Mkuu wa Mkoa wa Lindi huu ushuru wa taka tunaolipa mbona hatupewi risiti hela inafika yote kunako husika?

Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
4,911
3,080
Lindi mjini kila nyumba kila duka wananchi wanatozwa ushuru wa taka kumekuwa na utaratibu wa wananchi kutozwa ushuru kwa ajili ya usafi na utaratibu huo binafsi naona haujazingatia viwango kwani wengine wanatozwa fedha nyingi kuliko uhalisia

Nyumba ya wapangaji kila chumba shiling Elfu 2000 kaya moja Wengine wanatozwa
shiling 3000 kwa mwezi.

Maduka ya reja reja shiling 5000 maduka ya jumla yanaouza unga wa sembe Shiling Elfu 10,000 mbaya zaidi unatozwa fedha na kuandikwa jina lakini haupewi Risit.

Usafi ni muhimu Ila hapo kwenye viwango kuna uonevu watu hawakatai kulipa ghlama za usafi halafu kwa nini wanaotoza ushuru huo hawatoi Risit na Mheshimiwa Rais alishasema ukiuza toa Risit ukinunua toa Risit kodi ushuru wowote unaolipa dai Risit imekaaje hii?

Wengine wanatozwa ushuru mkubwa mfano mtu anaeuza jumla unga wa sembe afungui mfuko yeye nauza kwa kiroba anazalisha uchafu gani kiasi cha kutozwa shilling 10,000 kwa mwezi?
 
Taka zinaondolewa au haziondolewi?

Unaponunua kitu au kuuza kitu dai risiti.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom