Mkutano wa JK wafunga shule tano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa JK wafunga shule tano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RayB, Oct 27, 2010.

 1. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mkutano wa JK wafunga shule tano
  Tuesday, 26 October 2010 21:08

  Kizitto Noya, Mwanza
  SHULE nne za msingi na sekondari zilizo kwenye Kata ya Nkome wilayani Geita, jana ziliahirisha masomo ili wanafunzi wahudhurie mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete Shule hizo za sekondari za Kabwela na Nyamboge na shule za msingi za Ihumilo na Mwaloni zenye zaidi ya wanafunzi 5000 kwa pamoja zilisitisha masomo na wanafunzi kufurika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ihumilo ambako mkutano huo ulifanyika.

  Habari zilizopatikana uwanjani humo zimeeleza kuwa shule hizo zilisitisha masomo ama kwa wanafunzi kutaka kuhudhuria mkutano huo au walimu kuwalazimisha wafike kumwona mgombea huyo wa CCM.

  Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwenye Shule ya Sekondari ya Nkome, Michael Faustine alisema kuwa jana walisoma kipindi kimoja tu cha kwanza na baadaye walimu waliwataka warudi nyumbani kubadili nguo na kwenda kwenye mkutano huo.

  “Sisi tulisoma kidogo; tulifika na kusoma kipindi cha kwanza na baadaye walimu walitutawanya na kututaka kurudi kwenye mkutano huo,” alisema.

  Bertha Mabingo, mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ihumilo alisema waliambiwa tangu Oktoba 18 mwaka huu kuwa jana kusingekuwa na masomo na badala yake wafike kusikiliza mkutano wa Kikwete.

  “Sisi tulijua mapema kwamba leo (jana) hatutasoma. Walimu walituambia tangu Oktoba 18 kwamba tufike kumwona na kumsikiliza Kikwete,” alisema mwanafunzi huyo.

  Mwanafunzi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Happiness Yohana alisema ujio wa Kikwete ni faraja kwao kwa kuwa wanaamini angezungumzia mambo yanayohusu sekta ya elimu.

  “Sisi tuna matatizo mengi. Vitabu hatuna; walimu wachache; hatuna vyoo na mambo mengine mengi yanayofanana na hayo. Ningefurahi kama rais atazungumzia matatizo hayo,” alisema
  Akizungumza kwenye mkutano huo uliojaa wanawake na watoto, Kikwete alisema amekuja kuomba kura ili aendelee kuwa rais, akamilishe mambo mbalimbali aliyokwishayaanza.

  "Nakuja kuomba mtuchague tena kwa sababu tatu; Kwanza tumeongoza vizuri nchi hii na kwa amani na utulivu. Ingawa nchi bado maskini, lakini ni wazi kwamba kuna mengi CCM imefanya,”

  “Ninaposema tuchagueni ninamaana mimi niwe rais, ninaposema tuchagueni naamaanisha Donald Max kuwa mbunge weu na ninaposema tuchagueni naamanisha madiwani wa CCM.”

  Katika mkutano huo Kikwete alieleza mambo kadhaa anayotarajia kuyasimamia katika kipindi cha uongozi wake ujao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa gati ya Nkome, umeme katika vijiji vyote vinavyoelekea kwenye kata hiyo iliyo kwenye tarafa ya Buganda na ujenzi wa lami katika eneo hilo.

  “Tukimaliza uchaguzi tunaanza kushughulikia suala la kugawanya mipaka. Kata hii ina watu 51,000, idadi ambayo ni nusu ya idadi ya watu kwenye wilaya na zaidi ya mara mbili ya tarafa,” alisema Kikwete.
  “Niliahadi lami tumeweza, tutashindwaje kujenga gati,” alihoji. “Mambo haya yanawezekana kwa serikali ya CCM.”

  Source: Mwananchi
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hawapigi kura hawa!
   
 3. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Cha hatari ni humo nilimo highlight
   
 4. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Wanafunzi wanatangaziwa kuwa masomo hayatakuwepo kwa ajili ka kuhudhuria kampeni za Kikwete?
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hivi TUME YA UCHAGUZI INALIZUNGUMZIAJE HILO kama inaruhusiwa watoto wetu kutolewa madarasani kisa JK anafanya kampeni huko tunakoelekea ni kubaya ama TUME ingesema kuwa kipindi cha kampeni SHULE ZOTE ZIFUNGWE KUPISHA WANAFUNZI NA WALIMU KUHUDHURIA MIKUTANO YA KAMPENI! :A S angry::A S angry::A S angry:
   
 6. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kikwete anafahamu hapendwi,hakubaliki na hatashinda anajikaza kiume tu...
  Ndo maana nguvu zote hizo zinatumika...
  Tunamsihi hakuna ubaya akiwa Rais mstaafu..mbona wako wengi tu..
  Tusisahau kumpa na wabunge wa kutosha Mh.(Dr wa ukweli) W P Slaa..
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Hata watoto wanataka mabdiliko hawataki tena pipi za kikwete.................
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,634
  Likes Received: 4,738
  Trophy Points: 280
  Hataki watoto wa wenzake wasome.
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Kuna tofauti kubwa kati ya watu wanaokula samaki wa maji baridi na maji chumvi/bahari.

  Mwaka huu atapata kura za watu wenye ubongo wa chumvi tu.
   
 10. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  nawashangaa hao waalimu....!
   
 11. whitehorse

  whitehorse JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2010
  Joined: Aug 29, 2009
  Messages: 1,418
  Likes Received: 1,886
  Trophy Points: 280
  wanafunzi wakipigwa picha na bendera za chama, jamaa anapata shavu kuwa anakubalika , maskini watanzania macho na masikio yameshazoea kudanganywapoliics ni technic
   
 12. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  tehe tehe ...wanaona tumesema sana kuhusu kuwabeba watu kwenye malori..sasa wanatumia wanafunzi ili tu ionekane kuna watu wengi kweenye kampeni zake!! POOR MAN!!!:nono:
   
 13. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Exactly ... mtaji wa ccm ni umasikini na ujinga wa watanzania.
   
Loading...