Mkutano wa Masaburi leo Kimara mwisho stendi

Mkutano wa Masaburi leo Kimara mwisho stendi

manSniper

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2015
Posts
814
Reaction score
683
Asubuhi hii napita hapa kwenye daraja la juu Kimara mwisho pale kuna barabara imefungwa wanaweka mahema na maandalizi ya jukwaa na muziki yaani daraja limetapakaa bendera na picha tuu isitoshe imeanza foleni sasa hivi, Je jioni itakuaje? Kwa nini mikutano ya kampeni isifanyikie viwanjani na siyo stendi?
 
Anajisumbua huyo masaburi hata kura elfu 1 hapati
 
CCM wakiandaa Mikutano Ndani au Mbali Na Barbara Watapata Aibuu ya Mwaka Hawana Mvuto Kabissa.
 
Asubuhi hii napita apa kwenye daraja la juu kimara mwisho pale kuna barabara imefungwa wanaweka mahema na maandaliz ya jukwaa na mziki yaani daraja limetapakaa bendera na picha tuu isitoshe imeanza folen sasa hivi je jioni itakuaje? Kwa nn mikutano ya kampen isifanyikie viwanjan na siyo stendi?
Akifanyia viwanjani nani ataenda? Lazima afanyie masokoni na vituo ambako tayari kuna watu ili ionekane amejaza nyomi
 
imenisikitisha taarifa za UDP mwanza kuvamiwa na ccm hadi wakashindwa kufanya mkutano
 
Amefuata watu walipo. Akienda uwanjani hana uhakika kama watamfuata.
 
Walikataa picha/mabango za Lowassa pale Kariakoo wakidai mamlaka za soko hazihusiki na Siasa!! Leo wanafanyia mikutano stand na kusababisha usumbufu usio na sababu za msingi. Na tuambiwe leo kama Mamlaka za barabara Inajihusisha na Siasa ili wengine wakapige mkutano Manzese darajani.

Lowassa alikuwa akipita Gongo la Mboto na kwingineko wakasema anasababisha usumbufu kwa wakaazi wa maeneo husika!! Wacheni uonevu nchi hii yetu sote. Na mwaka huu imekula kwenu ni mwendo wa Lowassa to Ikulu.
 
Sio masaburi ni fenera Mukangara

Hahahhhaa ndo anashindana na Mnyika hahahhha very interesting akamuulize hawa ngumbi

Maana hawa ngumbi yuko miguu juu kaingia kwenye siasa kichwa kichwa yuko teee anajuta
 
Nadhani kama angekuwa na mshauri mzuri wala asingehangaika hivyo maana,mbunge wa ubungo imebaki kutangazwa tu,SAID KUBENEA
 
Walikataa picha/mabango za Lowassa pale Kariakoo wakidai mamlaka za soko hazihusiki na Siasa!! Leo wanafanyia mikutano stand na kusababisha usumbufu usio na sababu za msingi. Na tuambiwe leo kama Mamlaka za barabara Inajihusisha na Siasa ili wengine wakapige mkutano Manzese darajani.

Lowassa alikuwa akipita Gongo la Mboto na kwingineko wakasema anasababisha usumbufu kwa wakaazi wa maeneo husika!! Wacheni uonevu nchi hii yetu sote. Na mwaka huu imekula kwenu ni mwendo wa Lowassa to Ikulu.

Ccm wamefanya hii nchi kama yao yaani kufanyia mkutano stend ni karaha sana kwa ss watumiaji wa Barbara folen asubuhi hii imeanzia pale stop over je kuanzia mchana itakuje je ingekua ni ukawa ndiyo wanafanyia mkutano hapo ingekubalika?
 
Viwanja wameuziana yeye mwenyewe alikua Meya hajafanya lolote anataka ubunge
 
Back
Top Bottom