Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayub Rioba apata ajali Kigoma

Huko ndani TBC wafanyikazi wengi wamefurahi , wengi walitamani apendwe zaidi:

Wanakwambia huyu jamaa ni mdini sana, Kila kitengo kaweka head of department wa Dini yake.Hata kama mtu hana elimu husika kamuweka huko.

Ukija vitengo vya manunuzi, HR na Mbaya zaidi Kitengo cha MAFUNDI MITAMBO ,
Kama wewe si wa Dini yake utaishia kukaa ofisini, ila kama upo naye utaenda ziara zote, Za Raisi na pia kutangaza mipira,

Huko TBC wacheni kabisa, jamaa hatoi hata mafuta ya Gari, mafundi wanapanda Bodaboda na juzi tu fundi wetu wa TBC -Tazara kapata ajali na bodaboda pale ubungo akiwahi gari La Iringa , yu hoi mpaka leo.

JPM haoni hili,huyu jamaa kwakuwa katoka kanda ile anafanya atakavyo.
 
TBC wazitangaze barabara za KGM kama janga la taifa! Kila serikali inazipotezea na zinaendelea kukaanga watu!
 
Huko ndani TBC wafanyikazi wengi wamefurahi , wengi walitamani apendwe zaidi:

Wanakwambia huyu jamaa ni mdini sana, Kila kitengo kaweka head of department wa Dini yake.Hata kama mtu hana elimu husika kamuweka huko.

Ukija vitengo vya manunuzi, HR na Mbaya zaidi Kitengo cha MAFUNDI MITAMBO ,
Kama wewe si wa Dini yake utaishia kukaa ofisini, ila kama upo naye utaenda ziara zote, Za Raisi na pia kutangaza mipira,

Huko TBC wacheni kabisa, jamaa hatoi hata mafuta ya Gari, mafundi wanapanda Bodaboda na juzi tu fundi wetu wa TBC -Tazara kapata ajali na bodaboda pale ubungo akiwahi gari La Iringa , yu hoi mpaka leo.

JPM haoni hili,huyu jamaa kwakuwa katoka kanda ile anafanya atakavyo.
Duh,inaonekana karma saivi ina moto nchi hii,,,from tundu lissu to ndugai ,,,,from huyo jamaa to boss wake
 
tairi imejaa tope... shida ni mwendo wa kasi... poleni wahanga
 
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Dkt. Ayub Rioba amepata ajali ya gari huko Mgombe, Kigoma.

Taarifa za awali zinadai kuwa watu wawili wanahofiwa kufariki, huku yeye mwenyewe akipata majeraha kidogo.

Taarifa zaidi zitafuata..

=====

Watu wawili wamefariki Dunia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufuatia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba, lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.

Kamanda Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambae hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Amesmea Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

Kamanda Otieno aliongeza kuwa kutoa tahadhari kufuatia Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo,hivyo amewaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.

Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.
View attachment 720663 View attachment 720701 View attachment 720702
Mungu ailaze mahali pema roho ya Marehemu.
 
Back
Top Bottom