Wee upepo, akili yako umeiacha wapi? Huo ulikuwa ni mfano tu, na wala sikuwa namaanisha hivyo. Kwamba, yeye kateuliwa lakini hajui ni kwanini au kwa vigezo vipi kateuliwa, is that not stupidity?Mkuu kumbe ukuu wa Wilaya unapatikana kwa interview ya wazi? Unaijua katiba mkuu? Kumbe hata hujui ukuu wa wilaya unapatikanaje! Naona wewe unajua rabbish tu. Jishughulishe basi hata kidogo ili ujue ukuu huo unapatikanaje kisha uende kwenye tume ya katiba ili utusaidie kutoa mawazo ili tuje kupata wakuu wa wilaya kwa vigezo na interview za wazi!
Ndugu yangu nipo makini na uwezo ninao lakini ningeshauri hizi taarifa kabla ya kuchangia mada tuwe nasi tunajiridhisha kama ziko sahihi wengi wana post vitu ambavyo si vya kweli na hivyo kuonekana kana kwamba hatufai na wengi wetu tunashindwa kutoa ufafanuzi mfano hii taarifa nafahamu lengo la mtoa mada alitaka katika mkutano ule wa hadhara niamrishe watu wapige kura ya kumuondoa madarakani mwenyekiti lakini jiulinze ndugu yangu huo ni utaratibu wa mkutano wa kijiji ? Lakini pia amejichanganya kwa kudhani mimi nimemuondoa nilichofanya ni kuwasaidia ili baadaye waweze kutoa maamuzi sahihi,nawasilisha
Wee upepo, akili yako umeiacha wapi? Huo ulikuwa ni mfano tu, na wala sikuwa namaanisha hivyo. Kwamba, yeye kateuliwa lakini hajui ni kwanini au kwa vigezo vipi kateuliwa, is that not stupidity?
aa wapii!!!mnawatumikia wananchi kwa kukaa maofisini!!!..natambua hapo Kwasadala si mbali sana na Boma N'gombe yalipo makao makuu ya wilaya ya Hai ambapo ipo ofisi yako kama dc......Nachotaka kusema ni kwamba nyie ma dc wa JK mmechaguliwa kukidhi matakwa ya kisiasa zaidi ya kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi zao....na ndio sababu kila kukicha tunasikia mkitoa maamuzi ya ajabu ajabu kwenye kazi zenu.....wewe kama dc wa Hai(wilaya yangu)..Salama ndugu yangu tunawatumikia wananchi na wana haki ya kutuhoji,kutushambulia na pia kupata majibu sahihi
Nova si ulifanya usaili Mzee? Mbona lugha yako ngumu kumeza?
Dhaifu ni president wenu mliyemchagua kwa papara zenu peke yenu.Km umeshaniona kuwa president ahsante sana.Mlimchagua kwa sifa duni kama vile nakwenda oa zenj: kama ni handsome, mtu wa watu, naingia disco, anapenda u-miss na ujinga kama huo.Kila kundi lilikuwa na sifa za kijinga kama hizi kumchagua.Mbona hueleweki, ww ni Dhaifu, jipange upya unapoandika hbr. kalale ukiamka andika tena.
Nova report ipo wapi .Au ndio ndio ahadi ya kutorudi ktk hii thread ni kubwa kuliko kutatua tatizo la wananchi kwa staili ya wananchi na si ya magamba?
Dhaifu ni president wenu mliyemchagua kwa papara zenu peke yenu.Km umeshaniona kuwa president ahsante sana.Mlimchagua kwa sifa duni kama vile nakwenda oa zenj: kama ni handsome, mtu wa watu, naingia disco, anapenda u-miss na ujinga kama huo.Kila kundi lilikuwa na sifa za kijinga kama hizi kumchagua.
Nova sasa atuletee riport za kwasadala kama kweli ni mwadilifu.Otherwise tutaleta ztu halafu aje piga tumba kuwa kaonewa.
mkorakamili
Ndugu yangu moja sijamfukuza mtu madarakani ylakini pia sijaeleza nani kaiba pembejeo,ule ni mkutano wa hadhara kati ya wananchi wa kijiji cha kwasadala na mkuu wa wilaya, wananchi wale wana kero zao kibao za muda mrefu,lakini pia vikao vya vijiji vina sheria na kanuni zake zikiwemo namna ya kuviitisha, uendeshaji na jinsi ya kutoa maamuzi.
Masuala uliyoongelea bado ni tuhuma mfano la wizi wa pembejeo na mengine mengi yakiwemo ya kukuza maeneo ya ardhi na kadhalika yakiwahusu mwenyekiti wa kijiji na ofisa mtendaji wake.
Nilichofanya ndugu yangu ni kuwaweka nje ya ofisi viongozi hao ili wataalamu wangu watano ambao ni pamoja mwanasheria wa halmashauri, mkaguzi wa mahesabu,afisa ardhi na katibu tawala wa wilaya watumie muda wa siku Saba kutafuta ukweli wa tuhuma hizo na baada ya hapo tutaita mkutano wa kijiji utakaofuata taratibu na kanuni za kuitisha vikao va vijiji.
Uamuzi wa mwenyekiti utafikiwa na wananchi wenyewe na la mtendaji wa kijiji ni la mwajiri wake ambapo kiutaratibu ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya.
Kama kutakuwa na suala lolote la kijinai tutapeleka katika mamlaka husika, hayo ndiyo maamuzi yangu katika kikao kile ndugu yangu.
Mkuu wa wilaya.... Hiyo mwenyekiti angekua wa chadema ungeingilia kati?
Nova report ipo wapi .Au ndio ndio ahadi ya kutorudi ktk hii thread ni kubwa kuliko kutatua tatizo la wananchi kwa staili ya wananchi na si ya magamba?
ndugu yangu uliza, kwa matatizo na kero za wananchi nafanya kazi sana na wenyeviti na viongozi bila kujali itikadi zao za vyama kwa bahati mbaya mengi hayatangazwi na wengi hawamo humo ndani,lakini nikirudi kwenye swali lako kwa ufupi Sikutaka kuingia kwa undani kuelezea tatizo lililopo pale kwasadala,Ni kubwa na la muda mrefu na lingeweza kuleta hata umwagaji wa damu na ofisi ya kijiji ilifikia kufungwa hivyo kwa vyovyote vile ilikuwa lazima nichukuwe hatua,lakini la zaidi yule mwenyekiti wa kijiji ni wa ccm lakini kwa kukusaidia kama si mkazi wa hai hii post itakuchanganya sana,mwenyekiti wa ccm hai dr Uronu hajawahi kwenda pale kwa tatizo hili lakini hiyo siyo issue,kubwa ni kuwepo kwa tatizo,Nilichofanya ni kufuata taratibu na sheria za uendeshaji wa serikali za mitaa kuanzia vitongojini hadi kata na wananchi wameshafanya maamuzi yao katika mkutano wao uliofanyika juzi jumatatu.
mheahimuwa DC,nakuomba utembelee wilaya yako, najua ww n mchapa kaz, uspo fanya kaz utaaibika kama juzi halmashauri ilivyo aibika mbele ya mkuu wa Mkoa Gama kwenye kikao na waalimu.napenda kukumbusha uziangalie shule kongwe kama elyamungo na machame girlys.machame imeoza hata kwenye rank haipo tena,mkurugenzi,makange na Afsa taaluma wawajbike kuuacha uongozi ule pale ile hali umeshindwa ongoza shule na kuweka mikakati ya kufaulisha badala yake kuchonganisha waalimu na almashauri na kuwa hamisha.tafazali mkuu maslahi ya Mtu binafsi yasisababishe watoto wetu kupata sifuri. tembelea shule hii ongea na wanafunzi na waalimu uone uozo.hapoulipo fungua matokeo ujionee ya miaka mitatu mfululizo(09,10,2011).maytake shule kongwe kama machame wapewe wakina mama watu wazima na si sampuli ya materu, kashindwa shule.naomba kuwasilisha.
Mkuu wa wilaya.... Hiyo mwenyekiti angekua wa chadema ungeingilia kati?
sijui na sidhani kama matatizo ya wananchi pale kwasadala yanaweza kutatuliwa humo ndani ya jf,lakini pia nilisikitika sana kuniweka katika mazingira ambayo hayakuwa dhamira yangu ambayo ni kutaka kupata suluhu la kudumu la mgogoro ule,suala la magamba ama siyo magamba halina mantiki kwangu,kwa kifupi sana ndugu yangu nilishakamilisha utaratibu kwa kufuata sheria zinazosimamia uendeshaji wa serikali za mitaa katika ngazi za vitongoji na vijiji na wananchi kupitia mkutano wao wa kijiji uliofanyika juzi jumatatu wameshafanya maamuzi kwa kuwa wewe ni mwenyeji wa hai ni vyema kama ulivyoanzisha hii mada basi ungefuatilia kwa walioshiriki katika mkutano ule ambao ulimalizika saa mbili usiku
Mimi nilichoongelea ni Mwenyekiti wa CCM kufany ajaribio likagoma,akachukua polisi boma wengine wakagoma.Akamwita Nova ambaye kazi yake rasmi ni kulinda chama ktk wilaya yake.Otherwise sijui kazi nyingine kama zinamsaidia kwa lolote ku survive politically.
Huyu Jamaa kwa vile bado ana influence ktk media kaenda play kamikaze kwa staili yake.Sijasema kwa vile ni CCM ingawa this time CCM ndio wanachanganya office za serikali na utendaji wa magamba.Hata ingekuwa Chadema ningesema the same.