Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amshukuru Pierre Liquid kwa kuhudhuria na kuhamasisha TOKOMEZA ZERO KISARAWE

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,450
12,316
949019c787c7038898bcc6a5c4715006.jpg

Hakuna maneno Muhimu na Machache katika ustawi wa maisha ya Binadamu kama Tafadhali, Asante na Samahani.
Katika Dhifa niliyoiandaa jana, nilialika watu wengi, Wanasiasa, Taasisi za Kiserikali, Mabalozi, Wafanyabiashara, Wajasiriamali, Wasanii, Wadau wa Burudani N.k.

Na Makusudio ya yote hayo wote tunayajua, ni kutafuta MOTISHA juu ya ELIMU ya Mtoto wa kike, Kisarawe na kote nchini.

Na kwangu mimi na Wilaya nzima ya Kisarawe wote waliofika jana ni muhimu sana sana kwangu na kwetu.

Kipekee kabisa nimshukuru Piere Liquid wako watu maarufu wengi mno tuliowaalika lakini hawakufika. Ila wewe ulichukua muda wako kuhamamisha na kufika na zaidi ya hapo ukatoa mchango wa TSH LAKI MOJA!!! Hukuja kuuza sura tu!! Nasema ASANTE SANA. Wana Kisarawe tunakupenda na tunakukaribisha kuwekeza Kisarawe uanzishe hata mgahawa tutakusaidia kupata eneo.

Lakini pia nimesikia ni mtengeneza mzuri sana wa furniture. Hii Shule tunayoenda kujenga inahitaji madawati Naomba tufanye kazi nawewe katika hii fursa. Tuangalie namna japo kidogo tukuwezeshe.

Tunasema Karibu Kisarawe Ukae. Kisarawe Kunogile. Tunasema Samahani kwa kukwazika lakini zaidi Asante Sana kwa kushiriki kwenye

#TokomezaZeroKisarawe #ElimuItabakiKuwaJuuKileleni #KisaraweMpya
Ubarikiwe!!!!
 
Back
Top Bottom