Mkuu wa shule anapinga matumizi ya English shuleni,wakati watoto wake wote wapo E.Medium

shonkoso

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
671
1,427
Tulikuwa na kikao Jana cha kufungua shule, staff nzima tukaazimia kuwa kama Sera inavyoeleza kwa sasa kuwa the medium of instructions kwa elimu ya secondary ni English.

Kuwa matangazo yote na maelezo muhimu yatolewe kwa English, kwani wanafunzi tayari wanauelewa mzuri wa kiswahili,

Sasa siyo vibaya wakijifunza na lugha nyingine kwa ajili ya matumizi mengine,

Mkuu wetu alibisha sana bila aibu coz yeye huwa ndo no 1 kuongea Kiswahili parade, mshangao wangu unakuja ana watoto wanne wote wapo English medium schools.

Najiuliza ana nia ya dhati kwa kile anachokitetea?
 
mkuu wa shule anaetajwa inaonekana lugha ya kiingereza kwake ni tatizo ama la kutojifunza na kuielewa au kutoisoma kabisa. kufika alipo inawezekana alibebwa. uhakiki wa vyeti vyake ni muhimu. pia ni wakati wa kuwa na wasomi kuanzia pg kwa wakuu wa shule za sec.
 
Wakuu wengi wa shule ni janga kwa Elimu. Inakuwaje lugha ya kufundishia ni kiingereza na Mkuu wa taasisi hajui lugha hiyo. Yaani sielewi hata nchi hii inataka nini kwenye Elimu ?Na mtu huyu ndo anapewa kila aina ya offer na serikali kila mwaka ,kila mwaka ndo msimaz Mkuu wa mitihani, posho ya madaraka 250000/-kila mwezi. Na wengi darasani hawaingii yaani in short ni mweupe kichwani kuwa passive kwenye mambo yahusuyo uboreshaji ndo kumewafikisha ktk nafasi hizo_One day we shall decide what we need to teach.
 
Back
Top Bottom