Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amesema anafuatilia madai kuwa kuna taarifa za Shule ya Msingi Nyanga English Medium kukiuka taratibu za udahili na kwamba kuna mazingira ya kupeana nafasi ya Mwanafunzi kusoma hapo kwa njia ya “kujuana”.
Kusoma hoja ya awali, bofya hapa ~ Kuna mazingira ya ukiukwaji wa taratibu za udahili kwa Shule ya Nyanza English Medium (Mwanza)
RC Mtanda amesema hayo katika taarifa ya Mwanachama wa JamiiForums.com iliyochapishwa kwenye Ukurasa wa Instagram ambapo amesema “Nitafuatilia ukweli wa suala hili, tutatoa taarifa” wakati akimjibu Mwananchi mwingine ambaye alihoji kuhusu suala hilo kwenye sehemu ya maoni.
Wakati huohuo, Mwananchi mwingine naye akatoa maoni yake katika ukurasa huo kwa kuandika:
“Hili halina ubishi mimi mwenyewe nilienda ilikuwa siku ya Alhamis nikaambiwa muda wa kuchukua form umeisha jana yake, cha kushangaza baada kama ya wiki mbili jirani yangu akaniuliza nikamwambia walisema nilichelewa lakini kwake ikawa tofauti.
“Akasema yeye alienda akaambiwa aende Jumatatu ya wiki inayofuata, kilichofuata mwanaye anasoma hapo hadi leo licha ya kuwa alichelewa wiki mbili ila mimi nilipishana siku moja tu nikaambiwa nafasi zimejaa.”