Mkuu wa wilaya ya Hai ana PhD feki!

Mkuu wa wilaya ya Hai ana PhD feki!

kanda2

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2007
Posts
1,319
Reaction score
76

Mkuu wa wilaya ya Hai anajiita Dr.Norman Sigalla ana PhD feki kama za kina Nchimbi & co. yeye kaipata ndani ya wiki nane. bwana Msemakweli usimsahau kwenye orodha yako.Mke wake ambaye ni mbunge nae alikuwa anatafutiwa PhD Mzumbe.
 
Phd's ndo mtindo wa kuishi siku hizi kwenye serikali yetu mkuu. Kama mawaziri wanazo za bandia, unategemea nini kwa watu waliochini yao?
 
Their PHDs stands for Place Him\Her Down,and thats what they are realy doin to us!!
 
Jamani hizi PhD hizi zitawatoa roho.

Dr Hamza vipi PhD yako sio feki?
 
Kwani sheria zilizombana Mh Kihiyo wao haziwahusu?
 
Hivi yeye haoni aibu! Na wakumpa adabu juu ya madanganyifu yake ni nani? Je hajui? Hii ndiyo Tanzania!
 
duu jamani hivi ni kwanini? na ukimwona mambo yake fehi kweli
 
Hebu tupate data zake naye kasoma 'vyuo' vipi?
 
Mnashangaa nini sasa; huyu huyu ndio CCM ilimchagua akawa mbunge wetu kwenye bunge la Afrika Mashariki kwa kipindi kifupi na huko hakufanya lolote isipokuwa kuonesha ukihiyo wake!! Sasa hawa ndio vijana CCM ya wakina Malecela inawatayalisha kuwarithisha nchi!! Mkulu Jakaya yeye mambo ya elimu hayamkoseshi usingizi kwani alipopata ile B.A. yake imentosha na ndio maana hata hao wapambe wake wanaofoji vyeti hawashuhulikii kwani haoni tofauti!!
 
mkuu shkamoo..hahaaa kweli JK mamabo ya elimu hayamkoseshi usingizi kabisaaaaa.kwanza anawashangaa wanaopiga piga kelelee
 
Vipi Phd ya George Nangale,mbunge wa EALA?Nimegoogle,sipati kabisa CV yake!Ni feki vilevile
 
Kuna kundi la UVCCM wa zama za Nchimbi liliibuka kwa nguvu zote kusaka PhD kwa gharama yoyote ile na huyo Mkuu wa Wilaya ya Hai ni mmoja wao, kwa hiyo sishangai kusikia kwamba ana PhD, na sijui kaisoma lini, na ni ya nini.

Bongo kila kitu kinawezekana!
 
ya utawala.
 
Jamani hizi PhD hizi zitawatoa roho.

Dr Hamza vipi PhD yako sio feki?

😱 😱 Lahaulaah! Sikutegemea kabisa ungemuuliza swahiba wako "Duktur" Hamza swali kama hili!

Ama kweli mambo ni "As salaam'alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh"!!! Bwahaahaa! 😀

Nadhani kama kweli ana Phd basi kaipata baada ya kuandika "thesis" kuhusu "Mauaji ya Mwembechai" na historia ya "Vatican na Nyerere".
 
Vp Makete mpo hapo?

Mapembelo?
Ustake Ncheke we malila, huyo ni future MP wa Makete na labda atakuwa minister kwenye serikali ya awamu ya nne second term ha ha ha, kwa hiyo tupo kama hatupo tume-mute
 
Mapembelo?
Ustake Ncheke we malila, huyo ni future MP wa Makete na labda atakuwa minister kwenye serikali ya awamu ya nne second term ha ha ha, kwa hiyo tupo kama hatupo tume-mute

Mapembelo va vene va hwavwe,

Ina maana aliyepo kwisha habari yake? Naam ngoja tumute tuone nini kinakuja.
 
Back
Top Bottom