CDM wameandamana, wamefanya mikutano na kutoa elimu ya urai jinsi ya kuitetea Nchi yetu juu ya dhuluma inayofanywa na CCM wakaonekana wachochezi na wapenda fujo, lakini ukweli unabaki kuwa hali mbaya ya kipato cha mwananchi mmoja mmoja nayo pia inasababisha vurugu kama hizi, kwa wenzetu wa Zanzibar, wao muungano bado hawaridhiki nao, lakini kwa vile CCM wanajua wanacholinda kwenye muungano ndio maana hawataki hata kuuongelea wala kusikia mtu akiukosoa.
Mawazo yangu yananiambia adui anayefanya maisha yetu yawe magumu hata kushawishiwa kirahisi kujiingiza katika fujo za kijinga namna hii si makanisa wala wakristo ni SERIKALI YA CCM, fikirieni tena na tena, wanachofanya CDM katika M4C si kuchochea vurugu ni kwa ajili ya ukombozi wa Taifa hili.
Kwa kipindi kirefu baadhi ya watu wamedhani kwa kuwa na kiongozi Muislamu basi maisha ya Waislamu yatabadilika ghafla, haya sasa Rais, Makamu,IGP na mawaziri kibao, huko Zanzibar ndio usiseme karibu wote waislamu lakini maisha yako vilevile na yatabaki hivyo hivyo kama KIRUSI CCM hakitaondoka madarakani.
TUACHE UDINI, TUJIUNGE PAMOJA, TUILILIE NA KUIJENGA UPYA NCHI YETU......MUNGU IBARIKI TANZANIA