Mkuu wa wilaya Hai-Novatus Makunga kafanya alichoshindwa M/kit wa CCM Hai

Duuh,
Kumbe na mwenyewe yupo na hapa kakujibu,
Ingawa binafsi hata sijaelewa lugha uliyotumia nadhani sasa mtaelewana
Ukiandiak kiswahili fasaha, tutajua cha kuchangia, kwa sasa pambana na huyu DC mwenyewe

Walikuwepo waandishi wa habari wa magazeti naamini taarifa nzima inaelekea vizuri tu
 
Mkuu rekebisha bandiko lako la kwanza ili ueleweke,na pia achana na hizo lugha mbovu,yeye keshaonywa na members wengine na kawa mstaarab,licha ya kwamba ni wa magamba,lakini kama anajadiliana kwa hoja,JF haibagui,ni hoja kwa hoja.

Sasa anza kwa kurekebisha bandiko la kwanza,then ulete hoja kwa lugha ya kiungwana.
 

Ndugu yangu huu ni mjadala tujadili ili tueleweshane,Kama mwananchi wa kijiji cha kwasadala ni nyinyi wenye mamlaka ya mwisho ya hatma ya uongozi Kama ulikuwepo katika mkutano ule kauli hiyo nimeirudia zaidi ya mara tano cha msingi ebu tufute taratibu za mkutano mkuu wa kijiji.
 

Haya mushi kwa kuwa umenena miye sina la kujitetea hapo
 
Mkuu nova makunga sisi wengine hatuakuangalia taarifa ya habari na bahati mbaya mtoa mada naona katoa mada kwa kiarabu kama vile anaandika toka kulia kwenda kushoto. Hivyo basi tunashindwa kuelewa ni nini kilitokea. Ingekuwa vyema kama tungejua nini kilitokea nasi tukachangia tukiwa na uelewa. Pole naona unapita kwenye Tanuru la JF; vumilia ndio JF yetu hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Salama ndugu yangu tunawatumikia wananchi na wana haki ya kutuhoji,kutushambulia na pia kupata majibu sahihi

Hapo safi. Jibu kwa uungwana. Unajua ndani ya JF unaweza kujazwa upepo kisha ukajaa na kupoteza fahamu!
 

Hapo kwenye Red, unasema ni Mkutano wa Wananchi wa Kijiji cha Kwasadala na Mkuu wa Wilaya, Uliitishwa na nani na kwa kufuata taratibu zipi? Unazifahamu kweli taratibu za kuitisha mkutano wa Kijiji? Obvious huitishwa na wananchi wenyewe. Lakini pia wewe kama Mkuu wa Wilaya una mamlaka yapi ya kumsimamisha au hata kumuweka pembeni ya Ofisi Mwenyekiti wa Kijiji aliyechaguliwa na Wananchi? Kwa nini hukuwapa fursa Wananchi wenyewe kuamua la kufanya dhidi ya Mwenyekiti wao maana tayari walikuwa kwenye Mkutano? Wewe unaweza kumuweka pembeni au nje ya Ofisi Diwani eti kwa vile anatuhuma na kwamba unataka umchunguze? Mabaraza au Wazee wa Vijiji wapo? Kwa nini hukuwapa nafasi?

Nadhani bado kuna tatizo la Viongozi wa kisiasa kutambua mamlaka yao na zaidi kushindwa kutambua nguvu na nafasi ya mwananchi.

Maamuzi ya wewe kumuweka pembeni/nje ya ofisi Mwenyekiti aliyechaguliwa na wananchi ni makosa kiutendaji.Baada ya kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi ulipaswa kuwarudishia nguvu yao katika kuamua hatma ya Mwenyekiti wao, huwezi jua labda kwa kuwapa nafasi (nguvu yao Kikatiba na kisheria) wangeweza kabisa kufikia maamuzi ya pamoja na kulimaliza tatizo moja kwa moja. What if watu (wako) uliowapa kazi ya kumchunguza wakija na ripoti ya kumsafisha Mwenyekiti huyo na wakati huohuo Wananchi wamemchoka? Utang'ang'aniza aendelee kuwaongoza?
 
Napongeza alichofanya Makunga.
Kwa Sadala paliishakuwa shamba la Bibi.
Mkazi gani wa Kwasadala asiyekumbuka jinsi wajanja walivyokunywa gari (basi) la kijiji, mashine ya kusaga nafaka nk.
Mnakumbuka jinsi Shafii Alilu alivyopewa eneo la kijiji akajenga maduka na makazi yake.
Hongera Makunga
 

Ufafanuzi mzuri.
 
Muheshimiwa mkuu wa wilaya ,naomba uende na kule kambi ya raha ,kwa wasomali wanauza mashamba hovyohovyo baada ya lease yao kuisha, hakuna maeneo ya shule,hospital,viwanja vya michezo,simamia uwezo unao ,unafahamu baada ya moshi mjini ni HAI inayokuwa kwa kasi boresha miundombinu,TUIJENGE HAI KWA PAMOJA.
 

Hapa sasa ninaanza kuelewa....basi kama mambo yenyewe ni hayo basi hata mada zingine zitakazo letwa zitakua zina hitaji wahusika wajitokeze na kutuelewesha maana sio wote tunapata habari kamili especially watu walioko nje...
Pia ningependa kukuomba kama utapata muda hebu jitahidi uliweke sawa jambo hili kwa kutumia uzi mpya...Maana huenda ukawa sahihi lakini waleta mada wakatuchanganya na kuona kazi huifanyao ni bure kumbe upo sahihi...
Pia nakushukuru kwa kujaribu kufuatilia maoni ya watu na kuweka uwazi...
Hii ndo JF watu wanaelimishana...na kupeana ukweli...SO BIG UP kwa kujaribu kuliweka sawa..
 
Inapendeza kuona mkuu wa wilaya ''has guts'' kupita huku bila kujificha na kufafanua mambo.
 
heshima mbele mh nova

hongera sana kwa kujitokeza hapa JF na kujibu hoja, hata kama mleta hoja ametumia lugha ambayo pengine haijaeleweka kwa wengi na/au hata lugha isiyo ya kistaarabu, busara na hekima pamoja ukomavu wa uongozi huja na kuonekana unapojibu hoja husika kwa uwazi na utulivu. Usikubali uongozwe na hisia na hasira kwenye kujibu hoja zako na zaidi kwenye utendaji wako wa kazi. JF ni pa moto lakini taratibu utajenjwa hapa, utakomazwa, utafundishwa na mwisho wa siku utakuwa imara, hodari na mwenyewe elimu.

Sasa turudi kwenye mada: Pamoja na kwamba katika utekelezaji wa majukumu yako ya kazi, kwa namna yeyote ile hukupaswa kumuweka kiongozi aliyechaguliwa na watu pembeni unless wahusika waridhie wenyewe na tena wafuate taratibu zilizowekwa ya namna ya kumuwajibisha kiongozi wao. Kwa hivi natural justice itakuwepo na pia itaondoa uwezekano na kupinduana mara kwa mara na kuleta chaos katika jamii.

Kama kuna makosa ya jinai au hata matumizi mabaya ya ofisi yaliyofanywa na huyo mwenyekiti basi sheria zifuate mkondo wake. Lakini nionavyo mimi umeingilia uhuru na mamlaka wanakijiji bila 'ridhaa' yao, kwa sababu ulichofanya hakukuwa na consent yao. Kuwafanyia maamuzi wanakijiji, na huko ndio tunaita kubaka demokrasia.

Yawezekana motive yako pamoja na malengo yako ni mema lakini methodology uliyotumia kutatua tatizo inakosa nguvu ya kisheria na mantiki.

Tafakari tena juu ya hatua uliyochukua, kama kuna namna unaweza rectify mambo, which I believe ipo, nadhani fanya hivyo mkuu otherwise kukosea siyo tatizo, tatizo ni kukataa kurekesisha makosa.

MwanaJF WOWOWO amepose maswali na hoja za msingi sanagu. Kama una majibu tunaomba utupatie, pengine sisi hatuzijui hizo hizo kanuni na taratibu zilizopo za kuwaweka pembeni viongozi mbalimbali. Kama zipo tungependa kuzijua

ni hayo tu, nakutakia kila la kheri katika majukumu yako mkuu
 
Wewe jibu swali, mbona unakuwa kama sio kilaza vile? Umeulizwa vigezo vya kuteuliwa kuwa DC ni vipi, wewe unapiga blaa blaa tu! Hata unavyoandika sentensi hazileti maana na zenye maana hazina mantiki! Sasa nenda kwenye swali la msingi, wewe una vigezo vipi vilivyokufanya uteuliwe kuwa DC? Au ni kujipendekeza kwa wakuu wa Mabwepande? Maana unavyoandika na ku-argue inaonyesha kabisa wewe uliishia Form 4 yenye Div. IV ukaenda DSJ na baadaye ukaajiriwa na makampuni ya Iba Pole Pole (IPP) ukawa kuwadi wa Magamba full stop! Ama kweli ni nchi hii tu ndio utakuta AKILI NDOGO ZIKIONGOZA AKILI KUBWA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…