Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi wafutwa

Tajiel Urioh

Member
Oct 1, 2011
44
9
Rais wa Chile ametangaza muda mfupi uliopita kuwa nchi yake haitaweza kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.

images (14).jpeg


Hili limetokea baada ya maandamano makubwa ya raia kuendelea nchini humo na hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa washiriki wa mkutano huu wa ngazi ya juu kabisa kwenye suala zima la mabadiliko ya tabianchi duniani.

Kabla ya hapo mkutano huu ulipangwa kufanyika nchini Brazil ila baada ya Serikali mpya "ambayo haiungi mkono ipasavyo" juhudi za kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ikasema haitaweza kuwa mwenyeji tena kama ilivyokuwa imekubaliwa na uongozi uliopita.

Sasa kuna uwezekano wa mkutano huu kutafanyika January 2020 mjini Bonn Germany ilipo Secretariat ya UNFCCC.

Fuatilia kwa Kihispania zaidi hapa | Taarifa ya UNFCCC - English
 
Back
Top Bottom