Mkuu wa wilaya ya Kahama amuomba Magufuli ampumzishe kazi hiyo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Kahama. Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote.

Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti.

Chanzo:Mwananchi
 
umekurupuka sana mkuu kichwa cha habari na content ni tofauti kichwa cha habari kina sema mkuu wa wilaya ya kahama ila kwenye content umeeelezea wilaya ya iramba kipi ni kipi sasa
 
Bora huyu alieamua kupumzika, kuliko kukazana na kazi wakati umechoka na umejiona huwezi tena hiyo shughuli.
 
Kahama. Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote.

Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti.

Chanzo:Mwananchi
upo KAHAMA eeee:)
 
Mara kahama Mara Singida tukueleweje wewe?au ni mambo ya Umeya wa Jiji yamekuchanganya?
 
Serikali ishindwe kutoa pesa za madawati lawama iende kwa mkuu wa wilaya, watu waugue kipindupindu kwa sababu serikali imeshindwa kuzoa takataka lawama kwa DC, hali ya hewa wamedanganya Elinino mpaka leo tunapata elinino ya Joto kali tu, ikija njaa baadae lawama kwa DC na sio mungu, mbona majanga! Kuliko kumpa sifa Magufuli bora ukuu wa wilaya wapewe viherehere wa Lumumba
 
Back
Top Bottom