mkuu wa kaya, unayaona haya? funguka tuinusuru nchi!

Mangaline

JF-Expert Member
May 19, 2012
1,045
221
Katika hali isiyo ya kawaida, madaktari wameamua wao wenyewe, kuwa walinzi wa kamanda wao dr. uli. Hali hii inamaanisha kuwa madaktari hawa, hawana imani na jeshi la polisi, kwani hawaamini kuwa ulinzi wa polisi, waweza kuwa salama kwa kamanda wao. Kukosekana kwa imani ya madaktari kwa chombo halali cha usalama wa raia, kinazidi kujenga chuki kati ya makundi haya mawili. wakati huo huo, jeshi la polisi, linaendelea kuwa chombo cha dola cha kupiga, kunyanyasa, na kutesa raia.
Hali hii, inaweza kupelekea madaktari kutumia taaluma yao katika vita hii chafu. Hali ikifikia hapo, nchi inakosa uhalali wa kuwa dola.

WAZO LANGU:-
Mheshimiwa mkuu wa kaya, katika hali hii, iko haja ya kuvunja ukimya, utoe sauti angalau ya kupoza machungu ya jamii, la sivyo, magumu yakitokea, mimi na wewe, hatucheka wala kufurahia matokeo yake. Tafadhali mkuu, funguka.
"MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA"
 
Nashangaa kitu kama hiki rais amekaa kimya ndo maana tunaanza kufikiria kua they r involved
 
Amechilax kama vile hayupo nafikiri hapo alipo anesema ni mawimbi tu yatatulia
 
"Ni upepo tu unapita".Watanzania nas tufunguke kwani hatuna Rais,ni kiraka tu anasubiri NEC ya ccm wamushauri ya kutudanyanya ndo aanze kukenua meno yake,subiri mwisho mwezi atayoongea na wazee wa CCM drsm hana jipya!!!
Yaan ni bahati mbaya kua na rais kama JK msimamo wake ni sifuri.
 
Ni kweli unayosema labda amechoka na safari,naikumbuka ile message isemayo 'tell my people to continue with the struggle as my blood will nourish the tree that will bear the fruit of freedom'aliyoitoa solohmon mahlangu-mazimbu mpigania uhuru wa africa kusini aliyeuwawa kikatili wakati akipigania uhuru na mpaka sasa kampasi ya mazimbu sua-morogoro imechukua jina lake.Dr ulimboka ni mmoja wa hao.Tuko wengi sana wa dizaini za ulimboka ni ka upenyo tu tunakosa .ngoja nigombee hata saccos ya mtaa nilizue. heri ufe umesimama kuliko kuishi umepiga magoti
 
Naongeza kwa kusema kwamba fikra pana inaonesha pia kuwa mpaka madaktari wakagoma ulinzi wa vyombo vya dola kwa mtu huyo maana nyingine ni kwamba WANAJUA VITU AMBAVYO VYOMBO VYA DOLA VINAFANYA KWA WATU WAKE WAWAPO HOSPITALINI. HASA WATU AMBAO "WAKUBWA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA DOLA" HAWAWATAKI WAISHI. MADAKTARI WAMEBAINI VYOMBO VYA DOLA NA WAMILIKI WAKE HAWATAKI ULIMBOKA AISHI, WATADHURU ZAIDI YA WALIVYOMDHURU.

Katika hali isiyo ya kawaida, madaktari wameamua wao wenyewe, kuwa walinzi wa kamanda wao dr. uli. Hali hii inamaanisha kuwa madaktari hawa, hawana imani na jeshi la polisi, kwani hawaamini kuwa ulinzi wa polisi, waweza kuwa salama kwa kamanda wao. Kukosekana kwa imani ya madaktari kwa chombo halali cha usalama wa raia, kinazidi kujenga chuki kati ya makundi haya mawili. wakati huo huo, jeshi la polisi, linaendelea kuwa chombo cha dola cha kupiga, kunyanyasa, na kutesa raia.
Hali hii, inaweza kupelekea madaktari kutumia taaluma yao katika vita hii chafu. Hali ikifikia hapo, nchi inakosa uhalali wa kuwa dola.

WAZO LANGU:-
Mheshimiwa mkuu wa kaya, katika hali hii, iko haja ya kuvunja ukimya, utoe sauti angalau ya kupoza machungu ya jamii, la sivyo, magumu yakitokea, mimi na wewe, hatucheka wala kufurahia matokeo yake. Tafadhali mkuu, funguka.
"MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA"
 
Katika hali isiyo ya kawaida, madaktari wameamua wao wenyewe, kuwa walinzi wa kamanda wao dr. uli. Hali hii inamaanisha kuwa madaktari hawa, hawana imani na jeshi la polisi, kwani hawaamini kuwa ulinzi wa polisi, waweza kuwa salama kwa kamanda wao. Kukosekana kwa imani ya madaktari kwa chombo halali cha usalama wa raia, kinazidi kujenga chuki kati ya makundi haya mawili. wakati huo huo, jeshi la polisi, linaendelea kuwa chombo cha dola cha kupiga, kunyanyasa, na kutesa raia.
Hali hii, inaweza kupelekea madaktari kutumia taaluma yao katika vita hii chafu. Hali ikifikia hapo, nchi inakosa uhalali wa kuwa dola.

WAZO LANGU:-
Mheshimiwa mkuu wa kaya, katika hali hii, iko haja ya kuvunja ukimya, utoe sauti angalau ya kupoza machungu ya jamii, la sivyo, magumu yakitokea, mimi na wewe, hatucheka wala kufurahia matokeo yake. Tafadhali mkuu, funguka.
"MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA"

Usiwe na wasi, atafunguka muda mfupi ujao. nadhani atakapoongea na wananchi wake katika utaratibu wake wa kila mwisho wa mwezi utapata majibu ya maswali yako
 
Back
Top Bottom