Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amshukuru Pierre Liquid kwa kuhudhuria na kuhamasisha TOKOMEZA ZERO KISARAWE

Jumapili ijayo bashite anaenda kulia kanisani maana leo kapigwa ambush kila kona wanamsupport liquid
Aibu nimeona mimi
Ataenda kanisa gani sidhani kama RC watampokea wao huwa hawaendekezi mambo ya kulia lia na kujipendekeza kwa viongozi. Labda aende kwa mzee wa upako, kwa Gwajima, mama Rwakatare au Mwamposa. Lutherani na Ephata alishapita na kuangusha vilio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana Makonda kwa kweli kachemka. Hajaonyesha ukomavu. Hakuwa ma busara.
Makonda kasahau haraka sana alipotoka, ccm imembeba sana na itaendelea kumbeba sanaaaa kutokana na uoga wa JIWE kuvunja agano la kichawi alilofunga na Makonda ambapo yeye Makonda aliitumia fursa kumlisha maneno ya vitisho sangoma ambapo sangoma naye akamtisha jiwe. Ni kwa sababu ya agano hili Makonda amejaa kila aina ya kiburi,dharau, ushetani usiomithilika maana anajua fika kuwa JIWE hawezi vunja agano lao! lakini ni heri basi akakumbuka JIWE ipo siku ataondoka enzini na ni vyema kwa akiba ya roho yake angeanza kuwekeza katika wema, ustaarabu na yote yaliyo mazuri ili siku akifika kwa Muumba adhabu ya kaburi isiwe upande wake, maana hatujui siku wala saa.
 
Pale mkuu wa wilaya wa taifa anapoonekana kumfunika mkuu wa mkoa wa taifa ka pierre kanatolewa sadaka tu ili kumzima mkuu wa wilaya asije nyakua mkoa
 
Asante Jokate kwa kutokuonyesha unafki na kusimamia unachokiamini!

Binafsi namwona Pierre kama comedian na anachokifanya akiwezi kunishawishi au kunivutia kunywa pombe. Na ukiangalia watu wamekuwa wanavutiwa na anachokisema ndio maana phrases kama, “Mama nakufa, atabaki kuwa juu,....” na sio tume kuwa tukiona watu wakionyesha/kuposti clips za pombe au wakiwa wamelewa.

Nilichovutiwa na Jokate ni alichosema ni kumwunga mkono Pierre kwenye biashara zake za furniture na Wilaya ya kisarawe itanunua Madawati kutoka kwake.

Wasiwasi wangu tunao mtetea Piere leo na kesho.Je, wiki ijayo au mwezi ujao atutageuka na kuanza kumkebei Piere na kuunga mkono alichosema Makonda?
 

Attachments

  • 27B2482A-5CEB-4FA8-896E-ACD15A4D58CD.png
    27B2482A-5CEB-4FA8-896E-ACD15A4D58CD.png
    208.6 KB · Views: 88
Back
Top Bottom