Mkuu wa Shule ya Msingi Msakila aahidi kujiuzulu endapo Shule yake haitakuwemo katika kumi Bora

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
80,836
93,617
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Msakila, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi , Didas Makona ameaapa kuwa endapo shule yake ispokuwemo kwenye kumi bora ya shule zitakazoongoza Kitaifa katika matokeo ya Kitaifa ya kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka huu , atajiuzulu kwa hiyari wadhifa wake .

Akisisitiza kuwa itakuwa fedheha kubwa kwake na haoni sababu kwa nini shule yake hiyo ishindwe kuwemo kwenye orodha ya shule za msingi kumi bora katika matokeo ya Kitaifa ambayo yanatarajiwa kutangazwa baadae mwaka huu.

Mwalimu huyo alijigamba hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo , ofisi kwake shule hapo katika Mtaa wa Kawajense , Manispaa ya Mpanda ..

Nimekuwa Mwalimu Mkuu wa shule hii kwa miaka mitatu sasa nimewajengea misingi mizuri kielimu wanafunzi wanaosoma katika shule hii ambao wana nidhamu ya hali ya juu …..” alisisitiza .

Akifafanua alieleza kuwa mwaka 2012 ufaulu wa kuhitimu elimu ya msingi katika shule hiyo ulikuwa asilimia 52 .

“Mwaka 2013 nilihamia katika shule hii na ufaulu ulikuwa asilimia 76 mwaka 2014 asilimia 92 na mwaka jana ufaulu ulikuwa aslimia 100…… kwa matokeo hayo mwaka jana kimkoa shule hii ilishika nafasi ya kwanza huku kitaifa ilikuwa ya 200 “
alisisitiza

Alisisitiza haoni sababu itakayo ifanya shule hiyo kutokuwa kuwa kwenye kumi bora kutokana na jinsi ambavyo amewaandaa wanafunzi wake 76 waliohitimu elimu ya msingi mwaka huu..

Sababu nyingine aliitaja kuwa ni uwezo waliokuwa nao wanafunzi wake katika masomo ya Hisabati na Kingereza ambapo kwenye mitihani sita ya majaribio iliofanyika kimkoa robo ya wanafunzi 76 walipata alama A ya ufaulu , huku waliobaki wote walipata alam a B wanafunzi wake robo ya darasa wamekuwa wakipata alama B
ya ufaulu..

Chanzo: Katavi blog
 
Nimesoma hapo darasa la kwanza.... Kabla cjahama...
Wakat huo hata cjui nini Maana ya Engineering...

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng
 
Wana funzi shule za vijijini wana nidhamu na ndio maana ufaulu wao ni mkubwa

watoto wa mijini kazi kucheza na Ben ten
 
hii shule wako vizuri tangu zamani wakiongozwa na mwal. mwakasungura kaja huyu makona ndo imekuwa balaa tupu ni namba 1 mkoa na wilaya. nimesoma hapo pia.
 
Nimesoma hapo darasa la kwanza.... Kabla cjahama...
Wakat huo hata cjui nini Maana ya Engineering...

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng
nimesoma hapo pia, kitambo ukiwa bado eneo la kanisa.kuna darasa lilikuwa linaitwa MV unalipata.
 
Amejiuzuru au bado? Maana hata 50 bora naona hayupo. Aliiba pepa huyo kumbe walimu nao vilaza baadhi kama waliwandikia watoto majibu lkn wamekosa nn taswira kwa walimu hao?
 
Back
Top Bottom