Mkutano wa Kenyatta na Odinga umezua mgawanyiko katika upinzani Kenya?

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga walipokutana ghafla Ijumaa na kuahidi kuweka kando tofauti zao kwa maslahi ya taifa, hilo lilitazamwa na wengi kama ishara ya mwisho wa wingu la siasa ambalo limegubika taifa hilo tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka jana.
DX78cZ8WkAAIFKj.jpg

Bw Kenyatta na Bw Odinga waliitana "ndugu" na wakakubaliana kuundwe mpango wa pamoja wa kuangazia utekelezaji wa malengo ya pamoja ya viongozi hao wawili, ambao utazinduliwa rasmi karibuni.

"Huu ni mwanzo mpya kwa taifa letu," alisema Bw Kenyatta baada ya mkutano huo, akisisitiza kauli ya Bw Odinga kwamba "Tumekuja pamoja na ndugu yangu Kenyatta, tumeongea kwa kirefu na kukubaliana kwamba tunataka kuunganisha Kenya iwe taifa moja."

Katika mkutano wao, kuna wahusika ambao hawakuwepo ambao wengi walisubiri kusikia kauli yao.

Katika Muungano wa National Super Alliance (Nasa) ambao ulibuniwa mwaka jana, Bw Odinga alikuwa na viongozi wengine wa vyama vya upinzani, hususan makamu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka ambaye ni kiongozi wa chama cha Wiper Democratic Movement of Kenya Musalia Mudavadi wa Amani National Congress (ANC) na Moses Wetangula wa chama cha Forum for the Restoration of Democracy-Kenya (Ford-Kenya).

Wote wamekuwa viongozi wenza wa muungano huo.

Punde baada ya mkutano huo kufanyika, walikutana na kutangaza kwamba hawakuwa na habari kuhusu mkutano huo wa bw Odinga na Bw Kenyatta.

Kwenye taarifa ya pamoja, walisema hawana ufahamu kuhusu iwapo mazungumzo hayo ni sehemu ya mazungumzo ambayo Nasa, kama muungano wa siasa, umekuwa ukishinikiza kwamba yanafaa kufanyika kati ya serikali na upinzani.

"Asubuhi ya tarehe 9 Machi 2018, tuliona kwenye vyombo vya habari mkutano kati ya Bw Uhuru (Kenyatta) na Bw Raila Amolo Odinga...Ingawa tumekuwa tukisisitiza mazungumzo yafanyike, sisi kama viongozi wenza wa Muungano wa Nasa, hatukuwa na ufahamu kuhusu majadiliano hayo yaliyofanyika Jumba la Harambee (Afisi ya Rais)," taarifa yao ilisema.

Taarifa kwenye vyombo vya habari kenya zinasema Bw Odinga hajazungumza na viongozi wenzake watatu kuhusu yaliyojadiliwa katika mkutano wake na Bw Kenyatta Ijumaa.

Gavana wa Mombasa Hassan Joho ambaye ni katibu mkuu wa chama cha ODM chake Bw Odinga aliingia kwenye mitandao ya kijamii kujaribu kuondoa utata ambapo aliahidi wafuasi wa chama hicho kwamba wana imani na uongozi wa chama hicho.

Lakini mshauri wa zamani wa Bw Odinga ambaye alitia idhini hati yake ya kiapo alipojiapisha kuwa 'Rais wa Wananchi' mwezi Januari na akafurushwa Kenya na serikali na kupelekewa Canada alieleza hatua hiyo ya Bw Odinga kama "usaliti".

"Hauwezi kuwa na mazungumzo na mtu ambaye hamko katika ngazi sawa," alisema.

_100375127_e85261e7-a2c6-468f-a9ff-4aed06c3ade7.jpg


Bw Musyoka, Bw Mudavadi na Bw Wetangula walikuwa wamedokeza kwamba wangetafuta ufafanuzi zaidi kuhusu mazungumzo ya Ijumaa wakati wa mkutano mkuu wa muungano huo ambao ulikuwa umepangiwa kufanyika leo Jumatatu.

Dalili za mgawanyiko zilianza kuonekana pale taarifa za vyombo vya habari zilipodokeza kwamba kulikuwa na uwezekano Bw Odinga angesusia mkutano huo

Lakini Bw Odinga amefika kwa mkutano huo unaofanyika Athi River.

Wakenya sasa, na zaidi wafuasi wa upinzani, wanasubiri kusikia taarifa ya viongozi hao baada ya mkutano wao.


Chanzo: BBC Swahili
 
Mgawanyiko upo kwa Miaka 54 sasa, Hata kama hawa wawili watapigana mabusu na watoe nguo walale kitanda kimoja, Mgawanyiko upo.
There should be quick action on corruption, Land reforms, and Bridge the Gap between rich and poor
 
Kwani sasa hivi Kenya kuna upinzani? Au ni kongomano tu la watu ambao wamechanganyikiwa. Kama NASA wangeshinda uchaguzi ulopita, sasa hivi Kenya kungekuwa na upinzani ambao unaeleweka. Jukumu la upinzani, ambalo lipo kwenye katiba, wangekuwa wanalitimiza vinavostahili. Sio hawa jamaa wa kurusha rusha midomo ovyo ovyo na kudensi kwenye mazishi.
 
I think most people fail to realize that there is no permanent enmity in politics..There is only permanent mutual benefit/interests within politicians despite the party...That is why there is no point in fighting to the death for any politician...Most politicians are generally spineless and seek out for number one, which is mostly themselves...They are masters of reinvention......A politician who doesn’t understand this is only up for dissaapointment and disillusionment...I think the other co-principals don’t get this trick..Honor means nothing to this breed of humans..Politics is not for the faint hearted...There might be a few Mandela’s left but very few...Most are just tumbocrats...
 
Back
Top Bottom