaswa na uongozi wa serikali ya kijiji hicho walipokuwa wakienda kutafuta kuni na kila walipookota kuni hizo wanakamatwa.
 
Hadi baba mchungaji yupo kwenye mgawanyo wa mtonyo,ila naona amewapiga wenzie!!
 
DC yuko sawa kweli? Raia ananunua ardhi kwa sheria ipi? Huyo mwenyekiti na wenzake wako sahihi kabisa kuitafuna hiyo pesa bila kutoa ardhi.
Kama DC katumia kosa hilo kuwaadhibu, kawaonea.
 
DC yuko sawa kweli? Raia ananunua ardhi kwa sheria ipi? Huyo mwenyekiti na wenzake wako sahihi kabisa kuitafuna hiyo pesa bila kutoa ardhi.
Kama DC katumia kosa hilo kuwaadhibu, kawaonea.
Hata mm nashangaa. Mbona juzi kati Kuna mtu alituhumiwa kumdhulumu jamaa lakini ikakaushwa
 
Hivi DC ana mamlaka ya kumsimamisha mwenyekiti wa kijiji kazi mtu ambaye amechaguliwa na wananchi, ipo siku DC atamsimamisha mbunge kazi.
 
Tamaa hadi kwa wachungaji jamani! Haya wanatupeleka wapi haswa wanaojiita waunganisgaji wa waumini na MUNGU lakini? Huyo mchungaji ahukumiwe kulingana na dhambi same ili ujue kapotosha jinsi kuwa na hayaishii hapa duniani hata akhera anasubiriwa tu.hasa wengine wote nani kulingana na Sheri's ya nchi
 
Hii wilaya inahitaji mtu mwenye maono kama Mwl.Joseph KAHOKO Wa pale Lembeni mzee Yuko vizuri pamoja name umri kwenda
 
Hivi DC ana mamlaka ya kumsimamisha mwenyekiti wa kijiji kazi mtu ambaye amechaguliwa na wananchi, ipo siku DC atamsimamisha mbunge kazi.
Ndio ilivyo. Kwa mujibu za sheria za serikali za mitaa DC ana mamlaka hata ya kufuta serikali ya mtaa akijiridhisha kuwa uvunjifu wa sheria umefanya. Pia Dc ndio mamlaka ya rufaa iwapo mkutano wa kijiji ukaamua kumvua uongozi m/kiti au wajumbe wake.
 
DC yuko sawa kweli? Raia ananunua ardhi kwa sheria ipi? Huyo mwenyekiti na wenzake wako sahihi kabisa kuitafuna hiyo pesa bila kutoa ardhi.
Kama DC katumia kosa hilo kuwaadhibu, kawaonea.
Sheria ya ardhi ya tz hairuhusu mtu asiye raia kumiliki ardhi. Akimiliki basi iwe ni kwa uwekezaji na awe na kibali cha TIC. Ila bahati mbaya TIC pana rushwa ya kufa mtu. Hivyo vibali vinatolewa hovyo tu hata kwa asiye na sifa maadamu kaweka mpunga kwa meza.
 
Ndio ilivyo. Kwa mujibu za sheria za serikali za mitaa DC ana mamlaka hata ya kufuta serikali ya mtaa akijiridhisha kuwa uvunjifu wa sheria umefanya. Pia Dc ndio mamlaka ya rufaa iwapo mkutano wa kijiji ukaamua kumvua uongozi m/kiti au wajumbe wake.
Sheria hiyo ni mbovu sana yule ni mteule wa wananchi ndio wanaopaswa kumwajibisha
 
Hivi kumbe MWENYEKITI WA KIJIJI ni mfanyakazi mpaka asimamishwe kazi? Mimi nilifikiri ni KIONGOZI wa siasa/serikali kwa hiyo DC atakuwa amemsimamidha UONGOZI na sio kazi
 
Back
Top Bottom