Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Joketi Mwegelo ni mwanasiasa bora kwangu 2015 - 2020

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Neno siasa linahusu mfumo wa maisha. Katika vitu vinavyomtofautisha Joketi Mwegelo na wanasiasa wengine ni hiki.

Katika kipindi kifupi cha Ukuu wa Wilaya yake ametumia muda wake karibu wote kuzungukia wananchi wa vijijini na kujua changamoto zao.

Kama mkuu wa wilaya hakujihusisha kabisa na malumbano ya kisiasa bali kujalibu kutatua changamoto za watu wa wilaya yake. Mfano kafanikisha ujenzi wa shule nzuri sana ya wasichana ili kukabiliana na changamoto za mimba mashuleni.

Amejitahidi kulinda cheo chake kwa kufanya kazi siyo kusifu tu. Kwangu ni mtu bora sana.

Kwa ugeni wake wa siasa namuona mtu Bora Sana kwangu katika wakuu wa wilaya wote kwani wakuu wa wilaya wengi hujitenga na kuhamasisha shuguli za maendeleo na kujitwika uanajeshi na kuwaachia wabunge na madiwani pekee.

Natamani siku moja nimuone akiwa bungeni sema tu CCM hawataki mpasuko wowote ule kuelekea uchaguzi.
 
Back
Top Bottom