Mkuu The Bold, tuandalie Makala kuhusu Mhe. Andrew Chenge!

Aleyn

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
20,333
34,899
Habari Wakuu!

Binafsi namuona Mh. Andrew Chenge sio mtu wa kawaida kabisa, kila aina ya kashfa ya Ufisadi ktk nchi hii basi jina lake linahusishwa. Na kwa bahati mbaya au nzuri inaonesha huyu jamaa ana pesa nyingi sana mpaka kufika hatua kusema kuwa Milion 10 ni pesa ya mboga.

Kwa mtu mwenye akili timamu atagundua kuwa ili uweze kupiga pesa kama hizi hata kama sio kihalali lazima uwe na akili nyingi sana, mimi ninaamini Mh. Chenge ni kichwa. Inawezekana ametupiga saana kwa upumbavu wetu watanzania na hususani wale viongozi wakubwa zaidi.

Amefanya kazi na Marais wastaafu wakiwemo Mkapa na Rais Kikwete.

-Chenge ametwajwa sakata la ESCROW

-Chenge amehusishwa na mikata ya Madini, kwa sasa hivi ndio hot topic nchini.

-Chenge anahusika na manunuzi ya Radar nchini uingereza ambayo tumepigwa mabilion ya pesa

-Na mengine mengi.......

Sasa mimi Ombi langu ni kumtaka Mkuu The Bold atuandalie nakala juu ya hiki kiumbe, inawezekana Tanzania tuna watu ambao wamefanya matukio ya ajabu saaaana ila hatuyajui kiundani zaidi.

Ni mara nyingi ktk hili Jukwaa kuna uchambuzi wa watu mbalimbali, magaidi, majambazi, viongozi n.k

Mkuu The Bold, kama ulivyomchambua Plablo Escobar ktk ile Thread ya 'Plata o Plomo, Ulimwengu wa Siri kiganjani mwa binadamu mmoja' naomba utuandalie pia kuhusu huyu bwana Chenge. Na sio lazima awe The Bold tu ila kama unaweza ukaandika nakala nzuri kama ile Pablo Escobar a.k.a The Boss, El Patrin, The Don naomba wakuu wa hili jukwaa mtuandalie nakala.

Binafsi nitapendekeza Thread isomeke hivi

"Lete dili tupige Pesa, Ulimwengu wa Ufisadi Tz kiganjani mwa Binadamu mmoja'

Asanteni!
 
Mkuu unaonekana hata ukiona demu unaweza kumwita mtu mwingine unayemwamini kwa kutongoza aje amtongoze huyo demu, maana hapa umetumia akili za kushikiwa.

Jiamini mkuu, hata wewe unaweza kufanya na ikasomeka vizuri tu.
 
Chenge nmesoma kiukweli yule sio binadamu wa kawaida anaakili kuzidi wasomi wote Tz
 
Hahaha.!! Dah mkuu..

Tatizo la hapa kwetu ni kutafutana... And kumbuka mimi nimejiweka wazi... Sijajificha! Watu wanafahamu "The Bold" ni nani... Ndio maana huwa sipendi kuchangia mijadala ya jukwaa la siasa na mijadala inayo fanana na hiyo...

Huwezi amini nimeandika kijimakala tu kuhusu 'tiss' tayari nimeanza kuulizwa ulizwa kwa text kwenye simu... Kisa nimesema tu siku moja nitaandika kwa undani zaidi... Ati naulizwa "unataka kuandika nini?"

Ila sio mbaya... Siku moja nikiamka na "akili za usiku" naandika tu kuhusu joka la makengeza
 
Mkuu unaonekana hata ukiona demu unaweza kumwita mtu mwingine unayemwamini kwa kutongoza aje amtongoze huyo demu, maana hapa umetumia akili za kushikiwa.

Jiamini mkuu, hata wewe unaweza kufanya na ikasomeka vizuri tu.
Sitaki kuamini kuwa wewe unamjua Aleyn kuliko yeye anavyojijua.
Na sio kila mtu anaweza kuwa muandishi mzuri,ndio maana daktari nguli mwenye PhD hawezi kuijua sheria kama Lissu japo yeye ana elimu kubwa kumzidi.

My point is hakuna anayejua yote na kuweza yote,hata huyo The bold nguli wa makala zenye akili haniwezi linapokuja suala la 'ubuyu' hahahaaaa
Muhimu ni kukubali tu huwezi na kumuachia mjuzi afanye yake,sote hatuwezi kuwa waandishi mahiri.
#VITA YA THE BOLD HAIJAWAHI KUMUACHA MTU SALAMA#
 
Nina sababu bilioni za kukupenda wewe mwanamke..
 
Hahaha.!! Dah mkuu..

Tatizo la hapa kwetu ni kutafutana... And kumbuka mimi nimejiweka wazi... Sijajificha! Watu wanafahamu "The Bold" ni nani... Ndio maana huwa sipendi kuchangia mijadala ya jukwaa la siasa na mijadala inayo fanana na hiyo...

Huwezi amini nimeandika kijimakala tu kuhusu 'tiss' tayari nimeanza kuulizwa ulizwa kwa text kwenye simu... Kisa nimesema tu siku moja nitaandika kwa undani zaidi... Ati naulizwa "unataka kuandika nini?"

Ila sio mbaya... Siku moja nikiamka na "akili za usiku" naandika tu kuhusu joka la makengeza
Mkuu ilikuaje ukafahamika wakati wewe sio "Verified User"?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom