Mkurugenzi wanyamapori ang'olewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi wanyamapori ang'olewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Mar 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi wanyamapori ang'olewa

  Imeandikwa na Hellen Mlacky; Tarehe: 4th March 2011


  WIZARA ya Maliasili na Utalii, imefanya mabadiliko kwa kumuondoa katika wadhifa wake, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Erasmus Tarimo.

  Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka katika Wizara hiyo, nafasi ya Tarimo aliyeishikilia tangu Desemba 2007, imechukuliwa na Obeid Mbangwa aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi ya Wanyamapori.


  Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alipoulizwa kuhusu mabadiliko hayo, alielekeza aulizwe Katibu Mkuu, lakini anayekaimu nafasi hiyo kwa sasa, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale hakupatikana kuzungumzia hilo. Huenda taarifa rasmi ya mabadiliko hayo ikatolewa leo.


  Kuondolewa kwa Tarimo katika Idara ya Wanyamapori kumekuja siku nne tangu Rais Jakaya Kikwete abadilishe makatibu wakuu ambapo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Ladislaus Komba, amepelekwa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambako kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, atapangiwa kazi maalumu.


  Katibu Mkuu mpya ni Maimuna Tarishi. Wakati huo huo, Serikali imeanza makubaliano na India kwa lengo la kuweka kichocheo kwa watalii kutoka nchini humo kuwekeza katika utalii nchini kwa lengo la kukuza pato la taifa kupitia utalii hususan kwa kufungua mawasiliano ya ndege katika nchi hizo.


  Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutokana na ziara waliyoifanya India kwa lengo la kuhimiza utalii.


  Alisema katika ziara hiyo alizungumza na wamiliki wa shirika kubwa la ndege la India la ‘Jet Airways' ambalo lilikubali kuanzisha mchakato wa kuomba kibali cha kutua Dar es Salaam na katika kufanikisha azma hiyo, ameiagiza Bodi ya Utalii kufuatilia suala hilo ili shirika hilo lipate kibali.


  Aidha, alisema alihimiza utalii wa mikutano ambapo alizungumza na wakala wa Kampuni ya Sun Pharmaceutical Ltd ambayo ina watumishi 12,000 duniani kote kufanya mkutano na watumishi wake nchini Tanzania mwaka huu ambapo aliridhia katika juma la tatu la Julai.


  Alisema kampuni hiyo huwa inawapa watumishi wake motisha kwa kuwasafirisha kwenda nje ya India kwa ajili ya utalii na kufanya mkutano na kupongezana na watakaokuja ni 1,000 hivyo kutokana na maridhiano hayo, kamati maalumu itaundwa chini ya TTB ili kufanikisha maandalizi ya ujio huo.

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  Tanzania to promote tourism through its embassies


  By JAFFAR MJASIRI, 4th March 2011 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 106

  TANZANIA has finalized arrangements to reinstate tourism desks in its embassies around the world.

  Speaking to journalists on Friday in Dar es Salaam after opening the first Tanzania Tourist Board's stakeholders meeting to deliberate on the new proposed brand destination, the Minister for Natural Resources and Tourism, Mr Ezekiel Maige said that his ministry has already secured some funds to support the desk officers in the embassies abroad.


  "Any marketing needs strong brand, which after detailed research the experts have come up with the proposed brand: Tanzania Feel Great with Friends which is going to be discussed. However, in the past the country did not have a brand but slogans, such as the land of Kilimanjaro, Zanzibar and Serengeti," he noted.


  He observed that the meeting will enable experts in tourism and stakeholders attending a one-day meeting, to share ideas and give their views on whether to adapt the new brand or not.


  Mr Maige also said that the meeting will advise other areas that need improvement in order to strengthen the country's marketing strategies in promoting tourism around the world.


  "The process of having a brand in place will take a year, as it had taken time for the strategy to take off," he said.


  "This is an opportunity for the informal and formal sector in tourism to network and learn various issues which will help in increasing the frequency of promotion of tourism in the country and other tourism development opportunities," he said.


  Speaking on the outcome of the seminar which was organized for Tanzanian ambassadors to Asia recently in the country, the minister said that there were strategies drawn on the importance of promoting tourism in Asia.


  "The ambassadors have been given objectives and goals to accomplish in their respective areas in terms of promoting tourism and its attractions," he stated.


  Mr Maige said that the ministry will continue to organize similar seminars for other envoys stationed in other parts of the world.


  According to him, in order to expand tourism activities in the country, the government has continued to put more effort and concentrate on tourist circuits that have infrastructures in place, such as Arusha, Morogoro and Mwanza.


  "We continue to focus on Southern Highlands where soon the Songwe International Airport which is in its finals touches, will soon start operating," he said.


  Other attractions are in Tanga where the caves at Amboni heritage site can be easily accessible due to good roads, he noted.


  When asked to comment on the opportunities emerging following political crisis in Egypt which used to be a famous tourist destination, he said that Tanzania can take advantage of the situation to promote its brand.


  He cautioned that any negative information in regards to the stability of the country circulated around the world will discourage tourists to visit the country.


  "It can at times lead to investors pulling out their investment, which will have adverse effect to the country's image and economy," he said.


  The minister also hailed the co-operation that exists between the ministry and other stakeholders in a bid to promote tourism in the country.


  Speaking to this paper, the Treasurer of Tourism Confederation of Tanzania, Ms Zamzam Mtanda noted that there was every indication that the government was committed to promote tourism in the country.


  She praised efforts by the government to promote public-private-partnership in the country, saying that it was going to lay down a roadmap to create a win-win situation between the two, especially on issues of levies and taxes.


  In his remarks on the importance of the stakeholders meeting, the Chairman of Kibo Travel Bureau, Mr Aloyce Kimaro said that it was important to meet today (yesterday) to define strategies in streamlining the tourist activities in the country.


  "Through such deliberations it will enable the Tourism stakeholders to join hands in drawing strategies that will help to improve services to satisfy the tourists by rendering quality services," he added.


  On her part, TTB Senior Public Relations Officer Ms Mdachi said that the ministry had continued to collaborate with the Board by helping them to woo tourists through various exhibitions that take place in foreign countries.


  "We continue sending flyers and other brochures to the embassies so that they can distribute them to those coming to the embassy seeking information about Tanzania," she noted.


  Also the embassies using their websites have also been instrumental in promoting tourism attractions in the country, added Ms Mdachi.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  Magazeti wmawili yamerekodi habari ileile vinginevyo......................................Daily News halijui ya kuwa kibosile wa wanyapori is out....................
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  JK ateua bodi mpya TANAPA


  na Mariana Mathias


  [​IMG] RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ameteua bodi mpya ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kutengua madaraka ya Mkurugenzi wa Wanyamapori jana jijini Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ladislaus Komba, ilisema Modestus Lilungulu ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Februari 7, mwaka huu.
  Aidha, kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekieli Maige, aliwateua wajumbe wa bodi hiyo kuwa ni IGP Saidi Ali Mwema, Marcellina Chijoringa, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Jenista J. Mhagama (Mb), Michael Lekule Laizer (Mb), Ruth Mollel, Hajjat Riziki Lulida, Winfrida Nshangeki, George Fumbuka, Nyambari Nyangwene, Mtendaji Mkuu wa TANAPA-Katibu, na uteuzi huu umeanza mara moja.
  Wakati huo huo rais ametengua madaraka ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori, Erasmus Tarimo, kuanzia Februari 11 mwaka huu na kumpatia likizo akisubiri kustaafu.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Donatius Kamamba, ilisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi ya Wanyamapori, Obeid Mbangwa, kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mujibu wa kifungu 8(1) cha sheria ya utumishi wa umma namba 8 ya mwaka 2002.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa George Fumbuka,kawekwa hapo kwa misingi ya ukabila tu.................................kampuni yake ya uwakala pale Stock exchange ina kesi za kuwaibia wateja sasa kaingiaje huku na anatuhuma za kukosa uaminifu ambazo ni za muda mrefu.............................jingine idadi ya wabunge wengi ndani ya Bodi kunaashiria nini wakati Bunge hilo hilo linadai kazi yake ni kuidhibiti serikali katika kazi zake..........................sasa kama bunge limo ndani ya jiko la serikali ni nani atamvika paka kengele????????????????????
   
 6. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Unashangaa nini, haka kanaimarishwa zaidi kuwa sab-folder ya ufisadi. Maana Kametema mwaka huu kuliko sekta ya madini.
   
Loading...