A
Anonymous
Guest
Ndugu Watanzania, nimepokea malalamiko ya Waalimu kwamba Mkurugenzi wa Mbinga DC anawanyanyasa sana Walimu wa Mbinga DC.
Kwa mfano, Mkurugenzi huyo huwaita walimu wote kufika ofisini kwake bila kuzingatia utaratibu rasmi wa kiutumishi!
Mfano mzuri ni Ijumaa ya Tarehe 27/02/2026 aliwaita walimu wote wa Mbinga DC bila kuwapa nauli, posho Wala chakula.
Hata chai hawakunywa! Pia, tarehe 6 Machi alitoa magizo ya walimu wote wa somo la Hesabu kufika ofsini kwake siku ya Jumamosi tarehe 7 (leo), wakiwa na vifaa vyao vyote vya kufundishia pamoja na Madaftari ya Wanafunzi!
Fikirieni walimu wote wa Hesabu Halmashauri yote ya Mbinga DC wafike ofisini bila kupewa nauli, posho au Chakula kwa kadri ya miongozo ya utumishi wa uma!
Waende tena hiyo leo wakashindishwe njaa mpaka saa 12 jioni kama alivyofanyiwa wiki iliyopita!
Je haki za kiutumishi, hadhi na heshima ya walimu iko wapi katika nchi hii?
Mwalimu Nyerere baba wa Taifa letu angekuwepo leo angekubali Tena kuitwa Mwalimu kwa Matendo haya wanayofanyiwa wenzake na hawa wakurugenzi wasio na weledi na wasiotaka kufuata taratibu za utumishi wa uma?
Afisa Elimu wa Mbinga DC, Je unaona jambo hili liko sawa kwa walimu wenzako? Huoni kabisa kwamba huyu Mkurugenzi anaenda kinyume na Public Service Act- Sura ya 298 pamoja na Standing Orders for the Public Services?
Afisa;Je kama Mkurugenzi ana nia ya kufanya ukaguzi kwa walimu, Kwanini asingetumia gari na posho na mafuta anayopewa kutekeleza wajibu wake kwa kuwafuata mashuleni?
Utaratibu huu umekuwa ukisababisha usumbufu mkubwa kwa walimu kwani unatulazimu kusafiri kutoka vituo vyetu vya kazi kwenda ofisi ya halmashauri kwa gharama zetu wenyewe, bila kupewa nauli, posho ya kujikimu wala chakula.
Hali hii siyo tu inatuongezea mzigo wa kiuchumi kwetu walimu, bali pia inaathiri utendaji wetu wa kazi na muda wa kuwafundisha wanafunzi.
Ni muhimu mkumbuke kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Utumishi wa uma, pale mtumishi anapotakiwa kusafiri au kuitwa nje ya "kituo chake cha kazi" kwa shughuli za kikazi, mwajiri anatakiwa kugharamia stahiki zake ikiwemo nauli, posho ya kujikimu na mahitaji mengine muhimu.
Hivyo basi, kutuita walimu mara kwa mara ofisini kwenu bila kutupatia stahiki hizo ni kinyume na misingi ya haki na ustawi wa watumishi wa umma.
Ni muhimu mamlaka husika kuzingatia taratibu zilizowekwa ili kulinda haki za walimu na kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira yanayozingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma.