Mkuu mpya shule ya sekondari Kahororo anashusha taaluma

Feb 8, 2012
92
8
Huyu mkuu mpya aliyehamishwa Kahororo kutoka shule ya sekondari Bukoba ni kikwazo cha maendeleo ya taaluma.Ameondolewa Bukoba sec baada ya matokeo mabovu ya form iv kwani mwaka 2010 kulikuwa na ziro 95.Vilevile akiwa Kahororo sekondari ameishusha shule kutoka ya 2 mpaka ya 14 kati ya shule 18 matokeo ya form vi mwaka 2012.Amekuwa akiungana na wanafunzi kudharirisha walimu.
 
hovyo kabisa..mnaleta uvivu kusoma mnasingizia mkuu wa shule?kutwa mko kwenye fb halafu mnalalamika...chezeni na shule tu kama hamjawa wauza maji barabarani
 
Huyu mkuu mpya
aliyehamishwa Kahororo kutoka shule ya sekondari Bukoba ni kikwazo cha
maendeleo ya taaluma.Ameondolewa Bukoba sec baada ya matokeo mabovu ya
form iv kwani mwaka 2010 kulikuwa na ziro 95.Vilevile akiwa Kahororo
sekondari ameishusha shule kutoka ya 2 mpaka ya 14 kati ya shule 18
matokeo ya form vi mwaka 2012.Amekuwa akiungana na wanafunzi
kudharirisha walimu.
Acha majungu wewe,mbona huelezi anashusha vipi taaluma kazi kulialia tu.Uvivu wa kujisomea mnasingizia Mkuu wa shule.Shule ina walimu wangapi ? Kila somo lina mwalimu ? Kuna maabara na vifaa vya kutosha ? Kuna library na vitabu vya kutosha ? Acha kulialia.
 
Ina maana huyo jamaa ndiye anasoma au wanafunzi wenyewe!Hizo div 4 na 0 siyo kigezo cha kusema anashusha taaluma kama kuna wanafunzi wanaofaulu katika shule hiyo!
 
Uongozi wake mbovu ndo unapelekea taaluma kushuka.Amekuwa anawavunja moyo walimu wetu kufundisha.Hana mahusiano mazuri na walimu kwan amekuwa anawagawa walimu kwa misingi ya dini,kabila na maeneo.Huyu mkuu anapendelea uislam hata alipokuwa Bukoba sec aliwajaza wanafunzi wa kiislam na kuacha kuwachagua wakristo.Isitoshe anashirikiana na afisa elimu kunyanyasa walimu wasio wazawa.
 
nahh wakuu kijana ana hoja,uongozi wa shule unaweza shusha taaluma ya shule nzima,i،ve experienced t in my past studies. Hata ukiangalia zile special xuls(baada ya f6 mwaka huu cjui zinaitwaje tena) kunakua na ushirikiano mzuri baina ya wanafunzi ,waalim,makam msaidiz na mkuu. Hakika kukiwa na hitlaf popote baina ya hao wa2,matokeo ya m2,kwa m2 kwa wachache yanaweza yasiathirike vikubwa but shule nzima kiujumla lazima ishuke.
 
Dah! hii shule ilikuwa inatoa vichwa c mchezo! enzi za 70s ilikuwa sawa na mzumbe, tabora boys, iliboru au kibaha, maprof na madoct wa bk wengi wamesoma shule hii kwa kidato cha kwanza mpaka cha nne, amin usiamin hii shule imeanza kuzidiwa na za kata! kwanza ina mazingira ya kishule, na ipo sehem iliyotulia. na jamaa kama ameamua kuleta uisilam ndo kaimaliza hii shule. kweli hata mm inanisikitisha, ndo shule iliyokuwa inabeba mkoa wa kagera ukiondoa zile za seminari kama vile katoke na lubya seminari. sasa wahaya twafa kama hao jajawidi wamepewa shule yetu.
 
Miaka ya nyuma kabla ya yeye kuwepo pale shule ya sekondari Kahororo, shule ilikuwa ya pili matokeo ya kidato cha nne na kulikuwa zero 2...baada ya kuja yeye shule imeshika nafasi ya 14 kati ya 18 kimkoa matokeo ya kidato cha 6 mwaka 2012.Kuna zero 17.Anaipeleka wapi elimu? Hata ukuu wa shule alipata kwa misingi ya RUSHWA na kujuana kwani hakuwa na sifa ya kuwa mkuu wa shule.Alipewa ukuu wa shule akiwa na uzoefu wa miaka 2 tu na kuachwa walimu wenye uzoefu wa muda mrefu.
 
Nani tena huyo anayetualibia shule???
Kahororo tunaihistoria nayo bwana! Enzi za Mr.Ishengoma na timu yake(Agricola, Mkoba, Rweyemamu a.k.a Enkura, Mrs Buberwa, Kamugisha na Karuka....) ilikuwa inatisha. au ile Jangili Road imeimalishwa vijana wanakimbilia Nyaishenye Beach, Mafumbo na Kashai kula bata wanasahau prepooo???
 
Mwaka jana tarehe 01 Dec wanafunzi wa shule ya sekondari Kahororo waliwashambulia walimu na kuharibu mali zao.Walifanya jaribio la kumbaka mwalimu wa kike kwa kumvamia nyumbani kwake wakiwa na kondomu.Vilevile walipanga kumuua mwalimu huyo.Fujo hizi ziliibuka baada ya kuja mkuu huyo mpya.Kwani amekuwa anakaa na wanafunzi na kuwachochea wawe na mtizamo hasi kwa walimu.
 
hivi siku hizi huko bukoba mna matatizo gani? kwani mkuu wa shule anaingia darasani?
Nyie someni bana..kwani lini bukoba sec walishawahi kuwa na matokeo mazuri?.
Nyie mlitaka mletewe wa Ihungo au Nyakato. basi watawaleteeni wa rugambwa kwa mademu zenu. kahororo bana..mpira zero, kusoma zero, mnakaa mnakunywa maziwa ya ng'ombe wa shule tu. Piga buku bana.
 
..Huyu mkuu anapendelea uislam hata alipokuwa Bukoba sec aliwajaza wanafunzi wa kiislam na kuacha kuwachagua wakristo.Isitoshe anashirikiana na afisa elimu kunyanyasa walimu wasio wazawa.
Lini sekondari zimeacha utaratibu wa kuchagua wanafunzi kwa kigezo cha Cuf-Off-Point na kuanza kutumia dini? Kwenye kuchagua wanafunzi unajua ni nani wanashiriki na mchakato ukoje?
.....Isitoshe anashirikiana na afisa elimu kunyanyasa walimu wasio wazawa....
Una kila kimelea cha ubaguzi....chukua kauli mbiu ya Invisible "Ficha Upumbafu, Usifiche Hekima" kwa maana nyingine kutumia jina bandia haipaswi kuwa sababu ya kuandika upuuzi
 
Back
Top Bottom