Mkururugenzi wa Manispaa Zanzibar amwagiwa tindikali.................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkururugenzi wa Manispaa Zanzibar amwagiwa tindikali....................

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by meddie, Feb 18, 2011.

 1. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Siku za hivi karibuni hapa ZNZ kumekuwa na movement ya kuhamisha kwa nguvu wafanyabiashara kutoka ktk maeneo yanayodaiwa hayaruhusiwi kufanyia biashara . Moja ya maeneo mojawapo ni eneo maarufu kwa hapa zenji la Darajani.
  Hapa kumekuwepo na upinzani mkali na kwa zaidi ya wiki sasa askali wa jiji wanakuwepo masaa 24 kuzuia wafanyabiashara waliokwisha tolewa wasirudi. Wafanyabiashara wamekimbilia kufungua kesi mahakamani kupinga kuhamishwa eneo hili ni hii imejili baada ya kukosa msaada toka kwa watetezi wao waliowategemea ambao sasa ni sehemu ya serikali! Ktk kile kinachoonekana frustration za kukosa msaada mkurugenzi wa manispaa jana usiku amemwagiwa majimaji yanayosadikika kuwa ni tindikali na hivi leo amekimbizwa muhimbili kwa matibabu.

  Swali: Je njia kama hizi zinaweza kutumika kwa hapa bara kudhibitu watu kama rostam, menji n.k badara tu ya kukaa tunasema maneno mengi na kutukana? ....watu tayari wameshateka serikali, mahakama na hata bunge letu!
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Akiwa nje ya msikiti na huku akiongea na wenzie Mkurugenzi wa manispaa wa Zanzibar alijikuta akimwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana aliyekuwa amevalia mavazi meusi katika khali inayohusishwa na bomoa bomoa ya vibanda vya biashara madarajani............SOURCE: ZANZIBAR LEO.

  kwa wale wapiga baragumu la kuwa serikali ya mseto imeleta shwari Zanzibar wajue wanajidanganya wenyewe...................mlo wa viongozi kamwe hauwezi kuwafikia raia wa kawaida na hivi sasa raia hao hawana hata msemaji wao wa kuwatetea Bungeni baada ya CUF na CCM kurudisha mfumo wa chama kimoja Bungeni kinyemela na hivyo kuwasaliti wapigakura wote wa Zanzibar na mfumo mzima wa vyama vingi vya ushindani wa kisiasa......................JUDAS ISKARIOT must be smiling in his grave......................
   
 3. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hayo ya kuua upinzani waliyataka wenyewe, mtakuaje wapinzani nanyi mmekua kitu kimoja, sasa viongozi wameshapata madaraka hawawakumbuki hao wachini, wamekua bendera kufuata upepo, nani atakosoa utendaji mbovu?
  Pole kwa huyo bwana aliemwagiwa tindikali, tunamuomba Mungu amuafu.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Wameanza kugeukana sasa!
   
 5. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Shida ya wanaharakati wetu ni matumbo, wakishagawana ufalme wanasahau kabisa walichopigania mwanzo. Shame on them...
   
 6. D

  Danniair JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Darajani ni eneo maarufu sana East & Central Africa. bila kuwaelimisha na wao kuridhika kwa nini watoke hapo ni kujitafutia hizo esidi. Eneo kama hilo kama unataka kuliboresha kwa ajili ya machinga boresha kwa awamu huku nao wakiendelea kufanya biashara. Ukimaliza awamu hiyo wagawie ingia awamu inayofata. Mbona barabara hujengwa huku magari yakipita. Lakini yakifanywa kama Ya Lindi stiriti Mh!. Zanzibar I support YOU. Hapo ndipo mnapohudumia familia zenu na ni kwenu!
   
 7. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Jamaa wameamua short cut maana ni kweli hakuna wa kuwasadia,vibanda vimevyunjwa na wamepoteza mali zao hivyo imewachanganya sana na kufikia huo uamuzi ni hatari sana mpaka wananchi kufikia hatua hii.
   
Loading...