Mkurugenzi wa Uendeshaji ACACIA aeleza sababu za kitaalamu kwanini wanasafirisha mchanga wa dhahabu

Duuu,,, kweli uongozi ni kipaji, kama huna huna tu. Hata uwe professor. Kwani magu angetaka hizi informations kwa nafasi yake angezikosa! Au ndio kusaka kiki?
 
Tatizo huyo anaenda ofisi kusoma magazeti hajui kuwa kuna watu wanaenda ofisini na wanalipwa kutokana ka kazi wanayofanya.

Kuna consultant mmoja kwenye kampuni fulani alikuwa analipwa 2000$ kwa siku...ilibidi afanyishwe kazi harakaharaka ili aondoke.

Kuna mtu hata diary hajui ni nini. Ukimuuliza leo unafanya nini hajui wakati wengine appointment ya miezi sita mbele huwezi kupata maana imejaa.

Wanafkiri watu wengine wanalipwa kwa kuamka na kujiamulia leo ngoja niende bandarini bila ratiba yoyote ile.
 
Mimi ninachotaka kufahamu ni kuwa kumiliki na kusafirisha mchanga huo wa dhahabu ni sehemu ya mkataba?
 
TMMA ndio mdudu gani?
KULIKUWA NA WAPIGADILI WENGI TANZANIA KWAIYO HATUWEZI KUWAAMINI HAO TEMMA. SISI HATUONI HASALA YA KUZUIA HUO MCHANGA MAANA HATUJAWAI FAIDIKA KWAIYO HATA UKIKAA MIAKA 10 MPAKA TUPATE SMELTER NISAWA TU. SASA KAMA WAO WATAKULA HASALA KWA MCHANGA KUZUIWA WALETE HIZO SMELTER MAANA MAKAMPUNI MAWILI HAYA WEZI SHINDWA KUWEKEZA KWA HILO. LAKINI MCHANGA HAUTOKI HATA PUNJE. GODBLESS MAGUFULI
 
KULIKUWA NA WAPIGADILI WENGI TANZANIA KWAIYO HATUWEZI KUWAAMINI HAO TEMMA. SISI HATUONI HASALA YA KUZUIA HUO MCHANGA MAANA HATUJAWAI FAIDIKA KWAIYO HATA UKIKAA MIAKA 10 MPAKA TUPATE SMELTER NISAWA TU. SASA KAMA WAO WATAKULA HASALA KWA MCHANGA KUZUIWA WALETE HIZO SMELTER MAANA MAKAMPUNI MAWILI HAYA WEZI SHINDWA KUWEKEZA KWA HILO. LAKINI MCHANGA HAUTOKI HATA PUNJE. GODBLESS MAGUFULI
mkuu mbona uko hivyo?kuna mikataba ilishasainiwa kusafirisha huu mchanga wa shaba(makinikia ya shaba)
 
Nakubaliana na wewe 100% ndo maana karibu Mkuu aliyetumbuliwa alipendekeza hvo ila yule muandisi wa bandari akakomaa kuwa 90% ya kilichopo kwenye makontainer ni dhahabu...nilishangaa sana kusikia vile.

Ila alijichanganya kwani alisema tena 90% ni Madini....sasa ni Madini gani hakuelezea...kusema tu 90% ni Madini ni too general..inabidi uchukue sampuni ukapime hyo 90% yako ni ya Madini gani.

Katibu mkuu mtumbuliwa alikuwa sahihi Kabisa kusema iunde team ya wataalamu watakochunguza kuna nn hasa kwenye zile container...siju kwa nn alitumbuliwa tu...sijui.
Tuwe makini ili tunaposoma habari tuielewe! Ukitanguliza ushabiki na hisia mbele basi utaelewa kile ubongo wako unachotaka na si kile kilichandikwa. Ndugu, kwa taarifa yako huyo mkuu wa bandari alisema ''ana uhakika kwa asilimia 90 kile kilichopo ndani ni...
HAKUSEMA ndani ya kontena kuna dhahabu 90%!
 
Nimemwelewa vizuri aliyendika hapo hiyo habari ndefu. Ametuandaa pia kisaikolojia kwa kusema kampuni inapata hasara ya shs billion 1 kila siku kwa kuzuia kusafirisha mchanga. Sisi wengine tunajua nini kinafuata baada ya hapo.
Kiukweli, siwezi kuwalaumu wawekezaji. Kwani tulikuwa tumerogwa wakati tunasaini mikataba??? kwani hakuna watu waliotupa tahadhari kuhusu mikataba hiyo? Nia ni nzuri, lkn chochote tunachofanya sasa ni lazima tuumie. Ni sawa na ile issue ya makampuni ya kuzalisha umeme kuiuzia TANESCO umeme kwa shs 500 + kwa unit moja, kisha Tanesco nayo inawauzia wananchi kwa bei ya hasara!! Tunapenda kujitafutia matatizo sisi wenyewe.
 
Hakuna sababu ya muhimu hapo acacia kushindwa kujenga smelting Tanzania, kama tunapata tani 25-30,000 za Shaba basi ni wakati muafaka wa kujenga smelting Tanzania, pia hizo data ni za mwaka gani kuwa chile wana produce zaidi ya tone850,000 za copper kwa mwaka?
List of countries by copper production
Rank
Country/region 2014 copper production (thousand tonnes)
1 Chile 5,750
2 China 1,760
3 Peru 1,380
4 United States 1,360
Kama chile wanaproduce 5750 tones kwa mwaka wana smelting, iweje kwa Tanzania ambapo kwa mujibu wa mleta mada tuna produce 25,000-30,000 tones /yr?.
Google
 
Ndugu yangu asante kwa ufafanuzi. Watu tunamitizamo tofauti na kuna kundi moja la watu kazi yao nikupinga kwa kejeli hata kama lina mashiko kwa umma. Wapuuzie mbali watu hao. Sasa naomba nikuulize: Endapo serikali yetu itashikilia msimamo wake wakuzuia usafirishaji wa mchanga nje ya nchi vp kuhusu hasara itakayopatikana kwa kampuni ya uchimbaji nani atawajibika? Na je mikataba ilikuwa inasemaje?
 
Tuwe makini ili tunaposoma habari tuielewe! Ukitanguliza ushabiki na hisia mbele basi utaelewa kile ubongo wako unachotaka na si kile kilichandikwa. Ndugu, kwa taarifa yako huyo mkuu wa bandari alisema ''ana uhakika kwa asilimia 90 kile kilichopo ndani ni...
HAKUSEMA ndani ya kontena kuna dhahabu 90%!

Mkuu wangu mm huwa sikurupuki rudi ukasome Uzi wa BAK kwa makini. Ukisoma kwa makini nadhani ili povu ulilotoa hapa litapungu kama sio kuisha Kabisa

Ila anza na hiki nilichocopy huko.

Aliyekuwa Katibu Mkuu huyo alitoa ushauri ambao ulionekana kupingana na maelezo ya Mhandisi Kakoko ambaye alidai ana uhakika wa asilimia 90 kuwa kilichomo kwenye kontena hizo ni madini na siyo mchanga.

Prof. Ntalikwa, kwa upande wake, alishauri kuunda timu ya wataalamu kutoka sekta mbalimbali kuchunguza suala hilo.

Alishauri kuchukuliwa kwa sampuli na kuzipeleka maabara na kujua ukweli.

“Mheshimiwa Spika, napendekeza tutengeneze timu ya wataalamu kuchukua sampuli na kuzipeleka maabara kupima," alisema Prof. Ntalikwa. "Timu hiyo inaweza kujumuisha taasisi nyingine, alafu taarifa iwekwe wazi kwa umma.”

Ushauri huo haukumfurahisha Kakoko ambaye moja kwa moja alisema anaandaa barua kwa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Wizara waeleze kwa kina juu ya suala hilo na kwamba linahitaji kujipanga sana ili kuliendea.

“Katibu Mkuu wewe labda ni mgeni, hayamasuala huyajui vizuri," alisema Kakoko.

"Vipimo vinafanyika lakini humu kuna jambo la ziada, hatuwezi kuliendea hili jambo kwa‘theory’ (nadharia) bali ‘practical’ (vitendo) zaidi.


"Twende hadi kwenye migodi tuone wanavyochukua sampuli, zinavyopimwa na kule unapopelekwa China, Ujerumani na kwingine tujue matokeo ya vipimo vyao, vinginevyo hatutafanikiwa.”

Alisema kwa sasa kila kontena linaloingia bandarini humo lazima lipite kwenye mashine maalum kujua kilichomo, na kwambawameongeza mashine sita za 'scan' ili kuongeza ufanisi zaidi.

Baada ya ziara hiyo, Ndugai na wabunge hao walitoa majumuisho na kueleza kuwa Bunge litaunda kamati ya kuchunguza mikataba, sheria na mchakato zima wa sekta ya madini, ikiwamo kujua kilichomo kwenye makontena 256.

Ripoti ya kamati hiyo, alisema Ndugai, itaishauri serikali kama iendelee na biashara ya kusafirisha 'mchanga' huo au la.

Alipoulizwa na Nipashe, mbele ya Spika, wakati wa chakula cha mchana ana uthibitisho gani kuwa ndani ya makontena kuna madini na si 'mchanga', Mhandisi Kakoko alisema “Sisi ni watendaji wa serikali.

"Tumeshafanya uchunguzi wetu na kubaini kuwa ndani ya makontena yale kuna madini ya dhahabu kwa asilimia 90.”
Ziara ya Spika na wabunge imetokana na matokeo ya ziara ya kushtukiza bandarini hapo ya Rais Magufuli ambapo alionyeshwa makontena 20 ya kampuni ya Acacia ya 'mchanga' wa dhahabu, yakisubiri kusafirishwa nje ya nchi kinyume na maelekezo ya yake Machi 2.
 
huo ndio ukweli wao, sisi tusitoe povu tuupinge kwa facts and findings.
Vinginevyo dunia itatushangaa. Ndio maana JPM inabidi atupe facts au ukweli wetu pia maana kuishia kusema tunaibiwa tu haitoshi .
ndio maana tutapongeza kama wananchi tukipata taarifa iliyokamilika inayokanusha maelezo au ukweli wa hawa wazungu..
 
ok ngoja nikwambie,, hata kama mimi ni mnufaika ila ukweli ngoja nikusaidie,, Ban anazozipiga rais wako zina faida gan kwa nchi? mfano sukari si alipiga Ban? mwisho wa siku nini kilitokea? je unadhani sukari sasa haiingii nchini? hata kama sisi ni wanufaika ila hapa rais wako anachemka
Ni kweli Rais ametuingiza ktk wakati mgumu kuwahi kutokea Leo hii familia Masikini hawanywi chai Kibaha sukari 1kg=2800, Unga wa mahindi ni 2200 1kg
Haya yote ni maamuzi mabovu yanayo fanywa na Rais katika nyanja za kiuchumi, na kuwasababishia Raia kuishi katika mateso
 
Back
Top Bottom