real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania limefanya mkutano na waandishi na kutoa tahadhari juu ya matangazo yanayodai kuna nafasi za kujiunga JKT au JWTZ.
Amesema kuanzia leo mtu akimfuata nakumuambia kuna mafunzo ya kujiunga na JKT au jeshi la ulinzi wa wananchi mtu huyo atakuwa ni tapeli,
Amesema jeshi haliwezi kuchukua watu mtaani kiholela na sasa utaratibu wa majeshi yote ni ikiwemo Zimamoto, Tanapa, Uhamiaji, ,Magereza, Polisi, na Jeshi la Ulinzi kunakuwa na kikao cha utumishi jeshini kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, na vyombo vyote huleta idadi ya watu wanaowahitaji kuwaajiri kisha majina kuchukuliwa na mkuu wa utumishi jeshini na kuyapeleka kwa mkuu wa jeshi la kujenga taifa.
Mkuu wa jeshi la kujenga taifa anaratibu utaratibu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwenda kwenye makambi ya JKT vyombo hivyo kwenda kuchukua vijana wanaohitajika na mkuu wa jeshi la kujenge taifa upotoshaji
Utaratibu wa kujiunga na JKT ni mpaka mkuu wa JKT atoe taarifa kupitia vyombo vya habari na kutoa utaratibu unaotakiwa kufuatwa.
Utaratibu wa kujiunga na JKT huanzia kwenye vijiji, kata tarafa kisha kufikia ngazi ya wilaya na majina kuchujwa na kupelekwa baadae kwenda mkoani kisha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huwachuja na watakaofaulu hupewa fomu ya kujaza.