Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera amezindua mradi wa maji Katavi

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019
Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Chamalendi kata ya Chamalendi Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe wilayani Mlele.

Mradi huo wenye thamani ya Tsh 402,600,000/= umeshuhudiwa na wananchi wa eneo hilo ambapo mradi huu utahudumia wananchi zaidi ya 10,000 Katika kata hiyo ya chamalendi.

Mkuu wa mkoa Homera amempongeza waziri wa Maji Prof Makame Mnyaa Mbarawa kwa usimamizi wa karibu wa miradi ya maji mkoani Katavi na kupelekea kutekelezwa kwa asilimia zaidi ya 99.
Mkuu wa wilaya hiyo ya Mlele Mhe. Rachel Kasanda amewataka wananchi hao kuutunza Mradi huo kwa kutumia vyema fedha za michango ya watumia maji ili mabomba yakiharibika waweze kukarabati na kuongeza vioski vingine vya kuchotea maji kutoka 20 na kuongeza vingine zaidi.
1154748
1154749
 
Back
Top Bottom