Okol36
JF-Expert Member
- Jan 10, 2015
- 1,524
- 716
Nyerere: Kama vile nakufananisha?
Mandela: Hata mimi naona sio sura ngeni?
Nyerere: We ndie Mandela eee?!
Mandela: Ndiyo mimi haswa miaka 14 ni mingi.
Nyerere: Sana!!.
Mandela: Sasa nitakaa wapi mbona hakueleweki huku?
Nyerere: We ngoja utapaelewa tu.
Nyerere: Eeh!! vipi huko Tanzania? ulitembelea hata hivi karibuni?
Mandela:
Eeeh! we acha tu, huko mara Zitto msaliti, mara Umeme mgawo miezi sita, mara mgomo wa Gesi haitoki Mtwara, mara kifo cha Mwangosi, mara Dawa za Kulevya, mara Meno ya Tembo, mara kuchoma Makanisa, mara mabomu kwenye mikutano ya hadhara na makanisani, mara Ufisadi, mara Dr. Ulimboka na Kibanda kung’olewa kucha na meno kwa plauzi, mara Division 5, mara Udini, mara ngumi Bungeni, mara kifo cha Dr Mvungi, mara tindikali kwa mapadri, mashehe na wageni, mara Kagame kuishambulia Tanznia, Petroli kuchakachuliwa, mara wengine wanasema eti Muungano ulioasisi unatokana na Visiwa vya Zimbabwe na Zanzibar na sio Tanganyika tena, mara muungano wa serikali tatu ndio unaotakiwa, mara Kigamboni kapewa Obama, mara Bushi na mke wake kaja Tanzania, Clinton na mke wake kaja Tanzania, Kamerun na mke wake kaja Tanzania, Xiing wa uchina kaja Tanzania, mara puttin wa Urusi kaja Tanzania. Yaani hekaya ni ndefu bora urudi ukayashuhudie mwenyewe.
Mara Mandela alipomrushia macho swahiba wake kumbe kashazimia saa nyingi