Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa Kikatiba tu ndiyo utaandika Katiba Mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Dec 30, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Wengi hawaelewi ni kwa nini tunataka katiba mpya................ni kwa sababu tunataka raia wote tushiriki kuitunga katiba hiyo kupitia wawakilishi ambao tutawachagua sisi wenyewe kwa kazi hiyo tu...........hatutaki wabunge waturekebishie katiba iliyopo kwa sababu wataongozwa na masilahi yao binafsi.......na hivyo kutelekeza masilahi ya raia wengi wanyonge.................


  Huko nyuma CCM walipokuwa wanafanya marekebisho ya katiba ya 13 walijaribu kuwatumia mawaziri katika kuinadi kile walichokiita ni "WHITE PAPER" ambayo ilizingatia masilahi ya viongozi tu..............................kwa kujineemesha wenyewe..........na walipoipitisha walijisifu sana kuwa ilikuwa imeandaliwa na wananchi jambo ambalo halikuwa la kweli hata kidogo........................................


  Hili sasa limekuja kugundulika kuwa siyo la kweli hata chembe kwa sababu kiu ya watanzania kujipatia katiba yetu wenyewe badala ya hii iliyopo ya kuwalinda viongozi ipo pale pale...............................................


  Sasa katiba mpya tutaipima kuwa hii ni mpya kama itazingatia vigezo vifuatavyo katika kuiandika:-

  a) Bunge litapitisha sheria ya kuanzishwa mchakato wa wapigakura kuchagua wawakilishi wao wenyewe kupitia majimbo yao ya uchaguzi na wilaya zao kupata watakaoiandika katiba mpya...........................


  b) Katika uwakilishi huo watumishi serikalini wakiwemo wanasiasa watazuiwa kuwemo kama wajumbe wa MKUTANO huo wa KIKATIBA...............................wanasiasa hao ni wale ambao wanashikilia nyadhifa za aina yoyote ndani ya vyama vyao vya siasa au wanashikilia nyadhifa zozote serikalini ikiwemo Bungeni......................


  c) MKUTANO huo wa KIKATIBA utaratibiwa shughuli zake na kamati ya wataalamu ambao usaili wake utafanywa na Kamati ya Bunge inayoshughulikia masuala ya sheria na katiba.....na wajumbe hao wateule wa MKUTANO wa KIKATIBA kupitishwa na Bunge baada ya nafasi hizo kuwa zilitangazwa kwenye magazeti na waombaji kujitokeza.................

  Mchujo utafanywa na Kamati hiyo ya Bunge tajwa..........................


  d) MKUTANO huo wa KIKATIBA unapaswa uwe umemaliza kazi yake katika kipindi cha miaka miwili kwa sababu watapewa mapendekezo mengi kutoka kwa wadau mbalimbali hivyo hawana sababu ya kupoteza muda mwingi katika kukusanya maoni......ingawaje watafanya vikao vya wazi na umma maeneo mbalimbali nchini kukusanya maoni hayo................kwa muda maalumu........................

  e) Baada ya kukamilisha mapendekezo yao watayakabidhi kwa MWANASHERIA MkUU ambaye atapaswa ndani ya siku 90 awe amewakilisha mapendekezo ya sheria ya kujadiliwa Bungeni.......na kupitishwa...................

  f) Baada ya Bunge kuyapitia na kuyapitisha mapendekezo ya Katiba Mpya wananchi wapewe nafasi ya kupiga kura ya maoni...........hivyo tunahitaji sheria ya kura ya maoni kwa kazi hiyo na nyinginezo zitakazojitokeza..................

  g) Iundwe mahakama maalumu ya kusikiliza kero za wananchi juu ya kero za raia zitakazojitokeza wakati mchakato huu wa kuandika katiba mpya unaendelea.................

  Haya ni maeneo machache ambayo ninaona yafaa kuwa ni uangalizi wa kuhakikisha serikali iliyopo madarakani haitutupii changa la macho kwa kuiita ni KATIBA MPYA huku ni KATIBA ya viongozi tu kama zile zilizotangulia...................mwenye mchango wa ziada wa kuboresha haya mapendekezo anakaribishwa................
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  @ Ruta..... ahsante kwa mchango wa the process towards a new draft constitution........ but dont you foresee that we first need to beg some funds to finance from your listed processes a., b., c., d., e., f and finally.. g or suggest where should we get finance?..... i suggest we should use the 18.5 b supposed to pay remedy to Dowans....
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Wajibu wa Bunge utabaki palepale ndugu yangu hilo halikwepeki kwenye suala la katiba, nafikiri hayo maoni ya wananchi wasiojua katiba ni nini wengi wao na ina umuhimu gani yatashawishi wabunge kukubali mabadiliko ya katiba.mawazo mazuri.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Fedha wafadhili wapo kibao ni sisi kujiandaa na mpango madhubuti ambao unakubalika kitaifa...........................Thanks for your input..........
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  mawazo yangu haya yamelitambua Bunge katika kuziunda sheria za kuufanikisha mchakato huu.............Wapigakura wengi wameona ukweli ya kuwa viongozi wengi walipopo madarakani siyo chaguo letu na wap[o hawa kwa kufanikishwa na mfumo wa kidhalimu uliopo na ndiyo maana wanachotaka ni Katiba mpya ingawaje hawajui iweje.........................ni juu ya wasomi na wenye kiona mbali kuwasaidia kwenye hilo..........................hatuwezi tukaa kimya.............................................
   
 6. K

  Kwiifoenda Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 7. K

  Kwiifoenda Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani kasema Watanzania hawajui kuhusu madhaifu ya katiba ya sasa na mambo wanayotaka yawepo kwenye katiba mpya? Hata kama mtu mmoja hawezi kuyatambua madhaifu yote kwa pamoja atasaidiwa na watu wengine! na ukisikiliza mazungumzo ya watu wengi huku mtaani angalau kila mmoja anataja udhaifu mmoja anaoufahamu katika katiba ya sasa, hivyo watu wanaelewa sana kuhusu mambo ya katiba! mawazo na maoni yao yakiunganishwa lazima utakuwa mtaji mkubwa wa kuandikia katiba mpya!
   
 8. n

  niweze JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This is Good One Ruta. Wananchi Kweli Tujipange na Kipindi Hiki CCM Ulimi wa Ulafi Utaishia Hapa. Wananchi Lazima Tuelimishane Sana Jinsi ya Kupambana na "Uundwa wa Tume" na "Utaratibu wa Kufika Kwenye Katiba Mpya" na Mwisho "Kuipigia Kura Katiba Yetu" Tunanzasha TAIFA Jipya kwa Manufaa ya Wananchi
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Safi!
   
 10. n

  ngoko JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Alternatively , The Govt can pay the 18.5b to Dowans and then ask RA and other beneficiaries of the said sum to finance the processes.
   
 11. D

  DENYO JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  umenena mkuu -mkutano wa katiba ndio suluhisho la kupata katiba mpya lakini kwa sababu ya uoga, wasiwasi na udikiteta unaosemwa wanaweza lazimisha kutumia tume, hiyo itakuwa ni kuwa serikali yenye kiburi na isiyo sikivu. Kama wataalam wote wanasema constituional assembly -halafu wao wanalamisha constitutional review commission-huu utakuwa unyonyaji wa lhali ya ujuu usioltakia mema taifa hili
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Katiba Z'bar, Muungano zagongana


  Na Mwajuma Juma, Zanzibar

  WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar, Bw. Abubakar Khamis Bakar amekiri kuwa Katiba ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinagongana.Hivyo, alisema
  kutokana na hali hiyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano inapaswa kuangaliwa upya kwa lengo la kuondosha utata unaojitokeza hasa kwa kuanisha histoia ya nchi mbili zilizounda Muungano.

  Hayo aliyaeleza katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi jana, alipokuwa akijibu suali la mwakilishi wa jimbo la Chaani bw. Issa Jecha Simai, ambaye alitaka kujua wananchi wafuate katiba ipi kati ya mbili hizo kutokana na kuwa zimegongana kiuandishi.

  Alisema kuwa ni kweli kifungu namba 2(a) cha katiba ya Zanzibar kinampa uwezo Rais wa Zanzibar kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maneo mengine kwa kufata utaratibu uliowekwa na sheria na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi na pia ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri inampa uwezo Rais wa Muungano kuigawa Jamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu lakini kwa kwa Zanzibar alilazimika kushauriana na Rais wa Zanzibar.

  Ni kweli kuwa katiba hizi mbili zinazogongana kiuandishi na hivyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano inapaswa kuangaliwa upya ili kuondoa utata huo hasa katika kuainsisha historia ya nchi mbili hizi na kuainisha mamlaka na majukumu ya
  serikali hizi mbili kulingana na Mambo ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano kwa kila upande, alisema.

  Aidha alisema kwamba upande wa Mambo ya Muungano, katiba inayopaswa kufuatwa ni ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mambo Yasiyohusu Muungano, kwa Zanzibar, katiba inayopaswa kufuatwa ni ile ya Zanzibar ya mwaka 1984 kama ilivyorekebishwa kwa nyakati mbalimbali.

  Hata hivyo, alisema kuwa Marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yamezingatia zaidi maamuzi ya wananchi kuhusu mfumo mpya wa serikali, ambao utendaji wake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa
  kw umoja nchini kwa lengo la kufikia demokrasia.

  [​IMG]
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Akiri Katiba ya Z'bar, Muungano kugongana Thursday, 20 January 2011 20:47

  Salma Said, Zanzibar
  WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari, amekiri katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinagongana kiuandishi.

  Alisema kutokana na hali hiyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano inapaswa kuangaliwa upya kwa lengo la kuondoa utata unaojitokeza, hasa kwa kuanisha histoia ya nchi mbili zilizounda Muungano huo.

  Alikuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Chaani, Issa Jecha Simai, aliyetaka kujua katiba ambayo inatakiwa kufuatwa na wananchi kutokana na zilizopo kugongana kiuandishi.

  Waziri Abubakar alikiri kifungu namba 2(a) cha katiba ya Zanzibar kinampa uwezo Rais wa Zanzibar kugawa Zanzibar kwenye mikoa, wilaya na maeneo mengine kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

  Pia, ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri inampa uwezo Rais wa Muungano kuigawa Jamhuri ya Muungano kwenye mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu, lakini kwa Zanzibar analazimika kushauriana na Rais wa Zanzibar.

  "Ni kweli katiba hizi mbili zinazogongana kiuandishi, hivyo katiba ya Jamhuri inapaswa kuangaliwa upya ili kuondoa utata huo, hasa kuainisha historia ya nchi hizi mbili na kuainisha mamlaka na majukumu ya serikali hizi mbili kulingana na mambo ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano kwa kila upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema.

  Alisema upande wa mambo ya Muungano, katiba inayopaswa kufuatwa ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na mambo yasiyohusu Muungano kwa Zanzibar, katiba inayopaswa kufuatwa ni ile ya Zanzibar ya mwaka 1984 kama ilivyorekebishwa kwa nyakati mbalimbali.

  Hata hivyo, Waziri Abubakar alisema marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, yamezingatia zaidi maamuzi ya wananchi kuhusu mfumo mpya wa serikali, ambao utendaji wake utafanywa kwa utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini kwa lengo la kufikia demokrasia.
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Migongano ya katiba ya Muungano na ya Zanzibar ni uthibitisho mwingine ya kuwa michakato ya marekebisho ya katiba zetu siyo shirikishi hata kidogo...................................Mkutano wa kikatiba uliowekwa kisheria tu ndiyo utamaliza vurugu hizi zote................
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Kongamano la Katiba lilivyoleta msisimko
  [​IMG]

  Nasra Abdallah

  [​IMG] HIVI karibuni Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) iliandaa kongamano kuhusu mchakato wa uundaji wa katiba mpya.
  Katika kongamano hilo watoa mada wakuu walikuwa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji na Mwandishi mkongwe wa habari, Jenerali Ulimwengu ambao walianza kuchokonoa mada kwa kueleza historia, dhana na haja ya kuwa na katiba mpya.
  Profesa Shivji anasema lengo la kuanzishwa kwa Udasa ni kutetea maslahi ya wanyonge kwa kuendesha mijadala yenye maslahi kwa taifa itakayojenga hoja na si jazba hivyo suala la kujadili uundwaji wa katiba mpya ni kati ya jukumu lao.
  Maana na dhana ya Katiba
  Anasema zimekuwepo tafsiri nyingi kuhusu maana ya katiba ikiwemo ile inayosema ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa, tafsiri ambayo kwa sasa inaonekana kupitwa na wakati.
  Anafafanua kuwa maana sahihi na dhana ya katiba ni kielelezo cha muafaka wa kitaifa ambapo jamii, watu watakubaliana misingi mikuu ya kiuchumi na kijamii katika kuendesha nchi yao.
  Chimbuko linatokana na wananchi hivyo katiba itabaki kuwa mali ya wananchi, hivyo kutokana na uundwaji wake na ni muhimu katiba ikapita mikononi mwa wananchi.
  Kwa nini Katiba mpya?
  Anasema zipo sababu zinazosababisha katiba mpya kuundwa ikiwemo madai ya kupitwa na wakati pamoja na kuwepo kwa gazeti moja lililodiriki kuandika mapungufu 90 yanayoonekana katika katiba ya sasa, jambo ambalo iwapo angepata nafasi ya kuorodhesha yangefika 200 .
  Anasema hoja nyingine ni ile inayoonyesha katiba kuwa na viraka jambo ambalo serikali inaweza kuifanyia tu marekebisho.
  Profesa Shivji anasema kuwa kama ndivyo kuna katiba za nchi nyingine ambazo zinamiaka mingi ikiwemo ya India ambayo ina miaka 60.
  Anasema kwamba wengi wanaotoa kasoro hizo hawajasoma katiba ya sasa vizuri.
  "Kwangu mimi sioni kama katiba ina mapungufu ila ninachohitaji ndugu zangu ni kuundwa kwa katiba mpya hoja kubwa ikiwa ni kwamba zote zilizopita hazikushirikisha wananchi kama ambavyo tafsiri inasema," anasema.
  Historia fupi ya katiba iliyopo
  Profesa Shivji anasema kwa kipindi cha miaka 50 tangu tupate uhuru, nchi ishawahi kuwa na katiba tano ya kwanza ikiwa ya mwaka 1961 iliyojulikana kwa jina la katiba ya uhuru ambayo ilitungwa na Waingereza kwa maslahi yao.
  Katiba nyingine ni ya mwaka 1962 ambapo ilitungwa na Bunge la wakati huo na kupitishwa kama sheria kuu ambapo wakati huo wabunge 71 walikuwa wanatoka chama cha TANU.
  Katiba ya 3 ni ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa na lengo la kupatanisha muungano na Rais ndiye aliyepewa madaraka ya kuitunga.
  Pia anasema mwaka 1965 Bunge lilitunga katiba ya 4 ambayo iliitwa katiba ya chama kimoja na ya 5 ni ile ya mwaka 1977 chimbuko lake likiwa ni mapatano ya Muungano, ambapo ilijadiliwa kwa saa 3 tu na kupitishwa kuwa sheria mama.
  Kwa mujibu wa Profesa Shivji anasema katiba hizo zote hazijashirikisha wananchi na hivyo hazikuwa na uhalali wa kuwepo.
  Anasema katiba itakayoundwa ni muhimu ikashirikisha wananchi ndiyo itakuwa uhalali wa kisiasa na kisheria ili wapate katiba yao.
  Profesa Shivji anaeleza kuwa mchakato huo lazima wananchi waachwe wajadili, waelimishwe bila ya kutishwa ili waanze na mijadala midogomidogo na kuhitimisha kwa mkutano mkuu.
  Anasema mchakato wa pili unatakiwa kupitia bungeni na kumalizia kwa mkutano wa kura za maoni kama chombo maalumu cha maamuzi ya uundwaji wa katiba mpya.
  Hata hivyo anatahadharisha kwa vyama vya upinzani kutokubali suala la mjadala wa uundwaji wa katiba mpya lipelekwe bungeni kwa kuwa ni sawa na kuamua hoja hiyo ikaamuliwe na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao wana viti vingi.
  Anasema ni bora suala hili likabakia mikononi mwa wananchi na kwani itakuwa rahisi kutoa shinikizo kwa rais katika kuundwa katiba hiyo kuliko kushinikiza Bunge.
  Anavitaka vyama vya siasa kuangalia suala hilo kwa upana zaidi badala ya kuingiza siasa zaidi.
  Hoja Shivji ilikuja baada ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA), kuonyesha wasiwasi juu ya kutaka lipelekwe bungeni kwanza kwa madai ya kufanyiwa marekebisho baadhi ya vipengele vya sheria Ibara ya 98, inayosema Bunge ndilo lenye mamlaka ya kubadilisha katiba.
  Hata hivyo Shivji akitolea ufafanuzi hoja hiyo anasema bunge halina uwezo wa kupinga katiba na kwenye katiba hakuna sheria inayopinga mjadala wa kitaifa kama huu wa kujadili katiba mpya.
  Anasema hata ikitokea mchakato huu ukapelekwa bungeni, kamwe sheria hizo hawawezi kuzifanya zibadilishwe.
  Kwa upande wake kada wa CHADEMA, Mabere Marando, anasema kuwa mpaka sasa katiba mpya imeanza kuandikwa kutokana na tukio la vurugu zilizotokea hivi karibuni mjini Arusha.
  Marando anasema damu iliyomwagika katika vurugu hizo ndio wino wa kwanza wa kuandikia dibaji ya katiba hiyo huku harakati zikiendelea.
  Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, anasema mada aliyoitoa Profesa Shivji kwamba uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere ulikuwa na uhalali kutokana na kupendwa na sio katiba iliyomuweka madarakani, lakini hakuelezea kuhusu uhalali wa viongozi waliomfuata nyuma.
  Lipumba anasema katika ilani ya CCM hakukuwa na suala la katiba wala katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa bungeni hapakuwa na suala hilo hivyo kuna haja ya kuwa na mshikamano katika suala hilo kwani bila ya hivyo nchi inaweza kuingia kwenye machafuko.
  Kwa upande wake, Jenerali Ulimwengu anasema katiba msingi wake ni falsafa za Waingereza na kuongeza kuwa pamoja na mabadiliko mbalimbali yaliyowahi kufanywa hakuna hata katika mabadiliko hayo kushirikisha wananchi.
  Ulimwengu anasema haoni kama kuna gharama kubwa ya mchakato wa kuundwa kwa katiba ukilinganisha na machafuko yanayoweza kutokea baadaye.
  Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya, anaonyesha wasiwasi wa ushiriki wa wanawake katika mjadala huo wa uundwaji wa katiba mpya.
  Anasema kwa muda mrefu anafuatilia mijadala hiyo hata katika vyombo vya habari lakini suala la ushirikishwaji wa wanawake limekuwa dogo ukilinganisha na wanaume.
  Anaitaka serikali kuhakikisha inawekeza kwa wananchi ili kujua ni nini kilichopo katika katiba iliyopo kwanza kwa kutumia redio, televisheni na magazeti inayoyamiliki kwa kutoa elimu kupitia vipindi mbalimbali.
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Katiba mpya, nani, nini, namna gani?
  [​IMG]

  Deus Bugaywa

  [​IMG] ‘POLITICS are too serious matters to be left to politicians alone.'
  Nimeamua kufungua safu hii leo na nukuu hiyo inayomaanisha kwamba masuala ya siasa ni mambo nyeti sana kiasi kwamba hayapaswi kuachwa mikononi mwa wanasiasa peke yao.
  Ni ukweli mtupu kwamba masuala mengi yanayohusu siasa, hata kama wahusika wake wanaoonekana wazi ni wanasiasa lakini yanatuhusu wote, bila kujali kama tunafahamu hilo au kinyume chake.
  Taifa sasa liko katika mchakato wa mabadiliko ya katiba, tuko katika kipindi ambacho taifa linaelekea katika kufikia hatua ya kuandika katiba mpya ambayo itaakisi mahitaji ya makundi yote katika jamii.
  Katiba ni nyaraka muhimu sana kwa ustawi wa taifa lolote lile, kwa kuwa Katiba siyo tu ni mkataba wa kijamii, lakini pia inapaswa kuwa ni mwongozo wa jinsi jamii inavyotaka iendeshe mambo yake kisiasa, kijamii, kuchumi.
  Kwamba kupitia katiba wananchi wanawapa mamlaka yao watawala au viongozi ili kuweza kupata utangamano na ustawi katika jamii kwa mfumo wa sheria na taratibu ambazo zinatenda haki kwa kila mmoja bila upendeleo wa ana yeyote ile katika kutimiza yale ambayo jamii imekubaliana.
  Kwa mantiki hiyo, mjadala kuhusu kuandikwa kwa katiba mpya ni wa kila mwananchi kwa maana kwamba kila kundi katika jamii lishiriki kikamilifu katika kutoa maoni yake ni aina gani ya katiba tunaitaka.
  Hili hata hivyo, haliwezi kuwa jambo rahisi hivyo kwa kuwa ni lazima kwanza wananchi wafahamu zana nzima ya katiba na maana yake kwa maisha yao kila siku.
  Wanapaswa pia kufahamu vyema katiba iliyopo na kujua mapungufu yake na athari za mapngufu hayo kwa jamii yote, na zaidi sana wayaondoe na kuweka yale ambayo yataondoa au kupunguza kwa kiwango kikubwa mbinyo wa demokrasia.
  Bila shaka hili ni jukumu la kila mwenye uwezo wa kuyafafanu haya kwa wananchi akafanya hivyo kwa nia njema bila kutanguliza siasa wala ushabiki isipokuwa kwa maslahi ya taifa hili.
  Si kwa nia mbaya, lakini uzoefu umeonesha hivyo, kwamba katika mijadala ya namna hii, wanasiasa si aina ya watu ambao tunatakiwa tuwategemee sana katika kuendesha zoezi hili hasa la kuwaelimisha wananchi juu ya masuala mazima yanayohusiana na katiba.
  Sababu ziko wazi, wanaweza kabisa kutumia mwanya huu kutoa maoni au hata kushinikiza vitu fulani vifanyike au viwekwe kwenye katiba mpya siyo kwa sababu vinaweza kusaidia kujenga misingi imara ya ustawi wa taifa hili kiuchumi, kijamii na kidemokrasia isipokuwa kwa sababu tu anaona mwanya wa kufadika hapo baadaye.
  Ndiyo maana kwa maoni ya safu hii, huu ni wakati wa wataalamu na wanazuoni mbalimbali kutoka huko walikojifungia waanze kazi ya kuwamulikia jamii wapate mwanga hasa wa nini kinapaswa kifanyike katika kuandika katiba mpya.
  Ni vizuri pia kuwaelewesha waanchi mapema watambue kwa hili si zoezi jepesi na la muda mfupi kiasi hicho. Ukipita pita mitaani unaona matumaini ya wananchi ni kama katiba mpya itakuja mwaka ujao tu.
  Tuwasaidie na tuwaadae watu wetu waujue mlolongo mzima wa zoezi hili litapitia hatua zipi kwa muda gani na kufuatiwa na hatua ipi mpaka hatimaye tutakapopata katiba tunayoitaka.
  Mamlaka zinazohusika na mpangilio mzima wa namna zoezi hili litakavyoendeshwa zinapaswa zitoe utaratibu kamili na muda unaokadiriwa zoezi hili kuchukua, tunajua kutakuwa na tume au baraza la katiba litakalokuwa na jukumu la kukusanya maoni, kutakuwa na uchambuzi wa maoni na mambo mengine mengi mpaka kufikia hatua ya kuipigia kura rasimu ya katiba husika (referendum).
  Haya yote yanatakiwa yafahamike kwa wanachi kungali mapema ili waweze kujiandaa kushiriki vyema zoezi hili, tusifanye makosa ya kulifanya zoezi hili kama vile limekuja kwa bahati mbaya, tuandae mazingira ya kuwafanya wananchi waelewe nini kinaendelea na tuwaweze kushiriki kikamilifu.
  Ni kwa njia hiyo tunaweza kuwa na katiba ya wanananchi, haitakuwa na maana wala sababu kuandaa katiba mpya katika mazingira ambayo idadi kubwa ya wananchi hawaijui katiba yao, katika hali ya namna hii hata hiyo mpya itakosa uhalali wa kuwa katiba ya wananchi kama sehemu kubwa ya watu hawajui nini kinaedelea.
  Kwa umuhimu wake zoezi hili linapaswa kwa hakika kufanywa kwa umakini mkubwa na wa hali ya juu, ukereketwa wa siasa hauna maana katika kuendesha jambo hili, kama tunatengeneza Katiba ya Tanzania ni lazima pia tuje pamoja kama Watanzania.
  Tunaweza kuwa katika makundi mbalimbali ya kijamii, lakini msingi wa mchango wetu katika katiba uwe ni ustawi wa Tanzania na si maslahi binafsi ya kundi fulani maalumu bila kujali makundi mengine yanaathirika vipi na kupendelea kundi letu. Viongozi wa taasisi na makundi mbali mbali katika jamii yakiwemo ya dini, siasa, wanawake, vijana, walemavu na mengine yote, waanze kwanza kuwaelimisha wafuasi au wananchama wao maana na umuhimu wa katiba mpya na wayajue matatizo ya katiba ya sasa badala ya tu kukaa wao na kutoa mapendekezo yao bila kuwashirikisha kikamilifu wale wanaowawakilisha.
  Ili katiba hii iwe kweli msingi imara wa ustawi wa taifa letu ni lazima kila mmoja wetu atambue yeye ni nani, na nini mchango wake katika mjadala huu na atautoa namna gani, tukiyaweka sawa haya kwa hakika tutakuwa tumeweza kuvuka hatua ya kwanza ya kuweka mazingira mazuri ya uandikwaji wa katiba yetu.
  Kwa wananchi ni lazima sasa ninyi pia muanze kufanya juhudi za makusudi kujibidiisha katika kuutafuta ukweli na kujua chochote usichokijua kuhusu katiba ili muweze kujiweka tayari kwa ajili ya mabadiliko haya makubwa kwa taifa letu.
  Siyo tu kwamba kila mwananchi ana haki ya kufahamu na kuchangia kwa namna yake mabadiliko haya ya katiba lakini pia ni wajibu wa kila raia mwenye mapenzi mema, kuhakikisha kwamba haachwi nyuma na upepo huu wa mbadiliko unaopita katika Tanzania, hapa, kwenye uandishi wa katiba ndipo mahali mtu unaweza kufanya kosa moja ukalijutia siyo tu siku zote za maisha yako, lakini pia na kizazi chako.
  Ni vyema basi kila mtu akahakikisha kuwa anaijua nafasi yake vyema katika mchango huu na aitumie kikamilifu kwa manufaa ya taifa zima na vizazi vijavyo, kwa kuwa hapa ndipo tunapoweka misingi ya Tanzania ya miaka hamasini ijayo.
  Wewe ni nani, nini wajibu au mchango wako katika katiba mpya, unautimiza wajibu huo kwa namna gani? Haya ni maswali ya msingi kujiuliza kwa kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka kumi na nane kama una majibu yake, ni vyema una kazi moja tu, kutimiza wajibu wako.
  La kama bado haujajua nini hasa unapaswa kufanya na hauna majibu sahihi kwa maswali hayo, bado haujachelewa anza kutafuta majibu yake usaidie kuijengea Tanzania misingi imara ya ustawi wa kidemokrasia, kijamii na kiuchumi ambayo itadumisha umoja na mshikamano wa Watanzania wote bila kujali tofauti zao za makundi, dini au makabila.
  Mungu ibariki Tanzania, wabariki watu wake.
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Mtandao umemomonyoa maadili ya taifa-Wadau


  Na Jumbe Ismailly, Singida

  WADAU wa kongamano la kujadili Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 wamesema moja ya sababu zinazochangia mmomonyoko wa maadili kwa
  viongozi wa serikali ni uteuzi mbaya unaofanywa kwa kuangalia watu waliopo kwenye 'mtandao' wa kambi ya kiongozi mwenye mamlaka ya uteuzi.

  Wadau hao kutoka taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na kijamii waliyasema hayo kwenye semina iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA), mjini Singida.

  Wadau hao, Bw. Ivo Manyaku, Bw. Emmanueli Misholi na Bw. Eugen Shao waliweka bayana kuwa umefika wakati badala ya kuendeleza tabia ya kutoa madaraka kama takrima, wenye mamlaka waanze
  kuangalia watu wenye maadili mema.

  Bw. Misholi alibainisha kwamba wakati wa uchaguzi kulikuwa na makundi ya kampeni kwa wagombea wa nafasi mbalimbali, hali inayofanya wenye mamlaka ya kufanya uteuzi wa viongozi kupata na vigugumizi na kutaka kutoa takrima kwa waliowasaidia.

  Kusiwe na kutafutiana takrima kwa sababu uchaguzi umeisha, ifike wakati sasa tafuteni watu wenye maadili mema muwape nafasi ambazo ni dhamana kwa
  ajili ya taifa hili, ili wautengeneze upendo kwa watu,� alibainisha Bw. Misholi.

  Bw. Misholi aliweka bayana kuwa siyo rahisi kuhubiri upendo kwa mdomo wakati kwa matendo yao wana mmomonyoko.

  Ndiyo maana Nyerere alikuwa anaangalia, wakati mwingine utakuta mwalimu anatolewa wapi huko (asiyefahamika) na kufika mahali watu mnamshangaa.

  Halafu anafanya maajabu, lakini sasa hivi mambo yameshakwisha, sasa hivi tunatengeneza network (mtandao) kama mtu haupo kwenye mtandao hauwezi kwenda kokote kule,� alisisitiza.

  Alisema kutokana na dhana hiyo ya 'mtandao', viongozi wasiokuwa na maadili wameendelea kupatikana, na hivyo kuhoji endapo mtu akipatikana kwa njia ya rushwa, kitu gani atarajiwe kukifanya akiwa madarakani.

  Kwa upande wake Bw. Manyaku alisema kuanzia ngazi ya kijiji, kata, wilaya, mkoa mpaka taifa hakuna maadili, hali ambayo amaesema imesababisha hali ya uchumi wa nchi kuyumba.


  Hii imesababisha hata uchumi wetu kuyumba kwa sababu sasa ni suala la wizi, ufisadi, rushwa, utaifa hakuna watu waliopewa mamlaka na dhamana mbalimbali katika nchi hawana utaifa, wana
  umimi,รข€� alisisitiza Bw. Manyaku.

  Kwa mujibu wa msemaji huyo malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 hayawezi kufikiwa kwa sababu kila mmoja anaona kuwa akipata nafasi
  anadhamiria kuanza kujinufaisha kwanza mwenyewe.

  Naye Bw. Shao alisema kutokana na ubinafsi uliopo kwa idadi kubwa ya viongozi walipo madarakani, wamekuwa hawatendi haki katika dhamana walizopewa kwa manufaa ya wananchi.

  [​IMG]
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Hivi maadili yetu ni yepi........................................Ujenzi wa maadili utaanza pale tutakapokuwa na katiba ambayo misingi yake imejengwa kwa kuwashirikisha watanzania walowengi na ambao ni mafukara wa kutupwa.................
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Kuyumba maadili chanzo cha gulio la kura - Mbowe


  na Grace Macha, Hai


  [​IMG] MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe, amesema kuyumba kwa maadili nchini kumesababisha kuwepo na gulio la kununua kura za wananchi ili kupata nafasi za kuongoza.
  Mbowe alisema hayo mwishoni mwa wiki kwa nyakati tofauti alipokuwa kwenye mikutano ya kuwashukuru wananchi wa jimbo la Hai kwa kumchagua kuwa mbunge wao pamoja na kusikiliza kero zao kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.
  Alisema jambo hilo ndilo linalochangia watu wasio na sifa wala uwezo kuchaguliwa kuongoza hali inayosababisha viongozi kutowajibika kwa wapiga kura wao kutokana na ukweli kuwa kilichowaweka madarakani ni fedha zao walizotumia kununua kura.
  "Uongozi ni dhamana unayopewa na wenzako lakini leo umeingia sumu umegeuka mnada wa kura; mwenye fedha za kugawa na kununua pombe, chakula na vitu vidogovidogo visivyo na maana yoyote na kugawa kwa wananchi anapewa nafasi kubwa ya kuchaguliwa.
  "Lakini athari yake ni kubwa kwa sababu kiongozi aliyenunua uongozi anasema ‘si ni hela yangu imeniweka hapa!' hivyo hana haja ya kurudi kwa waliomchagua, lakini mimi kwa kuwa sikuwapa chochote ili mnichague ila mmenichagua kwa mapenzi na imani yenu kwangu na kwa tulikubaliana kushirikiana kwenye kutatua kwa pamoja changamoto zinazotukabili hivyo ninatekeleza wajibu kwa kuja kuwashukuru kwa kunichagua na tukae tuweke mikakati ya kusonga mbele.
  "Nawashukuru kwa kuniamini na kunichagua na kwa wale walioninyima kura nawaombea Mungu awape maisha mazuri na marefu ili waniangalie nikipiga mzigo kwa miaka mitano halafu wanipime kama walininyima kura kihalali au walinionea; natumaini baada ya hapo nao watanipigia kura," alisema Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.
  Akizungumzia tukio lake la kukamatwa na kushtakiwa jijini Arusha, Mbowe aliwataka wapiga kura wake kutompa pole bali wazidi kumuombea kwa Mungu ampe nguvu za kuendelea kupambana na udhalimu na ufisadi nchini mpaka hatimaye haki ipatikane na kila mwananchi anufaike na rasilimali za taifa.  [​IMG]

   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Sumaye: Dhamira ya Mnyika kuhusu katiba isibezwe
  Monday, 24 January 2011 23:56

  Felix Mwagara
  DHAMIRA ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika kutaka kuwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu katiba mpya, imemkuna Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, ambaye amempongeza kwa uamuzi huo aliouita kuwa wa busara.

  Juzi katika mahojiano na waandishi wa habari, mtendaji huyo wa serikali ya awamu ya tatu, alizungumzia suala la katiba mpya na alifanya hivyo baada ya hafla ya kusherehekea kumalizika kwa mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011.

  Hafla hiyo ilikuwa imeandaliwa na wanachama wa Umoja wa Wananchi wa Wilaya za Mbulu, Babati, Hanang na Karatu, (NORIVADA) na kufanyika katika ukumbi wa JWTZ Lugalo, jijini Dar es Salaam.

  Sumaye alisema wazo la kutaka kuwepo kwa katiba mpya si haramu hasa ikizingatiwa kuwa ni ya muhimu katika kutoa huduma kwa wananchi.


  "Mimi ningekuwa mbunge si lazima niwe mbunge wa upinzani, hata mbunge wa CCM, ningepeleka hoja ya katiba bungeni. Lakini nashukuru kwamba Mnyika amefanya hivyo, namshukuru," alisema Sumaye.

  Alielezea matumaini yake kuwa wabunge watajadili hoja hiyo kwa kina ili kuiwezesha kamati itakayoundwa na serikali kuratibu mawazo ya wananchi, kuwa na mahali pa zuri pa kuanzia.

  Waziri mkuu huyo mstaafu, alisema kupitia kamati hiyo, wananchi watakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu katiba inayopendekezwa, ambayo alisisitiza kuwa si haramu.

  Alisema watu hawapaswi kumbeza Mnyika kwa azma yake ya kutaka kuwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu suala hilo na badala yake, wampe moyo na kumuunga mkono.

  Kuhusu baadhi ya mawaziri wa serikali kupingana hadharani juu ya mambo mbalimbali yanayohusu utendaji wa serikali, Sumaye alisema "kuna mambo ya uwajibikaji wa pamoja katika serikali, lakini pia mtu ana utashi wa kuzungumza analoona linafaa.


  "Kuna msimamo wa serikali na pia kuna maoni ya watu, kila mtu ana utashi, si kwamba ukiwa waziri usizungumze," alisema Sumaye.

  Hivi karibuni, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mathias Chikawe, alisema ni kosa kwa mawaziri kupingana hadharani na kwamba kama kuna mwenye dukuduku, anapaswa kufuata taratibu za kuwasilisha maoni yake.

  Pia Sumaye alizungumzia hatua ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kukutana na wabunge wa CCM, ambapo alisema hilo ni jambo la kawaida kwa wabunge wakiwemo wa vyama vingine.
  Katika hotuba yake kwa watu wa Babati, Mbulu, Hanang na Karatu, Sumaye aliwataka wananchi wanaoishi Dar es Salaam wawe na moyo wa kusaidia watu wa vijijini ili nao waondokane na umasikini

  "Ombi langu ni kwamba tuwe tunapiga darubini kule tunakotoka, hata kwa kusaidia wazo, inatosha,"alisema Sumaye ambaye aliwataka wananchi wawe na moyo wa kuendelea kusaidiana katika mambo mbalimbali yakiwemo misiba na elimu.


   
Loading...