Mkutano wa CCM Kizota, Novemba 11-13, 2012

Mkutano wa CCM Kizota, Novemba 11-13, 2012

Kama nilivyoeleza katika thread yangu niliyoitoa wiki mbili zilizopita ni kuwa kuna Mpambano mkali kati ya Mh Bernard Membe (anaewakilisha Kundi la Wapinga ufisadi) na Mh Edward Lowasa(aliye katika kundi la Mafisadi) katika kuwania kuteuliwa kupeperusha bendera ya Chama chetu mwaka 2015. Matokeo ambayo yamejiri hivi karibuni, kwangu mimi naona hadi sasa Scoreboard inaonyesha Lowasa anaongoza 2-1 na sasa ni Half time.

Lowasa ndie aliyetangulia kupata bao baada ya kumsambaratisha vibaya Membe katika chaguzi za NEC wilaya mbalimbali Tanzania. Katika chaguzi hizo, Lowasa alimtimulia vumbi vilivyo bwana Membe kwa kambi yake kushinda kwa ushindi wa kishindo.

Wakati Membe akishangaashangaa, Lowasa alipiga bao la pili fastafasta baada ya Kundi lake lenye nguvu kubwa ya kifedha kutwaa Jumuia zote za chama ie Wazazi, Vijana na Wanawake na kumwacha Membe akin'gaa macho!

Membe, baada ya vipigo hivyo viwili vitakatifu nae alijufutafuta vumbi na kujipatia bao moja ambapo Mwanachama mzoefu na Mwadilifu na anayeuchukia kwa dhati Ufisadi Mh P. Mangula kuchaguliwa kua Makamu Mwenyekiti wa CCM Tz Bara na wajumbe wa NEC. Kwa hakika kitendo cha kuchaguliwa Mangula ni pigo kubwa kwa kundi la Lowasa kwani Mangula ni mtu anayeichukia rushwa kwa dhati na DAIMA haoni aibu kuweka bayana msimamo wake huo. Mwaka 2005 akiwa Katibu Mkuu wa CCM hakusita kusema katika kamati ya maadili ya chama kua JK na kundi lake la akina Rostam hawafai Urais kutokana na matumizi yasio halali ya pesa ! Kutokana na kitendo hicho ccm ilimpotezea kabisa. Alijaribu kugombea Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa na kugoma kabisa kutoa rushwa na matokeo yake akashindwa na mhuni Sanga aka Jah People. Akagombea NEC na kuhutubia sera za CCM wakati wenzake wakigawa rushwa nako akaishia kukosa! Hivyo, kuchaguliwa kwa Mangula ni pigo kubwa kwa kundi la Lowasa.

Hapa Dodoma kwa sasa, mpambano huu utaendelea kwa nafasi ya Mwenyekiti. Lowasa na kundi lake wanaonekana hawataki J. Kikwete aendelee kua Mwenyekiti kwani wanaona nae ni mmoja kati ya walioshiriki kuharibu nyota ya Lowasa!. Hotuba aliyoitoa Lowasa mwezi Novemba 2011 NEC-Dodoma ambapo alimwaga mboga na ugali kwa pamoja na kumpelekea mwenyekiti mashambulizi makali ambayo Mwenyekiti alishindwa kabisa kuyajibu yanaonyeshafika kambi hiyo isivyo na imani na Mwenyekiti. Aidha,Kitendo cha Bashe, Freddy na Malisa kutapanya mabango mji mzima wa Dodoma kumkataa JK kuendelea kua Mwenyekiti inaonyesha azma hii ya kumkataa Mwenyekiti ambaye upande wa Lowasa unajua fika yuko upande wa Membe. Hivyo JK akichaguliwa tena kuwa mwenyekiti Lowasa atakua kapigwa bao la pili.

Na jambo kubwa na la mwisho linalosubiriwa kwa hamu KUBWA ni kuona kama Membe atafanikiwa kuwemo katika TOP TEN YA NEC. Kundi la Lowasa limetumia "yale mambo yetu" kuwashawishi wajumbe wa NEC kumsabaratisha Membe. Kundi hilo la Lowasa linaamini hiyo ni kazi nyepesi kama kumsukuma mlevi kwani watakaofanya uchaguzi huo wa NEC ni wajumbe wa NEC ambao 90% ndio waliochaguliwa majuzi na wako kundi la Lowasa. Bashe alitamka wazi kwenye press conference kwamba wanafanya kila njia Membe asipite. Katika kuhakikisha wanafanikiwa wameishatayarisha majina KUMI ya watu ambao wanafaa kuingia kumi bora ambapo jina la Membe halimo na wamekua wakiipitisha orodha hiyo kwa wajumbe mbalimbali wa NEC ili Membe atoswe.

Iwapo watafanikiwa hilo, basi huo ndo utakua MWISHO wa hekaheka za Membe kuelekea Ikulu kama vile Sumaye nae alivyoangukia pua na kuishia kulalama tu! Hoja hapa ni kwamba, kwakua chama makini Chadema kinaendelea kuitimulia vumbi CCM kila kukicha hivyo kumpitisha mtu ambaye hata kwenye NEC ya chama chake tu hakubaliki, Watanzania watamkubalije?Kwa upande mwingine, iwapo Membe atashinda litakua ni pigo KUBWA kwa kundi la Lowasa kwa hoja kwamba 90% ya NEC ni wafuasi wa Lowasa, sasa wamewezaje kumchagua Membe?

Yangu macho, hii imekaaje wadau?

Kwa analysis hii maana yake ni kwamba sasa Lowassa katunguliwa maana pamoja na kampeni hizo hasi dhidi ya JK amechaguliwa kwa kura za kishindo na Membe huyooooo kajipetea bila kampeni za kuzunguka mikoani au kutoa hata shilingi. Lowassa na vikaragosi vyake ambavyo vingine hata uraia wake ni wa kughushi wamebaki wamebung'aa tu. Waliapa kumuadabisha sasa wameadabishwa wao. Utamu wa filamu hii ni pale walipochezewa offside trick baada ya kuamuliwa kwamba uchaguzi ufanyike jana badala ya leo maana Lowassa alikuwa kaandaa dinner ambayo ingekusanya idadi kubwa ya wajumbe wa Mkutano Mkuu ili kugawa mbumba na kusisitiza msimamo wa kumpa kura za hapana JK na kumuadabisha Membe. Zile fedha zilizokusanywa toka arusha na dar ziliingia jana lakini hazikufua dafu. Desperately, wakawa wanapiga kampeni ukumbini muda mfupi kabla ya uchaguzi na kusisitiza "msichague jina namba 14 - ambalo ni la Membe lakini wapi!

Udhibiti huu ukiendelea mpaka kwenye kuhesabu kura walikotegemea wangejaribu kuvuruga lakini wapi. Mahotelini, kwenye mabaa na maeneo ya CCM makao makuu na eneo la ukumbi wa mkutano askari kanzu na wenye nchi walitanda huku Takukuru wakiwa wametoa hotlines zao. Hakika jamaa walikuwa suffocated na ushindi wa Membe umedhihirisha kwamba uchaguzi bila rushwa unawezekana na mikakati ya kisayansi ndiyo inayoshinda uchaguzi.
 
Kuna dalili kubwa sana January Makamba akapata kura nyingi sana katika nafaai kumi za bara kupita wagombea wengine na huenda Membe akapata kura kama za JK mwaka 2002 ambako alikua wa 12 kati ya wagombea 20.... lakini siasa za wakati ule na za sasa ni tofauti sana

tunakumbuka hii.?
 
tunakumbuka hii.?

Nilikuwa natafuta hi comments nashukuru umeiweka hii nyota njema sana kwa JM mbele ya safari pia tusishangae Mzee Wassira akachukuwa form za kugombea urais kunathead nilishaiweka hapa nimeitafuta sijaiona lakini kunamember ameweka thead hiyo.
 
Live toka Dodoma.

Rais Jakaya kajiuzulu saa sita na dakika 35 kwa muda ili kuepusha uchaguzi wa nani akalie kiti hicho cha Chama taifa.
 
Naomba kutoa hoja,mleta mada ale ban mara moja iwe fundisho kwa watu wote wenye kuleta mada za uongo!
 
hata kujiuzulu bado, wanapiga picha wakimaliza ndo wale viongozi watatu wajuu akiwemo huyo jk watajiuzulu kupisha uchaguzi
 
72166_479549425423429_671526178_n.jpg
 
Ni utaratibu mzuri, ila walau ingekuwa kwa masaa mengi ili kutoa nafasi kwa wanaotaka nafasi hiyo kufanya kampeni alafu usiku waanze uchaguzi. Katiba mpya ianayotarajiwa iweke na muda wa rais kujiuzuru kupisha kampeni za urais kama naye ni mshiriki mmoja wapo.
 
Back
Top Bottom