Mkurugenzi wa Mount Meru Hotel Arusha amwaga chozi Mahakamani

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mlalamikaji katika kesi ya wizi wa sh,milioni 300 namba 87 ya mwaka 2020, Emmanuel Wadoo maarufu kwa jina la Sunda ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa Madini na mmiliki wa hotel ya kitalii ya Mount Meru jijini Arusha ,amejikuta akiangua kilio mahakamani katika kesi hiyo ambayo anamtuhumu mfanyakazi wake wa ndani (houseboy)kumwibia mamilioni ya fedha hizo.

Wadoo ambaye ni shahidi namba moja katika Shauri hilo,alilazimika kuangua kilio huku akitokwa na jasho jingi na akiagiza maji ya chupa Mara kwa Mara mahakamani hapo wakati akihojiwa na wakili wa upande wa utetezi, Edmund Ngemela baada ya kubanwa kuhusu madai yake ya kwamba nyumba yake haina uzio, haijafungwa cctv camera na hana mlinzi Wala wafanyakazi wa ndani na alikuwa akiishi yeye na mke wake tu wakati tukio hilo likitokea

Hata hivyo shahidi wa pili , Jeremiah Mchome,alitofautiana na mlalamikaji huyo baada ya kuieleza mahakama kwamba nyumba ya mfanyabiashara huyo imefungwa camera na ana wafanyakazi watatu wa kike ,uzio na mlinzi na kwamba hakumwona mtuhumiwa akiiba kiasi hicho Cha fedha bali aliambiwa na mlalamikaji.

Shauri hilo linalosikilizwa na hakimu Pamela Meela wa Makahama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Arumeru ,Wadoo anamlalamikia ,Joel Keya ambaye alikuwa Mtunza bustani nyumbani kwake eneo la PPF Njiro, jijini Arusha .

Wado aliiambia mahakama hiyo jana kwamba Joel Keya akiwa mfanyakazi wake,Kati ya April na June mwaka 2018 alimwibia Madini ya Tanzanite yenye thamani ya sh,milioni 60,dola 7000 za kimarekani ,fedha tasilimu sh,milioni 200 ,sh,milioni 6 na simu aina ya iPhone vyote vikiwa na thamani ya sh,milioni 300 .

Wakili Ngemela alimhoji mlalamikaji kwanini hakutoa taarifa kituo Cha polisi tangu mwaka 2018 wizi ulipotokea hadi mwaka 2020 alipoamua kutoa taarifa polisi ,Wado alieleza kwamba alikuwa akifanya uchunguzi na baadaye alielezwa na mke wake kwamba Joel ndiye amekuwa akimwibia kwani siku moja alirudi nyumbani na alipoingia ndani alikuta kabati la fedha limevunjwa na alipotoka nje alimwona Joel akiondoka na pikipiki. .

Naye shahidi wa tatu, Jackson Marunda(39) Mkazi wa Olorien ambaye ni mwosha magari kwa mlalamikaji alisema mnamo desemba 19 ,2019 akifanya kazi ya kuosha gari ya mlalamikaji alimwona Joel Keya akitoka ndani kupitia dirisha la choo Katika nyumba ya mlalamikaji.

Huku akiongozwa na wakili wa serikali Grace Mesikenya alisema kuwa taarifa za wizi alizisikia kituo Cha polisi baada ya kuitwa na kumkuta mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi .

Shahidi alieleza kwamba desemba 27 mwaka 2019 alifika nyumbani kwa mlalamikaji kwa ajili ya shughuli za kuosha magari lakini mlinzi wa eneo hilo alimwambia asiingie ndani kwani Kuna wizi umetokea.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 20 ,mwaka huu itakapoendelea kwa upande wa mashtaka kutoa ushahidi.


Ends...
 
Sunda, hili jina kuna wakati lilitamba sana miaka kadhaa nyuma hapa Arusha.

Ila kuhusu hiyo kesi kama huyo Dogo kapiga huo mpunga mbona itakuwa kazi kumshinda maana atatumia vizuri hiyo pesa.
 
Shahidi no 3 kanichanganya kwamba alimuona mtuhumiwa anatoka kupitia dirisha la choo muda huo huo mlinzi akamwambia usiingie ndan kuna wiz umetokea mbona wanajichanganya wenyew
 
Shahidi no 3 kanichanganya kwamba alimuona mtuhumiwa anatoka kupitia dirisha la choo muda huo huo mlinzi akamwambia usiingie ndan kuna wiz umetokea mbona wanajichanganya wenyew
Na mm hapo ndio nimeduwaa huyu Shahid Kama vile kapangwa na hakuandaliwa vzuri
 
Back
Top Bottom