Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda akwaruzana na Fatuma Karume

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Kauli ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kabla ya mchezo kati ya Taifa stars na Kenya:
"Taifa Stars ni Mali ya Serikali, inatekeleza ilani ya CCM" huenda ndio inasababisha baadhi ya watu kufurahia Kipigo cha Taifa Stars (3-2) dhidi ya Timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ huku wengine wakihuzunika.

Kumeibuka vita mpya ya maneno kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Hamasa wa Taifa Stars na aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) Fatma Karume.

Fatma Karume alianza kuandika kwenye Twitter:
“Paul Makonda arudi tu. Maana yeye kukaa Misri haisaidii kitu,”

Makonda amejibu: “Tulia wewe, hujanilipia nauli.”

Fatma Karume akaongeza tena: “Tulia jina la Naibu Spika sio langu. Ninaitwa Fatma Amani Karume. Jina langu lakuzaliwa nililopewa kwenya Birth Certificate, sina jengine. Wewe una majina mangapi? Acha kuomba omba nauli kwa kiherehere. This city does not belong to you. Umelikuta na utaliacha. Take a chill pill!”

Screenshot_20190629-105621.png

Screenshot_20190629-105753.png

Screenshot_20190629-105833.png
 
hanaga kazi ya kufanya bora aende akajiuze tu buguruni pale watu wamleeeeee
Moja ya kazi muhimu ndiyo hii anaifanya ya kumpa za USO Makonda. Kazi ambayo wapo wanaume wenye vyeo vya juu wanashindwa.
Waziri mkuu anashindwa kumkemea Makonda, Spika hawezi hata kumtaja anabaki anazunguka zunguka hata na Jafo hawezi.
Hongera Fatma kwa kazi nzuri
 
Back
Top Bottom