Ezekia Wenje adai Serikali imeshindwa kudhibiti mfumuko wa bei

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,340
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa Victoria , Ezekia Wenje , mmoja wa Wahanga wa Uchaguzi wa 2020 , ambaye Mkutano wake wa mwisho wa Kampeni Ulimiminiwa risasi utadhani Ukraine , na kumuua Kaka yake , sasa amejitokeza nchini ili kuimarisha chama chake .

FB_IMG_1666280123805.jpg

Wenje baada ya tukio lile alilazimika kukimbia na kujificha kusikojulikana ili kuokoa uhai wake , na wala hakushiriki mazishi ya kaka yake , maana yeye ndiye alikuwa Target ya waliotumwa kummaliza.

Utukufu wa Mungu ni wa Ajabu sana , leo wenye amerudi na kushiriki Chadema Digital kwenye kanda yake , HATIMAYE SHETANI AMESHINDWA .

FB_IMG_1666088004685.jpg

Mytake : Kuwasamehe walioshiriki unyama wa uchaguzi wa 2020 ni Sawa ngamia kupita kwenye Tundu la Sindano , Sidhani kama inawezekana .

TUOMBE SANA MUNGU .

=====

Wenje aunguruma Sengerema​

wenje-pic.jpg

Muktasari:​

  • Mbunge wa zamani wa Nyamagana (Chadema), Ezekiel Wenje amesema Serikali imewatekeleza wananchi katika jambo la mfumo wa bei hasa upande wa mahitaji muhimu ya wananchi hususani chakula na kuwaweke wananchi njia panda.
Sengerema. Mbunge wa zamani wa Nyamagana (Chadema), Ezekiel Wenje amesema Serikali imeshindwa kudhibiti mfumuko wa bei na kuwaacha wananchi wa Tanzania walikia na kutaabika.

Wenje ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria, ametoa kauli hiyo leo Oktoba 20, 2022 kwenye mkutano maalumu wa chama hicho wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

Amesema Serikali imewatekeleza wananchi katika jambo la mfumo wa bei hasa upande wa mahitaji muhimu ya wananchi hususani chakula na kuwaweke wananchi njia panda.
“Wanakalia kuumiza wananchi kwa tozo zisizo na ulazima wanashindwa kuangalia jambo linalogusa maisha ya watanzania,” amesema Wenje.
Amesema wananchi sasa wanatakiwa kusimama na kuamua kufanya mabadiliko ya kweli ndani ya nchi ili wapate unafuu wa maisha na jambo hilo litaletwa na Katiba ambayo ni chaguo la wananchi.

Hivi sasa hapa nchini, wananchi wanalia kutokana na mfumuko wa bei, hii imesabibishwa na wafanyabiashara kupandisha bei ya vyakula, hali inayowafanya wananchi kulia na hali hiyo.

Sambamba na hilo, Wenje amesema zama zimebadilika, walikimbia nchi sasa wamerudi kuisuka Chadema, hivyo wanachadema wanapaswa kuungana kwa pamoja ili kuwasaidia wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Pambalu amesema nchi hii wananchi wanatakiwa kufanya mabadiliko ili kuwaondolea msongo wa mawazo waliyonayo kutokana na mfuko wa bei.

Mabaliko haya nikudai katiba mpya ambayo nimkombozi wa Watanzania wote, hivyo wanatakiwa kuwa wamoja ili wasonge mbele.

Paul Lufungulu ni mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Sengerema, amesema wako tayari na wamejiandaa kutembea kwa kila kijiji kutoa hamasa kwa wananchi juu kilio cha katiba mpya.

Maye katibu mwenezi wa Chadema Jimbo la Sengerema, Stanley Kakele amesema wamejipanga kuhakikisha jamii inapata elimu juu uwepo na wakatiba mpya.

Chanzo: Mwananchi
 
Ukisikia unafiki ndio huu, na huenda kwenye hili bandiko lako Kuna chumvi nyingi sana, unasema.

"TUMUOMBE SANA MUNGU", Ili afanyaje?

Yani huku unatangaza visasi vya kuto samehe alafu hapohapo unamuomba Mungu ambae wakati wote Mungu anataka binadami wote kusameheana

Labda kama wewe mungu wako ni shetani hapo sawa sababu shetani ndio hanaga msamaha.
 
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa Victoria , Ezekia Wenje , mmoja wa Wahanga wa Uchaguzi wa 2020 , ambaye Mkutano wake wa mwisho wa Kampeni Ulimiminiwa risasi utadhani Ukraine , na kumuua Kaka yake , sasa amejitokeza nchini ili kuimarisha chama chake .

View attachment 2393010

Wenje baada ya tukio lile alilazimika kukimbia na kujificha kusikojulikana ili kuokoa uhai wake , na wala hakushiriki mazishi ya kaka yake , maana yeye ndiye alikuwa Target ya waliotumwa kummaliza.

Utukufu wa Mungu ni wa Ajabu sana , leo wenye amerudi na kushiriki Chadema Digital kwenye kanda yake , HATIMAYE SHETANI AMESHINDWA .

View attachment 2393041

Mytake : Kuwasamehe walioshiriki unyama wa uchaguzi wa 2020 ni Sawa ngamia kupita kwenye Tundu la Sindano , Sidhani kama inawezekana .

TUOMBE SANA MUNGU .
Aliyetaka auawe yuko wapi?
 
Ukisikia unafiki ndio huu, na huenda kwenye hili bandiko lako Kuna chumvi nyingi sana, unasema.

"TUMUOMBE SANA MUNGU", Ili afanyaje??.

Yani huku unatangaza visasi vya kuto samehe alafu hapohapo unamuomba Mungu ambae wakati wote Mungu anataka binadami wote kusameheana.

Labda kama wewe mungu wako ni shetani hapo sawa sababu shetani ndio hanaga msamaha.
Kuna makosa kumuomba Mungu ?
 
Herode aliyetafuta uhai wake ameishakufa na kutangulia motoni
 
Ukisikia unafiki ndio huu, na huenda kwenye hili bandiko lako Kuna chumvi nyingi sana, unasema.

"TUMUOMBE SANA MUNGU", Ili afanyaje??.

Yani huku unatangaza visasi vya kuto samehe alafu hapohapo unamuomba Mungu ambae wakati wote Mungu anataka binadami wote kusameheana.

Labda kama wewe mungu wako ni shetani hapo sawa sababu shetani ndio hanaga msamaha.
Upumbavu huu, Mungu hasamehi mashetani, yasiyojali utu wa kibinadamu, elewa family nyingi hadi leo hazina closure na wapendwa wao, jitu katili halifikiri jirani yake na familia yake, kila damu iliyomwagika itakuwa accounted no matter what,huwezi ukawa trigger happy halafu Mungu atasamehe...msamaha on my foot
 
Back
Top Bottom