Mkuu wa Mkoa apigwa kombora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Mkoa apigwa kombora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Ni kwa harakati za kusaka jimbo la uchaguzi
  [​IMG] Pia adaiwa kuwamwagia misaada kibao
  [​IMG] Mwenyewe adai yuko gizani  [​IMG]
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro.  Wakati Rais Jakaya Kikwete akiwa ametia saini muswada wa sheria ya gharama za uchaguzi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro anadaiwa kuikiuka kwa kuanza kampeni zinazodaiwa kuhusisha ugawaji wa misaada, zikiwemo fedha.
  Kandoro anadaiwa kuingia katika utata huo akihusishwa na mchakato wa kuhakikisha anachaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Kalenga lililopo Iringa Vijijini.
  Jimbo hilo hivi sasa linashikiliwa na Stephen Galinoma ambaye hata hivyo, alishatangaza kutogombea tena.
  Mbali ya kutajwa kutoa misaada mbalimbali kwa wananchi wa jimbo hilo yenye lengo la kuwashawishi wampigie kura wakati ukifika, Kandoro anadaiwa kuwa amekuwa akiwatumia watu mbalimbali ambao hukodi pikipiki na kuzunguka kijiji kwa kijiji ili kumnadi.
  Hata hivyo, Kandoro mwenyewe amekanusha vikali madai hayo na kueleza kuwa ni mbinu za kumchafua kisiasa kwa kuwa amekwishaonyesha nia ya kuwania jimbo hilo.
  Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza anadaiwa kutumia fedha huku akiwa ametengeneza mtandao wa vijana ambao wamekuwa wakipita vijijini kumnadi.
  Habari hizo zimebainika siku chache baada ya watu wanaodaiwa kulipwa na Kandoro kufanya kazi hiyo kupata ajali ya pikipiki karibu na kijiji cha Ugwachanya na kujeruhiwa vibaya wakati wakitoka katika kijiji cha Magulilwa kwa lengo hilo.
  Watu hao ambao walipata ajali mwanzoni mwa Aprili, mwaka huu, ni Anitha Kindole aliyekuwa amekodi pikipiki ya Eliah Mwakalembusye ambao siku hiyo, walipita karibu vijiji 10, ikiwemo Magulilwa, Ng’enza, Mlolo, Ilangi na Banawanu kwa lengo hilo.
  Uchunguzi unaonyesha kuwa Kindole alikaririwa akiwaeleza wananchi mbalimbali aliokutana nao kwamba wamchangue Kandoro kwani ndiye anayefaa kwa Jimbo la Kalenga kwa sasa kutokana na kutoa misaada mingi, ikiwemo mabati kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya madarasa kwenye shule mbalimbali jimboni humo.
  Akizungumza kwa njia ya simu, Kindole ambaye alijeruhiwa kwenye unyayo na pikipiki hiyo na kulazwa katika hospitali ya misheni ya Ipamba, alikanusha kukodiwa na Kandoro.
  Alisema yeye ni mratibu wa wilaya wa shughuli za Village Community Bank (Vicoba) na kwamba siku hiyo alikuwa na kazi ya kuhamasisha wananchi kujiunga na benki hizo za vijijini.
  Hata hivyo, alikejeli kuwa yeye hawezi kumnadi Kandoro kwa kuwa mwenyewe (Kandoro) alishajinadi muda mrefu kwa kazi alizofanya jimboni humo na kwamba ni suala la wakati tu kabla hajasimikwa rasmi kuwa mbunge wa Kalenga.
  Kwa upande wake, Mwakalembusye ambaye naye aliumia vibaya goti la kulia alithibitisha pikipiki yake kutumika, lakini alisema si vyema kuyazungumza yaliyokuwa yakizungumzwa na Kindole anapokutana na watu kwa kuwa yeye (Mwakalembusye) ni mfanyabiashara tu na alichokuwa anafanya ni kumpeleka Kindole kila alikotaka kwenda.
  “Hivi ninapozungumza nawe nipo wapi? niko Mwanza na sijawahi kufika huko hata siku moja, tusianze kuchafuana,” alisema Kandoro alipohojiwa kwa njia ya simu.
  “Watu walioanza kampeni kabla ya muda unawafahamu, wanaogawa vitenge kwa wananchi, fedha, mipira, jezi na vitu vingine vingi unawafahamu,…eeh ndugu yangu, mimi niko huku Mwanza, huko (Iringa) sijafika,” aliongeza Kandoro.
  Kuhusu watu wanaopita kila kijiji kumnadi, Kandoro hakujibu chochote bali alisema: “Ukishatangaza nia (ya kuwania ubunge) huwezi kuwaziba mdomo watu wasiseme wanavyojisikia.”
  Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Luciano Mbossa, alisema hana taarifa za Kandoro kuanza kampeni, lakini akaonya kuwa yeyote anayefanya hivyo wasilaumiane mbele ya safari.
  Uteuzi unatarajiwa kuanza mwishoni mwa Julai, mwaka huu, ukitanguliwa na uchukuaji fomu za kuwania nafasi hizo na mchakato huo utaanza baada ya Bunge la sasa kuvunjwa.
  Kwa mara ya kwanza, uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika chini ya udhibiti wa sheria mpya ya Gharama za Uchaguzi iliyotungwa kwa lengo la kudhibiti vitendo vya rushwa na matumizi makubwa ya fedha.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. G

  Genda Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais, fukuza kazi huyu mtu wako (Mkuu wa Mkoa), kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,827
  Trophy Points: 280

  ahhhhh! ana ubavu wa kufukuza mtu?
   
Loading...