Mkutano wa CHADEMA Kasulu mjini wafanyika, lakini...

ISMAIL MKIMBIZI

Senior Member
Jan 13, 2013
192
23
viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiwamo Shaban Mambo Mwenyekiti wa chadema Kanda ya magharibi na Rajabu Bujoro Mwenyekiti wa Kasulu wamefungua mkutano hali ikiwa shwari watu wa Kasulu wakionesha ustaarabu wa hali ya juu. Lakini kufumba na kufumbua alipopanda jukwaani Dr Slaa Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa kikundi cha watu kiliibuka na mabango mbalimbali huku wakitamka kwa jazba maneno mbalimbali ya kumtaka Zitto na kukejeli upngozi wa juu wa CHADEMA.

Katibu Mkuu ameonesha ustaarabu na demokrasia iliyokomaa alipo ruhusu mabango yasogezwe mbele na kuwataka askari polisi wasiwachukulie hatua wenye mabango. Pia aliwauliza wanakasulu ni wangapi wanataka mkutano uendelee wengi wamenyoosha mikono kutaka mkutano uendelee. Hali si salama sana na nimeacha mpaka naingia mitamboni polisi wanatafuta mbinu mbadala za kuimarisha ulinzi na kuongeza kikosi.

======================
Habari Zaidi
======================


===========================
Kwa Mujibu wa Kurugenzi ya Habari
==========================

 
Niko chumba cha habari nasikia mlio wa mabomu ya machozi bila shaka mkutano umevunjika au........
 
Bado masaa machache tuazimishe miaka 52 ya uhuru(1961-2013)...Je vile vitu vitatu,Siasa Safi,Uongozi Bora,na Watu=Maendeleo,jambo gani linaturudisha nyuma kati ya hayo?
 
Teh teh teh ningefurahi sana kama vijanaa hao wangenyanyua mabango ya kukataa kodi ya simu,kupanda kwa bai ya umeme,elimu duni lakini maskini hawajijui kabisa na hao hao ndio jua linawachoma kila siku na wanayejidai ati wana mtete yeye anakula good time ndani ya gari kubwa Hammer kiyoyozi kikubwa na hao vijana hata kwenye magetho yao hawana hata Feni lol aibu sana kwa Tanzania ama kweli ni vigumu sana kujenga nchi hii chini ya vijana wenye akili mgando kama hawa.Isitoshe Mabango yameandikwa na mtu mmoja yaani nina maana hati ni ya mtu mmoja so hawa wanatumiwa tu kama kondom then kesho hawawatambui tena.Kwa ufupi ni kwamba hata wanyanyue mabango hadi kesho bila kushusha mikono chini Zitto hana chake tena ndani ya Chadema. Yaani ni aibu kijana kupewa ati 5000Tsh sasa hii ni hela nayo jamani??
 

Well, hiyo ndio demokrasia. Lakini MBONA KAMA MABANGO YOTE YAMEANDIKWA NA MTU MMOJA?? Ni vizuri kwa watu kutoa hisia zao lakini haipendezi pale ambapo watu waliobeba mabango wengine wao hata hawajui yameandikwa nini.
 
Ziara za Dr. Slaa huko Kahama na Kigoma ziliwahishwa sana. Wangesubiri mpaka maamuzi ya hatima ya hao walioambiwa wajieleze...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…