DOKEZO Mkurugenzi wa AUWSA asaini Mkataba wa kifisadi wa TZS 36.3 Bilion na Mchina bila Ridhaa ya Bodi ya Ununuzi ya AUWSA na wafadhili AfDB

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Moshi town

Senior Member
Dec 7, 2021
171
120
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Eng Justin Rujomba Tarehe 7.7.2022 amesaini Mkataba wa Construction of water blending system for FLOURIDE reduction wenye thamani ya TZS 36.3 Bilion na Kampuni ya Sinohdro Engineering ya china bila zabuni kutangazwa , Mkataba Ulisainiwa Tarehee 7.7.2022 kisiri bila kushuudiwa na Bodi ya AUWSA, Meneja Mradi Eng Mkawe na Menejimenti ya AUWSA kama utaratibu unavyotaka

Eng Rujomba hakupata Ridhaa ya Tender Board ya AUWSA kusaini Mkataba na wafadhili wa Mradi mkubwa wa Maji.

Arusha Bank ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) ilishatoa maelekezo kwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji AUWSA kuwa.

Wasitumie mfumo
Wa single source bali zabuni itangazwe apatikane
Mkandarasi mwenye uwezo lakini Eng Rujomba amekaidi kwa madai kuwa Kuna 10% ya kwake na Viongozi wa Wizara ya Maji.

PPRA Mwezi Novemba 2021 walitoa maelekezo zabuni zote zenye thamani inayozidi 5Milion itangazwe kupitia TANEPS,

Hata hivyo, Bank ya maendeleo Afrika (AFDB) wamegoma kutoa kibali ( No Objection ) ya kusaini Mkataba bila zabuni kutangazwa.

Maswali ya Msingi kwa nini zabuni haikutangazwa? Engineer Rujomba ametumia vigezo gani kuipatia zabuni kampuni ya sinohydro mkataba wenye Fedha nyingi kiasi hiki thamani ya TZS 36.3 bilion ?Kwanini mradi umesainiwa bila kushuudiwa na Wajumbe wa bodi ya AUWSA? kwanini Mradi umesainiwa bila kushuudiwa na Meneja wa Mradi na Menejimenti ya AUWSA? Kwanini mradi umesainiwa kisiri? Kwanini ENG Rujomba amekaidi
Maelekezo ya wafadhili Bank ya AFDB,

Ufisadi huu unafanyika AUWSA katika kipindi cha miezi Mitatau baada ya Kuvunjwa kwa Mkataba wa kifisadi wa Tzs 2.5 Bilion wa Ujenzi wa mfumo wa uondoaji Majitaka wa A to Z. Cha kushangaza walioshiriki kusaini huu mktaba wapo huru wanatamba kuiweka PCCB na wizara ya Maji mfukoni.

Waziri Mkuu , DG wa TAKuKuRu na CAG fanyeni uchunguzi wa mkataba wa Construction of water blending system for FLOURIDE reduction wa AUWSA na Sinohydro muokoe hizi pesa za wananchi maana mwisho wa siku watakaoumia ni wananchi amba ni walipa kodi na wahusika walioshiriki kusaini huu mkataba wachukuliwe hatua za kisheria.

62A03DA0-703F-4E9E-B3FE-21845C5097D4.jpeg
4F96E0A6-AC3F-4533-9CFD-3CC3D8802A36.jpeg
6CF38D7C-B382-4E08-BDC5-EF3F50501E81.jpeg
 
I chunguzeni sino hydro ndiyo mtoa rushwa mkubwa vinginevyo wataalamu wetu wa maji na barabara tutawapoteza wote. Hakuna mwenye akilu timamu atajataa rushwa ya hao jamaa, utendaji duni lakini wanaendelea kuoewa miradi serikali kama kawaida.
 
Tanzania Shillings 36 Billion kwa single source aliweza Magufuli tu kwa namna alivyokuwa ananunua zile Boeing na bombardiers.

Siamini kama hii taarifa Ina ukweli halafu bila idhini ya Bodi ya zabuni Wala hao AfDB??
 
Tanzania 36 Billion kwa single source aliweza Magufuli tu kwa namna alivyokuwa ananunua zile Boeing na bombardiers.

Siamini kama hii taarifa Ina ukweli halafu bila idhini ya Bodi ya zabuni Wala hao AfDB??
Mkandarasi Mshauri alitengeneza BOQ ikielekeza Gharama za ujenzi isizidi 20 bilion .. Rujomba Yeye kasaini mkataba wa 36 bilioni bila zabuni kutangazwa , aikupitishwa na bodi ya zabuni ya AUWSA ( AUWSA Tender Board) na hadi sasa Mfadhili Mradi Bank ya AFDB amegoma kutoa barua ya No
objection
 
AUWSA pia Wamesaini ..
 
Wasitumie mfumo
Wa single source bali zabuni itangazwe apatikane
Mkandarasi mwenye uwezo lakini Eng Rujomba amekaidi kwa madai kuwa Kuna 10% ya kwake na Viongozi wa Wizara ya Maji.
Mfumo wa single source naona ndio wapigaji ktk awamu hii wanatumia, si mliona hata wale wachina walipewa tenda ya kujenga SGR na waziri wa fedha kwa mfumo huu huu?
 
Kwa sasa nchi inapigwa kila mahali.kwenye maji,madini,rushwa kwa magari barabarani yaani kila sehemu.Tuvumilie tu hadi pale wazalendo tutakapoiongoza nchi na kuinyoosha tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upigaji Umezidi na anatamba waziri wa Maji Aweso na PCCB Arusha wapo kwenye payroll yake hivyo atishwi na chombo chochote cha Dola.

Ofisi ya CAG imetuma wakaguzi
Mara kadhaa bahati mbaya wakaguzi wanaotumwa wanapewa Pesa wanachomoa hoja.

AUWSA inatakiwa ifanyiwe Special Audit

PCCB Tumeni kikosi kazi waende wakachunguze AUWSA, Kamanda wa PCCB Arusha ameshindwa kutekeleza Majukumu yake
 
Swali mkuu, hivi huu umatemate ungekuwa umekupitia kweli ungekuja kulalamika hapa? sema mzigo umekupita pembeni, fedha nyingi kama hivyo ujue mpaka Waziri husika anajua, KM wake, RAS, RC n.k, sema hizi rushwa kubwa kwa mtu wa chini huwezi kuhusishwa, acha watu waitafuna hii nchi maana ni shamba la bibi
 
Aliyekwambia PCCB wao hawataki asali ni nani? PCCB waambie kuna mwalimu amechukua elfu 2 3 sijui 5 hapo wanajaa kama nyuki au mtendaji wa mtaa hao ndiyo wateja wao wakubwa hizo rushwa kubwa hawaziwezi hata kidogo maana zinaanzia juu kwa wateule wa no 1
 
Mkandarasi Mshauri alitengeneza BOQ ikielekeza Gharama za ujenzi isizidi 20 bilion .. Rujomba Yeye kasaini mkataba wa 36 bilioni bila zabuni kutangazwa , aikupitishwa na bodi ya zabuni ya AUWSA ( AUWSA Tender Board) na hadi sasa Mfadhili Mradi Bank ya AFDB amegoma kutoa barua ya No
objection
Kama ni hivyo basi imekula kwake maana amesaini mkataba na mfadhili amegundua kuna hiyo dosari, hakuna kitu kutaendelea
 
Swali mkuu, hivi huu umatemate ungekuwa umekupitia kweli ungekuja kulalamika hapa? sema mzigo umekupita pembeni, fedha nyingi kama hivyo ujue mpaka Waziri husika anajua, KM wake, RAS, RC n.k, sema hizi rushwa kubwa kwa mtu wa chini huwezi kuhusishwa, acha watu waitafuna hii nchi maana ni shamba la bibi
Yani hao jamaa waya zishatembea na msainishaji amefanya hilo kwa kujiamini kwamba wanaipiga hio 16B iliozidi hapo. Sijajua kwenye mgao itakuwaje ila kuanzia waziri hadi huyo mkurugenzi wanakula share ya zaidi ya billion kila mmoja wao.
 
Back
Top Bottom