Mkuu wa Wilaya Hai, Ole Sabaya usikubali kutegeka

Kimetah

JF-Expert Member
May 8, 2013
1,049
188
Nimekumbuka Wimbo mmoja wa zamani kwenye kiitikio una maneno "Hilooo umejidai mbabe sana, leo umepigwa na kijana mdogo, aibu imekupata"

Pia, simulizi Moja ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere akiwaasa Watanzania wasisikilize kelele za watu bali waangalie lengo lao, alitoa mfano wa kijana mmoja mdogo ambaye alishinda vikwazo na kuchukua mke.

Hapa nakusudia kusema kwamba pale Jimbo la Hai maneno ya wimbo huo na simuliz ya Baba wa Taifa yametimia. Mkuu wa wilaya ya Hai aliteuliwa na Mh. Rais JPM:

> lengo kubwa na mahususi la Mh. Sabaya kufika wilaya ya Hai ni KUWALETEA MAENDELEO WATU WA HAI yakiambatana na KUTATUA KERO ZA HAI. Maendeleo hayo yameainishwa vizuri sana katika ILANI ya CCM 2015-2020.

> Pia kama kamisaa wa Chama cha Mapinduzi aliyekuzwa kwa kutumia mbinu zote, ni kuhakikisha jimbo la Hai linarudi mikonono mwa CCM.

SASA KIMETOKEA NINI?
1. Lengo mahususi la kuleta maendeleo Wilaya ya Hai limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kero zimetatuliwa.

2. Hili la kurudisha jimbo kwa CCM tayari limekaribia ni muda tu ndio unasubiriwa kwani watu wa Hai wameona kwa macho yao jitihada shirikishi za kufanya watu wanapata maendeleo.

NINI KIFANYIKE?
Mh. Lengai Ole Sabaya usisikilize kelele za hao watu watakupotosha kwenye lengo lako la kuwazawadia CCM jimbo. Una mbinu zote ulizokuzwanazo toka chipukizi mpaka UVCCM; hizo ndizo silaha tosha ya kuchukua jimbo. Chonde chonde usijeangalia nyuma ukageuka JIWE.

NAJUA HAI KAZI INAENDELEA
 
DC Ole Sabaya wa wilaya ya Hai ni mchapa kazi lakini kero za watu kuhusu Ardhi zinakwamishwa na afisa ardhi wa wilaya chini ya uongozi wa mkurugenzi kutumia utoaji wa hati za kumiliki Ardhi kama uchochoro wa kula rushwa!

Inashangaza kuona kuwa ofisi za Takukuru na ofisi za usalama wa taifa za wilaya ya Hai hawajawachukulia hatua wahusika kwenye idara ya Ardhi hapa Hai!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom