E. J. Magarinza
Member
- Jan 13, 2011
- 37
- 10
Picha zote ni baada ya mkutano. Hawa ni wananchi wa jiji la Mwanza wakimsindikiza mbunge wao Wenje kwa maandamano makubwa katikati ya jiji baada ya mkutano.
Mheshimiwa Wenje kaongea mambo mengi ya msingi ila nililolipenda mimi kama mkazi wa Nyamagana jijini Mwanza ni hii kauli ya Wenje, nanukuu "mimi sataki kuwa mbunge wa wananchi waoga". Hii kauli kaitoa akiwahamasisha wananchi wa jiji la Mwanza kutokubali kunyanyaswa na vyombo vya serikali pale vinapoonea wananchi na kuhimiza kudai maisha bora kwa ujumla na yeye kuwa kiongozi katika harakati hizi.
Kwa ufupi nimejionea kwa macho yangu Wenje ni nani Mwanza. Anapendwa kupita kawaida, hivyo kuanzia leo nawahakikishia wanajamvi wenzangu tuwapuuze wote wanaokuja hapa wakimponda kamanda Wenje kwa kauli za uwongo.
Nawasilisha....