Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,337
- 120,836
Mkoa mpya wa Songwe umekuwa ukitumia shilingi Milioni 250 kwa mwaka kwa ununuzi wa makaratasi.
Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luteni Mstaafu Chiku Galawa, amepiga marufuku matumizi hayo na badala yake mkoa wake utatumia mfumo wa Serikali Mtandao, hivyo machapisho yote yatafanyika kwa I CT, na mawasiliano yote ya machapisho yatafanywa online kupitia barua pepe, hivyo hakuna tena haja ya kuchapa kwenye makaratasi.
Chiku Galawa ameyasema hayo, katika ziara ya ujumbe mzito kutoka nchini Sweden ukiongozwa na balizi wa Sweden nchini, kutembelea mkoa huo kwa mwaliko wa Taasisi ya TradeMark East Africa.
Akifafanua zaidi, Mkuu wa mkoa amesema, wanaoongoza kwa matumizi ya karatasi ni mabaraza ya madiwani ambao wanachapiwa makabrasha na makabrasha, hivyo ameanza nao, kila mjumbe wa baraza la madiwani, anamiliki IPad or smart phone ambayo iko connected na Internet ya Halotel kupitia mkonga wa taifa wa mawasiliano uliotapakaa nchi nzima, hivyo kila kitu ni kwa mtandao.
Hata hivyo, amesema taarifa maalum za kiserikali zikiwemo taarifa za vikao vya ulinzi na usalama vitaendelea kufuata taratibu za kawaida za kiserikali na kiusalama na taarifa nyingine zote za kawaida za serikali (not confidential) zitasambazwa kupitia wakala wa E-government ambao uko salama.
Akiuzungumzia mkoa wake wa Songwe ni mkoa tajiri sana, wana kila aina ya rasilimali yakiwe madini mbalimbali, udongo wenye rutuba na mvua za kutosha ila watu wake ni masikini wa kutupwa kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto kuu ya ukosefu wa umeme wa kutosha.
Ujumbe huo umeongozwa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania na umejumuisha Mkurugenzi wa TradeMark East Africa tawi la Tanzania, John Ulanga, Ofisa wa Juu wa TradeMark Tanzania, Israel Sekirasa.
Ujumbe kutoka nchini Sweden ni Karin Olofsdotter, Director-General for Trade, Ministry for Foreign Affairs (MFA), Sweden, Johannes Oljelund, Director-General for International Development Cooperation, MFA, Anna Ryott, Managing Director, Swedfund International AB na Bengt Carlsson, Ambassador, Africa Department, MFA
Wengine ni Margareta Brisman, Deputy Director, Africa Department, MFA, Hans Daag, Special Advisor, Department for the Promotion of Sweden, Trade and CSR, MFA, Stefan Falk, Special Advisor, Department for International Development Cooperation, MFA, Hanna Lambert, Deputy Director, Office of the Director-General for International Development Cooperation, MFA, Karin Kronhöffer, Director Strategy and Communication, Swedfund International AB, na Sonia Albarello, Special Advisor, Department for Trade and Policy Developments, National Board of Trade.
The essence ya bandiko hili.
Zaidi ya kutoa info, hii maana yake Shilingi milioni 250 ambazo zilikuwa ziingie kwenye mzunguko wa pesa, mkoani Songwe, sasa hazitaingia.
Hiyo ni ya kwenye makaratasi tuu! . Akibana na posho za vikao, safari, mikutano, semina, warsha na makongamano, akifuatilia manunuzi yote ya umma mkoani kwake, hayo yakifanyika, hali ya mzunguko wa pesa mkoani humo itakuwaje?.
Mkiona bar haziuzi, nyumba ndogo zinakuwa abandoned, circulation ya pesa ni ndogo, mtaelewa ni kwa nini watu wanalalamika maisha magumu.
Paskali