Mkuu wa Mkoa wa Iringa hajui Sheria

Mkuu wa Mkoa wa Iringa hajui Sheria

Kuntakint

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,767
Reaction score
1,526
Nimesikiliza nakuona video ya Mkutano wa Hapi na wanaringa. Magufuli anaipeleka nchi pabaya. Hawezi kuwapa vitoto ukuu wa mkoa au wilaya, watoto ambao hawajielewi wala hawajui sheria inasemaje. Hapi kamweka Diwani wa CHADEMA ndani eti kwasababu ya kuvunja nyumba ya mwanaccm.

Nimuulize Hapi je huyu mwanaccm nyumba yake iliyovunjwa ilijengwa ndani ya hifadhi. Huyo aliyevunjiwa wala siyo nyumba kwani ilikuwa bado inajengwa. Mwenyewe akasema ilikuwa hata aijawekwa paa.

Manispaa wanao uwezo wa kubomoa nyumba yoyote hata likiwa imeisha kama atakuwa ajafuata sheria. Halafu huyu Diwani hana mgambo, mgambo ni wa manispaa kwahiyo nyumba ilivunjwa na MANISPAA YA IRINGA SIYO DIWANI WA CHADEMA.

Halafu kwanini alikuwa hataki kumpa nafasi diwani nae aeleze jinsi ilivyokuwa. Yaani yote haya kwasababu manispaa inaongozwa na Opposition. Magufuli anaiangamiza nchi.

Hivi huyu Hapi ni mtoto wa Warioba, kama ni wake basi hapa Warioba aliteleza au alipakaziwa. Hizi co akili ya warioba, mara nyingi mtoto hurithi matendo au akili.
 
Umemsikiliza lakini hujamuelewa,umeamua kuwa shabiki,kasikileze tena kwa umakini wote ,kuanzia maswali ya RC Hapi,viongozi wa idara mbalimbali waliotoa maelezo yao pale kwenye panel.
Sema jamaa alikua mkali sana
 
Nimeiangalia ile video..niliyogundua ni kwamba. Yule mama hakupewa mda wa kujieleza.. halafu kuna yule kaka ni kama anachuki naye.. yaani alimpondea mpaka basi.
Lakini yule mama alijieleza vizuri kuwa yeye hajavunja nyumba na yule mwenye nyumba alishapewa kiwanja kingine ili ahame kwa utaratibu.
Mwisho yule mama alisema yuko tayari kuwajibika.
NAAMINI IGEKUWA NCHI ZA WENZETU HUYU MAMA KAMA AKIWA HANA MAKOSA KIUKWELI ANATAKIWA KUMSHITAKI MKUU WA MKOA
HAPI ALISEMA YEYE NI MTU HATARI SANA NA USIMCHEZEE
 
Umemsikiliza lakini hujamuelewa,umeamua kuwa shabiki,kasikileze tena kwa umakini wote ,kuanzia maswali ya RC Hapi,viongozi wa idara mbalimbali waliotoa maelezo yao pale kwenye panel.
Sema jamaa alikua mkali sana
Wewe uligundua nini pale baada ya kuangalia
 
Wasiwasi wangu historia ya Dr Kleruu na Mzee wa kihehe Mwamwindi isijirudie.
Unaweza kuta Hapi haijui historia hiyo maana alikuwa hajazaliwa na hasomi

Na kweli unajua sisi wabantu tu waoga sana ila hawa ndugu zetu Narcotic sio wa kuchezea kabisa kama wanaweza kujinyonga na ukichunguza wanaojinyonga wengi ni hawa Narcotic kama wahehe, masai, wambulu, wanyakyusa sio wa mchezo mchezo. Subirini ngoja siku ajichanganye akutane na kisirani mwisho arudishwe kama Kleruu kwenye mfuko wa rambo
 
Back
Top Bottom