Mkutano wa CHADEMA Kasulu mjini wafanyika, lakini...

ISMAIL MKIMBIZI

Senior Member
Jan 13, 2013
192
23
viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiwamo Shaban Mambo Mwenyekiti wa chadema Kanda ya magharibi na Rajabu Bujoro Mwenyekiti wa Kasulu wamefungua mkutano hali ikiwa shwari watu wa Kasulu wakionesha ustaarabu wa hali ya juu. Lakini kufumba na kufumbua alipopanda jukwaani Dr Slaa Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa kikundi cha watu kiliibuka na mabango mbalimbali huku wakitamka kwa jazba maneno mbalimbali ya kumtaka Zitto na kukejeli upngozi wa juu wa CHADEMA.

Katibu Mkuu ameonesha ustaarabu na demokrasia iliyokomaa alipo ruhusu mabango yasogezwe mbele na kuwataka askari polisi wasiwachukulie hatua wenye mabango. Pia aliwauliza wanakasulu ni wangapi wanataka mkutano uendelee wengi wamenyoosha mikono kutaka mkutano uendelee. Hali si salama sana na nimeacha mpaka naingia mitamboni polisi wanatafuta mbinu mbadala za kuimarisha ulinzi na kuongeza kikosi.

======================
Habari Zaidi
======================

Wakuu,taarifa za kusikitisha ni kwamba Mkutano wa Dr.slaa umevunjika Kasulu,amepigwa mawee na vijana wasiojulikana akiwa Jukwaani,Polisi wanapiga mabomu ya Machozi Muda huu kutawanya watu,haijulikani Slaa ameumizwa kiasi gani lakini polisi wamewahi kumuokoa na kumtorosha kusikojulikana.
hali ni tete wakuu,naomba Munipe muda wa kuwawekea Picha hapa.
Pia awali Mkutano ukiwa unaendelea,Waitara ambaye ni Mkurugenzi wa CHADEMA alitangaza kuwa Matamko na mambo mengine yote ya kumtibulia Dr.slaa yanaratibiwa na Kijana Habib Mchange na Diwani mmoja wa Mwanza(Hakutaja jina).

MODS naamini mnawatu KASULU,wapigieni simu MUDA huu,Mpigieni Tumaini Makene mjue Ukweli huu.naomba muiache Post watu wachangie

1456056_1495108347381861_1615035006_n.jpg

Moja ya bango Mkutano wa slaa kasulu kabla haujavunjika

===========================
Kwa Mujibu wa Kurugenzi ya Habari
==========================

Umati wa wananchi waliokusanyika kumsikiliza Katibu Mkuu, Dkt. Slaa leo mjini Kasulu Uwanja wa Kiganamo. Hapa ilikuwa kabla ya vijana wapatao 10-15 hivi kurusha mawe, baada ya wananchi kuwafukuza wakitaka kuwapiga, wakipinga kitendo cha vijana hao kupiga kelele ili mkutano usiendelee.

Mbinu ya kuhakikisha mkutano hauendelei kisha itokee vurugu, ambayo ingefuatiwa na mabomu ya machozi ili kujustify headlines ambazo tayari zimeshaandaliwa kuwa ''Dkt. Slaa aokolewa kwa mabomu...Dkt. Slaa ashindwa kuhutubia, Polisi wamwokoa Dkt. Slaa n.k', ilipangwa kutumika leo baada ya Dkt. Slaa kufanikiwa sana ku-counter issue ya vijana na mabango kwa kuwapatia fursa ya kukaa mbele katika mikutano iliyopita.

Tutawaletea maelezo ya kutosha juu ya mpango huo na mwingine unaoendelea kupangwa kwa ajili ya kufanyika Kigoma mjini na maeneo mengine. Tutajibu maswali na hoja za watu kuhusu tukio la leo.

attachment.php

Niko chumba cha habari nasikia mlio wa mabomu ya machozi bila shaka mkutano umevunjika au........
 
Bado masaa machache tuazimishe miaka 52 ya uhuru(1961-2013)...Je vile vitu vitatu,Siasa Safi,Uongozi Bora,na Watu=Maendeleo,jambo gani linaturudisha nyuma kati ya hayo?
 
Teh teh teh ningefurahi sana kama vijanaa hao wangenyanyua mabango ya kukataa kodi ya simu,kupanda kwa bai ya umeme,elimu duni lakini maskini hawajijui kabisa na hao hao ndio jua linawachoma kila siku na wanayejidai ati wana mtete yeye anakula good time ndani ya gari kubwa Hammer kiyoyozi kikubwa na hao vijana hata kwenye magetho yao hawana hata Feni lol aibu sana kwa Tanzania ama kweli ni vigumu sana kujenga nchi hii chini ya vijana wenye akili mgando kama hawa.Isitoshe Mabango yameandikwa na mtu mmoja yaani nina maana hati ni ya mtu mmoja so hawa wanatumiwa tu kama kondom then kesho hawawatambui tena.Kwa ufupi ni kwamba hata wanyanyue mabango hadi kesho bila kushusha mikono chini Zitto hana chake tena ndani ya Chadema. Yaani ni aibu kijana kupewa ati 5000Tsh sasa hii ni hela nayo jamani??
 
viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiwamo Shaban Mambo Mwenyekiti wa chadema Kanda ya magharibi na Rajabu Bujoro Mwenyekiti wa Kasulu wamefungua mkutano hali ikiwa shwari watu wa Kasulu wakionesha ustaarabu wa hali ya juu. Lakini kufumba na kufumbua alipopanda jukwaani Dr Slaa Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa kikundi cha watu kiliibuka na mabango mbalimbali huku wakitamka kwa jazba maneno mbalimbali ya kumtaka Zitto na kukejeli upngozi wa juu wa CHADEMA.
Katibu Mkuu ameonesha ustaarabu na demokrasia iliyokomaa alipo ruhusu mabango yasogezwe mbele na kuwataka askari polisi wasiwachukulie hatua wenye mabango. Pia aliwauliza wanakasulu ni wangapi wanataka mkutano uendelee wengi wamenyoosha mikono kutaka mkutano uendelee. Hali si salama sana na nimeacha mpaka naingia mitamboni polisi wanatafuta mbinu mbadala za kuimarisha ulinzi na kuongeza kikosi.

Well, hiyo ndio demokrasia. Lakini MBONA KAMA MABANGO YOTE YAMEANDIKWA NA MTU MMOJA?? Ni vizuri kwa watu kutoa hisia zao lakini haipendezi pale ambapo watu waliobeba mabango wengine wao hata hawajui yameandikwa nini.
 
Ziara za Dr. Slaa huko Kahama na Kigoma ziliwahishwa sana. Wangesubiri mpaka maamuzi ya hatima ya hao walioambiwa wajieleze...
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom