Mkutano wa Pongezi kwa CHADEMA

Kuanzia leo nakiri na kuamini kuwa vyama vya siasa Tanzania vimebakia viwili tu;

  1. CCM - zee lililochoka linalojikongoja kwa fimbo kuelekea kaburini.
  2. Chadema - kijana mwenye afya huku damu yake ikizidi kuchemka.
Huu tena si muda wa kukaa pembeni, huu ni muda wa kujitambulisha rasmi uko upande gani kwenye mapambano, asante Chadema.
  • Huu si muda wa kulegeza mabano, huu ni muda wa kuzidi kuchochea moto wa mabadiliko kila moja kadri ya uwezo wake, asante Chadema.
  • Huu si muda wa kuendelea kukaa gizani, huu ni muda wa kuangaza macho na kuyaona maovu ya CCM, asante Chadema kwa kutuwashia taa.
  • Huu si muda wa kukubali kuendelea kuzugwa na laghai za CCM, huu ni muda wa kukataa dhuluma, asante Chadema kwa kutupatia elimu.
  • Huu si muda wa kuendelea kuwavumilia mafisadi, huu ni muda wa kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria, asante Chadema kwa kutuondoa woga.
  • Huu si muda wa kuwachekea viongozi wabovu, wezi na wauaji, huu ni muda wa nguvu ya Umma kufanya kazi yake, asante Chadema kwa kutupa ujasiri.
  • Huu si muda wa kuendelea na maisha duni, huu ni muda wa kudai na kupigania maisha bora, asante Chadema kwa kuonesha uthubutu.
Chadema mmewasha indiketa Arumeru, ambaye hatawapisha asilalame kwani kujaribu kuizuia tsunami mwisho wake ni maafa tu ya kusombwa na maji, heko Chadema. A luta continua...!
 
Mimi hii style ya kulinda kura waliyonayo chadema ndio ninaihusudu kwani ni mwiba mchungu kwa magamba.....
 
Pipooooooooooooooooooooooz powerrrrrrrrrrrrrrrrr..............................

Hakika Mungu amesikia kilio cha wana arumeru kwani hata mvua imenyesha katika tukio hilo baada ya kupita muda mrefu bila mvua kunyesha.
 
Peoplessssssssssssssssssssssssssssssssssssss powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Mkuu huwa sipendi mzaha kwenye masuala ya msingi......nakushauri futa hii post yako au ID hii iwe merged kwenye ban.

then who are you to ask my ID name??how sure are you am just a new member in JF??haya kanisemehe kwa Mods wanipige ban ufurahi...tusherehekee cdm imeshinda tuache haya
 
Hongera CDM. Hata hv namuonea nyundo fupi ya magamba na mzee mamvi. Moto ule ule hakuna kulala nchi nzima
 
Mh Halima Mdee naona pimples hakuna tena!Mambo ya proactiv ama?Karibu JF bidada, tulisikia unakuja, ikawaje tena?

Hongereni cdm.
Kuna siku nilimuuliza kuhusiana na swali hili akasema tayari yee ni member wa JF ila ni kazi tu ndizo zimemtinga...
 
Jihadharini na uwezekano wa kujikuta katika 'fungate ya ushindi' kisha muda ukayoyoma mkiwa mnakula na kunywa. kutakavyokucha Chama Cha Magamba watawasema hao!!!! Shangilieni aste then twende kazi; au vipi macomrade?!!
 
[h=1]Taswira Za Hali Halisi Iliyokua Arumeru Mashariki Leo Asubuhi baada Ya MgombeaUbunge Kiti Cha Arumeru Mashariki Joshua Nassari(CHADEMA)Kutangazwa Mshindi[/h]

Written by haki | // 0 comments

arumeru.jpg

arumeru1.jpg

arumeru3.jpg

arumeru2.jpg

arumeru4.jpg

Mitaa mbalimbali Arumeru ilifurika leo asubuhi kama muonavyo pichani muda mfupi baada ya mgombea wa Ubunge kiti cha Arumeru Mashariki Joshua Nassari Kutangazwa Mshindi.Picha na Habari na Mjumbe Maalum -Arumeru
 
Apr 2

[h=1]Live Kutoka Arumeru Hivi Sasa: Umati wa maelfu ya watu wakusanyika sasa katika viwanja vya Shule ya msingi ya Leganga ambapo mkutano mkubwa wa kuwashukuru wana Arumeru Mashariki Kwa Kuichagua kuchagua CHADEMA[/h]

Written by haki | // 0 comments

chad+s3.jpg

chad+s5.jpg

chad+s4.jpg

chad1.jpg

Taswira mbalimbali za Umati Mkubwa na Wafuasi wa CHADEMA ukiwa umekusanyiaka shule ya msingi leganga hivi sasa tayari kabisa kwa mkutano mkubwa wa kuwashukuru Wanaarumeru Kwa Kuichagua Chadema na kumpa ushindi Mgombea wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki(CHADEMA)Joshua Nassari aliyekua anachuana Vikali na Mgombea wa CCM Sioi Sumari Kwenye Uchaguzi uliofanyika Jana
 
[h=1]Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC -CCM Nape Nnauye Akutana na Waandishi Wa Habari Nakusema "Tunampongeza Joshua Nasari(CHADEMA)na Hakuna Hujuma Yoyote Uchaguzi Ulikuwa Huru na Haki",Lakini Pia Akawapongeza Wananchi wa Jimbo la Arumeru Kwani hiyo Ndiyo Demokrasia Yao.''[/h]

Written by haki | // 0 comments

1.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw.Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi ndogo ya chama hicho zilizopo mtaa wa lumumba jijini Dar es salaam, juu ya uchaguzi mdogo wa ubunge ulifanyika jana katika jimbo la Arumeru mashariki, ambapo mgombea wa CHADEMA Joshua Nasari ameibuka mshindi kwa kura 32.972, chama cha mapinduzi kimekubali matokeo hayo yaliotangawa na Tume ya uchaguzi leo asubuhi




Nape kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi amempongeza kijana Nasari na kusema "Tunampongeza Joshua Nasari na hakuna hujuma yoyote uchaguzi ulikuwa huru na haki", lakini pia akawapongeza wananchi wa jimbo la Arumeru kwani hiyo ndiyo Demokrasia yao.
 
Back
Top Bottom