Mkuu Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Afungwa Mwaka Mmoja kwa Kuajiri Watumishi Darasa la 7

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
1.JPG

MKUU wa Chuo cha Uhasibu (IAA) Njiro mkoani Arusha, Profesa Johannes Monyo amehukumiwa kifungo cha nje kwa sharti la kutofanya kosa lolote ndani ya mwaka mmoja.

Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa iliyopita na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Devotha Msofe baada ya kujiridhisha kuwa Profesa Monyo alifanya makosa ya kuajiri watumishi wanane wenye elimu ya darasa la saba bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma.

Hakimu Msofe alisema Profesa Monyo akiwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro, aliwaingiza watumishi wanane kwenye ajira ya kudumu bila ya kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu Mkuu Utumishi.

Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani kwa mashahidi 10 pamoja na vielelezo vinane vilivyotolewa mahakamani hapo na upande wa mshtakiwa kuwa na mashahidi wawili, mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka kuwa Profesa Monyo alifanya kosa hilo la kuajiri wafanyakazi hao wanane bila kufuata taratibu za kisheria.

“Mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa ulifanya kosa hili la kuajiri wafanyakazi wanane bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma hivyo mahakama hii inakutia hatiani kwa kukupa kifungo cha nje kwa sharti la kuutofanya kosa lolote katika kipindi cha mwaka mmoja,” alisema Hakimu Msofe.

Awali, Mwanasheria kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Adam Kilongozi alidai kuwa Juni, 2010 Profesa Monyo anatuhumiwa kuwapa ajira watumishi wanane ambao ni Pamela Maboko, Samson Mbarya, Mawazo Ndaro, Juma Nyarutu, Lilian Ngowi, Godfrey Mollel, Musa Maiki na Salim Shabani.

Kosa jingine ni Profesa Monyo kwa kutumia mamlaka yake vibaya,kuwaingiza watumishi hao wanane katika ajira, ilhali akijua elimu zao ni darasa la saba. Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo kutolewa, Profesa Monyo ameonesha kusudio la kukata rufaa kupitia kwa wakili wake, Severine Lawena.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa, mwandishi alimhoji Mwanasheria wa TAKUKURU, Kilongozi, kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma au Kanuni zake inasemaje juu ya mtumishi anapohukumiwa akiwa bado yupo kazini, ambapo alisema kama mtuhumiwa amehukumiwa na akaonesha nia ya kukata rufaa, basi hukumu hiyo inaweza kufanya kazi au kutofanya kazi hadi hapo rufaa itakaposikilizwa.

Alisisitiza kuwa Takukuru wameshatuma nakala hiyo ya hukumu Tume ya Utumishi wa Umma, mwajiri wa Profesa Monyo, ili mamlaka husika zilifanyie kazi suala hilo lakini pia ni lazima mwajiri wake naye ajiridhishe na hukumu hiyo.
 
Nimeshuhudia mara kibao...watu wenye elimu kubwa wanashindwa na,wenye elimu ndogo kwenye utendaji wa kazi.
Nampongeza the prof......kwa kufikiria nje yabox.
 
1.JPG

MKUU wa Chuo cha Uhasibu (IAA) Njiro mkoani Arusha, Profesa Johannes Monyo amehukumiwa kifungo cha nje kwa sharti la kutofanya kosa lolote ndani ya mwaka mmoja.

Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa iliyopita na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Devotha Msofe baada ya kujiridhisha kuwa Profesa Monyo alifanya makosa ya kuajiri watumishi wanane wenye elimu ya darasa la saba bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma.

Hakimu Msofe alisema Profesa Monyo akiwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro, aliwaingiza watumishi wanane kwenye ajira ya kudumu bila ya kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu Mkuu Utumishi.

Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani kwa mashahidi 10 pamoja na vielelezo vinane vilivyotolewa mahakamani hapo na upande wa mshtakiwa kuwa na mashahidi wawili, mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka kuwa Profesa Monyo alifanya kosa hilo la kuajiri wafanyakazi hao wanane bila kufuata taratibu za kisheria.

“Mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa ulifanya kosa hili la kuajiri wafanyakazi wanane bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma hivyo mahakama hii inakutia hatiani kwa kukupa kifungo cha nje kwa sharti la kuutofanya kosa lolote katika kipindi cha mwaka mmoja,” alisema Hakimu Msofe.

Awali, Mwanasheria kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Adam Kilongozi alidai kuwa Juni, 2010 Profesa Monyo anatuhumiwa kuwapa ajira watumishi wanane ambao ni Pamela Maboko, Samson Mbarya, Mawazo Ndaro, Juma Nyarutu, Lilian Ngowi, Godfrey Mollel, Musa Maiki na Salim Shabani.

Kosa jingine ni Profesa Monyo kwa kutumia mamlaka yake vibaya,kuwaingiza watumishi hao wanane katika ajira, ilhali akijua elimu zao ni darasa la saba. Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo kutolewa, Profesa Monyo ameonesha kusudio la kukata rufaa kupitia kwa wakili wake, Severine Lawena.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa, mwandishi alimhoji Mwanasheria wa Takukuru, Kilongozi, kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma au Kanuni zake inasemaje juu ya mtumishi anapohukumiwa akiwa bado yupo kazini, ambapo alisema kama mtuhumiwa amehukumiwa na akaonesha nia ya kukata rufaa, basi hukumu hiyo inaweza kufanya kazi au kutofanya kazi hadi hapo rufaa itakaposikilizwa.

Alisisitiza kuwa Takukuru wameshatuma nakala hiyo ya hukumu Tume ya Utumishi wa Umma, mwajiri wa Profesa Monyo, ili mamlaka husika zilifanyie kazi suala hilo lakini pia ni lazima mwajiri wake naye ajiridhishe na hukumu hiyo.
Darasa la saba hawana haki ya kuajiriwa? hata kufunga na kufungua geti hawawezi?
 
Darasa la saba hawana haki ya kuajiriwa? hata kufunga na kufungua geti hawawezi?

Swali zuri...la msingi taarifa inayotolewa si kamilifu. Haisemi watu hao waliajiririwa katika nafasi zipi, na pili kama kweli walipewa kazi katika nafasi wasizostahili, Chuo ama serikali imeathirika kwa namna gani, ...wizi wa mali ya umma? Au kushukka kwa heshima ya utumishi wa chuo?
 
kwani darasa la 7 sio watanzania??? mbona kwenye majeshi wanaajiriwa????
 
kwani darasa la 7 sio watanzania??? mbona kwenye majeshi wanaajiriwa????
Wanaajiriwa kuenda kufanya kazi gani, kuna nafasi zinakua ni rahisi hata mtoto wa darasa la saba anaiweza, iyo ni kweli lakini kwa pengine sheria inasema muajiriwa wa nafasi hiyo lazima afike form 4, inawezekana huyu prof alifanya kosa kama hili, aliangalia zaidi cheap labor kuliko hata sheria inavostahiki
 
Huu upuuzi, sasa sioni mantiki, msomi anashindwa kufanya kazi ila wa darasa la saba akiifanya hiyo kazi aliyemuajiri anafungwa, hovyo kabisa!Prof, safi sana kwa kufikiria nje ya box, kweli wewe ni Prof wa ukweli, ni quality kichwani ndo yatakiwa sio quantity ya elimu, go prof!
 
Inavyoonekana suala hapa ni mkuu wa chuo kuajiri bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma kwa maana ya kupata kibali utumishi. Hili la kuajiri darasa la saba huenda limetumika kwa lengo la kuwanyanyapaa walioajiriwa, vinginevyo tungeambiwa waliajiriwa katika posts zipi jambo ambalo lilipaswa lifanywe na mwandishi aliyeandika habari hiyo.
 
Nadhani issue kubwa hapa ni mbili. Kwamba mkuu wa chuo kaajiri watu bila kupata kibali kutoka Utumishi kinachoridhia ajira ya watu hao na cha pili ni kuajiri watumishi hao wenye elimu ya darasa la saba wakati nafasi zenyewe zilihitaji watu wenye elimu ya juu zaidi ya hiyo ya darasa la saba m.f. elimu ya kidato cha nne, sita n.k.
 
Arusha ipo chini ya chadema lkn yote haya yanatokea.

Inasikitisha sana chadema hawasimamii vizuri .
Embu punguzeni mihemuko ya kivyama kidogo, ndo maana hata nchi yetu kwenda mbele itakua shida sana, watu wanafikiri vyama zaidi kuliko umoja wetu kama Taifa, kila linapotokea jambo tunajaribu kucheki namna gani tutalitumia kumponda mpinzani wetu kisiasa, hii hali imepoteza kabisa maana ya siasa hapa bongo, siasa imekua ka ushabiki wa mpira , watu hawatafakari tena bali wanashabikia tu kile kilicho na masilahi na chama chao bila kujali kina manufaa au hakina manufaa kwa taifa, yatupasa tubadilike
 
Back
Top Bottom