Mkuu wa mkoa, wilaya wamkimbia Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa mkoa, wilaya wamkimbia Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 12, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Norman Sigalla, juzi walimkimbia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, katika shughuli za upandaji miti na uzinduzi wa usafi wa mji mdogo wa Bomang’ombe yaliko makao makuu ya wilaya, ikiwa ni sehemu ya sherehe za jubilee ya miaka 50 ya kuzaliwa kwa Mbowe. Viongozi hao wakuu wa serikali, awali walikubali na kuthibitisha kushiriki tukio hilo la kimaendeleo juzi, lakini wote wakatoweka muda mfupi kabla ya kuanza kwa shughuli za upandaji miti na usafi.

  Tukio hilo lililoonekana kuwasononesha wananchi wengi waliojitokeza katika shughuli hizo, lilimsikitisha Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai (CHADEMA), aliyewataka viongozi na watendaji wa serikali nchini kuacha kuchanganya shughuli za maendeleo ya wananchi na masuala ya siasa na waelewe kuwa nafasi hizo wamepewa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi.
  Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema kuwa suala la utunzaji wa mazingira halina itikadi kwani linawanufaisha wananchi wote, hivyo inashangaza kwa viongozi hao kukwepa kushiriki.

  Mbowe aliandaa na kuratibu zoezi hilo linalogharimu sh milioni 300, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya kuzaliwa kwake, jumla ya miti 10,000 ilipandwa kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Bomang’ombe pamoja na kugawa vifaa vya usafi na trekta lenye tela kwa ajili ya kukusanyia taka. “Nadhani huu ni mkakati wa makusudi kujaribu kunidhoofisha, wanafikiri wakishiriki watanijenga kisiasa au wanahisi wataniongezea umaarufu, jambo ambalo si sahihi kwani Mbowe kama ni umaarufu ninao wa kutosha wala siwezi kuwategemea wao wanijenge,” alisema Mbowe. Hata hivyo, mbunge huyo alielezea kupata faraja kutokana na mwitikio wa wananchi waliojitokeza kushiriki kupanda miti na kusafisha mji na kuongeza kuwa anaamini malengo ya kuufanya mji wa Bomang’ombe kuwa safi yatafanikiwa huku akiahidi kukabiliana na yeyote atakayejaribu kurejesha nyuma harakati hizo.


  Akihojiwa na Tanzania Daima juu ya hatua yake ya kutoonekana katika shughuli hizo dakika za mwisho, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Gama, alikiri kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo lakini alishindwa kuhudhuria baada ya kupata maelezo ya kitaifa yakimtaka akapokee Mwenge wa Uhuru uliokuwa ukishuka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro ulikopandishwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru. Alisema kuwa kutokana na nia njema aliyokuwa nayo, baada ya kupata udhuru huo alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Hai, Sigalla, akamwakilishe kwenye hafla hiyo lakini naye alishindwa baada ya muda mfupi kabla ya kuanza kwa shughuli hizo juzi asubuhi kuitwa mjini Dodoma.


  Juhudi za kumpata Sigalla kupitia simu yake ya kiganjani kujua, ikiwa baada ya kupata udhuru alimwagiza kiongozi mwingine akamwakilishe ziligonga mwamba baada ya simu hiyo kuita muda mrefu bila kupokewa. Zoezi hilo la kupanda miti na kufanya usafi kwenye dampo la Green Belt liliwashirikisha wananchi wa Wilaya ya Hai, wabunge 15 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Maasei na Meya wa Manispaa ya Moshi, Jafar Michael, pamoja na baadhi ya madiwani kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

  Aidha, Mbowe aliongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Lambo uliopo Kijiji cha Nshara ambapo jumla ya sh milioni 30 zilipatikana katika hafla hiyo iliyotanguliwa na ibada iliyoongozwa na Sheikh Yusuf Lyasenga, ambapo mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Bakwata mkoani Kilimanjaro, Sheikh Rashid Mallya.


  Mbunge huyo wa Hai kwa vipindi viwili tofauti alichangia sh milioni tano, wakati kada maarufu wa CCM , Mustafa Sabodo, ambaye hakuweza kushiriki shughuli hiyo kwa maelezo kuwa yuko India kwa matibabu alichangia sh milioni tano. Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alichangia sh milioni 4.5 ikiwa ni gharama ya mazulia. Wengine waliochangia ni mbunge wa viti maalumu, Leticia Nyerere sh milioni moja, huku wabunge wengine kwa pamoja wakichangia sh milioni tano na kaka wa mbunge huyo wa Hai, Twalib Mbowe, akichangia sh milioni tano.


  Mbowe alizindua ofisi ya Taasisi ya Kusimamia Mpango wa Maendeleo ya Wilaya ya Hai ( HAKIDI) ambapo kupitia taasisi hiyo anatarajia kutengeneza ajira zaidi ya 5,000 katika kipindi cha miaka mitano kwenye sekta ya utalii na kilimo. Alisema kuwa tayari HAKIDI imekwisha kutoa mafunzo kwa vijana 450 kwenye sekta ya utalii, ambao walipewa ujuzi katika upandishaji wageni Mlima Kilimanjaro na tayari 200 wamekwisha kupata ajira kwenye makampuni mbalimbali ya uwakala wa utalii.
   
 2. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ccm wameoza..wanajistukia kama wamevaa Pichu mbichi.
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  hiyo kali kweli na ya mwaka bila shaka
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wangekuwa wajinga kama wangehudhuria? Jubilee Ya mbowe? who is mbowe by the way? Narudia kusema hivi, wangekuwa wajinga wangehudhuria, full stop.
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  ukiachia Elimu ya Uraia ambayo ilibidi watu wote wapewe kabla ya kuingia kwenye mfumo wa vyama kingine kikubwa zaidi
  ni KATIBA ambayo inawafanya VIONGOZI kuwajibika kwa WALIOWATEUA ZAIDI kuliko kwa WANANCHI kama mkuu wa mkoa
  angekuwa anachaguliwa mojamoja na wananchi lazima angeudhulia kwa sababu mabosi wake wengi wameudhulia nao ni wananchi. moja kati ya Badiliko kubwa sana la katiba tulaliitaji ni kutengeneza mfumo ambao viongozi wengi na hasa taasisi
  nyingi za enforcement kuwajibika kwa Bunge badala ya mtu mmoja. WE SHOULD GET RID OF SYSTEM OF HAVING UNELECTED
  LEADERS WHO ACCOUNTABLE BASICALLY NO ONE. LEADERS MUST BE ANSWEREABLE TO THE PEOPLE.
   
 6. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  And who are u any way to dictate their attendance, these guys are fool's to run away from obligations, period!!!!!!!!

   
 7. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivyo huu mwenge una faida gani?
   
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  What a foolish comment! Duh.!? I wish mods could see where you were during the above comment. I can bet it was in sewarage system. Mavi....!.
   
 9. Rocket

  Rocket Senior Member

  #9
  Dec 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Viongozi wa serikali acheni siasa mjali mambo ya maendeleo
   
 10. h

  hans79 JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  aliyepanda miti na alifanya sherehe za urembo uwanja wa uhuru a k a tshs 46 b, who is better? kufiri kwa makario kazi kweli kweli
   
 11. h

  hans79 JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  wasifu wa elimuyo?
   
 12. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kutumia 300Mil kwa shughuli za maendeleo hasa usafi na kupanda miti kwa mazingira ya kilimanjaro ni bonge la idea kuliko aliyetumia 64bil kwa sherehe za uhuru. Big up Mh. Mbowe kwa harakati zako wewe ni kama mvua ukiamua kunyesha unanyesha hakuna wa kukuzuia kufanya maendeleo hilo hata ccm na utaahira wao wanalitambua .
   
 13. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #13
  Dec 12, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kaaaaziiiii,kwelikweli
   
 14. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Watu Wenye kutumia Ubongo kufikiri utawaona- wanapanda miti na kufanya usafi ili afya iimarike kwa 300miloni tu; ;Wenye kutumia Masaburi kufikiria utawaona Wanakusanyika uwanjani kuangalia gwaride, ngoma, silaha na kukimbiza mwenge kisha wanalipana posho na kuandika Kuwa tumetumia bill 64.
   
 15. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Songa mbele zaidi Mbowe.
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Tangu lini kunguru akaruka na njiwa kwani hata kusogeleana hawasogeleani
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Tangu lini kunguru akaruka na njiwa kwani hata kusogeleana hawasogeleani. Kungu mwenyewe kwanza ni mchafu na anakula uchafu siku zote
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Angalia ulivyo mvivu wakufikiria, wamealikwa kupanda miti ili kutunza mazingira wao mamehi ni kwenda kuwaumbua mafisadi sijui wakaanza mbele
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa umenena ukweli mtupu na nadhani umechambua kwa makini sana hii habari heko kwa hilo
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  We unadhani wakiacha kuukimbiza magamba watakula wapi na kueneza siasa zao uchwara?
   
Loading...