Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,172
- Thread starter
- #21
Wafungwa wataka Katiba mpya
na Sitta Tumma, Mwanza
MOTO uliowashwa wa kudai Katiba mpya, umezidi kushika kasi kubwa hapa nchini, ambapo safari hii wafungwa na mahabusu wa gereza la Musoma, mkoani Mara, wameungana na Watanzania wenzao kudai kuundwa kwa Katiba hiyo mpya ya Jamhuri ya Muungano, na kusema hiyo ndiyo itakayokuwa suluhisho la matatizo na ucheleweshwaji wa kesi mahakamani.
Kana kwamba hiyo haitoshi, wafungwa hao pia wamepinga vikali mpango wa serikali kutaka kuilipa sh bilioni 94 kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans, wakisema kulipwa kwa kampuni hiyo ni sawa na wizi wa waziwazi, jambo ambalo wameapa kugoma kula iwapo serikali itailipa kampuni hiyo inayosadikiwa kuwa ni ya kitapeli.
Wamesema, suala la kuundwa kwa Katiba mpya hapa nchini haliepukiki hata kidogo, kwani matatizo, umaskini na masuala mengi ya kifisadi yanatokana na ubovu wa Katiba iliyopo hivi sasa, hivyo wanaamini ikiundwa Katiba mpya mlundikano wa kesi mahakamani na watu kubambikiziwa kesi hakutakuwepo tena.
Wafungwa na mahabusu hao waliyasema hayo juzi mjini hapa, baada ya mbunge wa Jimbo la Musoma mjini, Vincent Josephat Nyerere (CHADEMA), kutembelea gereza hilo kwa lengo la kuwasalimia na kupokea kero kutoka kwa watuhumiwa hao.
Akizungumza na Tanzania Daima muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na wafungwa na mahabusu hao gerezani, Nyerere alisema kwamba wamemtuma kwenda bungeni kuwasilisha kero na matakwa yao ya kuundwa kwa Katiba mpya pamoja na kupinga serikali kuilipa mabilioni ya fedha kampuni ya Dowans.
"Kikubwa walichonieleza ndugu zetu wafungwa na mahabusu, wanataka Katiba mpya, pia hawataki kusikia serikali imeilipa Dowans...na wanasema Katiba mpya itasaidia kuondoa mlundikano wa kesi pamoja na raia wema kubambikiziwa kesi," alisema mbunge huyo wa Musoma Mjini, Nyerere, ambaye alishabatizwa jina la ‘Obama' wa Musoma.
Mbunge huyo wa Musoma mjini ambaye katika ziara yake hiyo ya kuwatembelea na kuwasalimia wafungwa wa gereza hilo la Musoma, alikuwa ameambatana na mbunge wa Jimbo la Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Dibogo Wenje (CHADEMA), aliyekuwa amezuru mjini hapa, kwa mazungumzo maalumu na Nyerere.
Mbunge Nyerere alisema, wafungwa hao wanahitaji kuona Tanzania inapata maendeleo makubwa yatakayotokana na mabadiliko ya Katiba ya nchi na kwamba ni vema suala hilo likafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo na viongozi wa kiserikali wanaokataa kuundwa kwake, hawana budi kujiuzulu nyadhifa zao.
Aliongeza kusema kwamba: "Wametutuma mimi na Nyerere na Wenje tutakapokwenda bungeni tuhakikishe tunaibana serikali ifanye kila namna kuruhusu rasimu ya Katiba iandaliwe haraka na Katiba mpya iwe imekamilika kabla ya mwaka 2015."
Kuhusu Dowans, wafungwa hao walimweleza mbunge wao huyo wa Musoma mjini kwamba fedha ambazo serikali inataka kuilipa kampuni hiyo inayodaiwa kuwa ni ya kitapeli, ni vema zikaelekezwa kuajili na kuwalipa mishahara majaji na mahakimu, ili kuiwezesha mahakama kuwa na majaji wengi watakaoharakisha maamuzi ya kesi.
"Hawa ndugu zetu walio gerezani wanataka hizi bilioni 94 zinazotaka kulipwa Dowans zielekezwe kuajili majaji na mahakimu ili kesi ziwe zinaamuliwa haraka zaidi," alisema mbunge huyo wa Musoma mjini.
Hata hivyo, kabla ya kutembelea gerezani hapo, wabunge hao, Nyerere na Wenje walihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya shule ya Mkendo Musoma mjini ambapo kilio kikubwa cha maelfu ya wananchi hao kilikuwa ni kutaka Katiba mpya, kupinga kulipwa kwa Dowans pamoja na umaskini hapa nchini.