Waziri Mkuu kuna Ufisadi wa Kutisha AUWSA, tuma kamati

Moshi town

Senior Member
Dec 7, 2021
171
120
Mheshimiwa Waziri Mkuu tunakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mhe Waziri Mkuu kuna Ufisadi wa Kutisha katika Miradi ya Maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Arusha ( AUWSA), Hizi Taarifa zimefika PCCB Arusha, Bodi ya AUWSA chini ya DR Masika Kwa Waziri wa Maji Ndg Juma Aweso awachukui hatua zozote na cha kusikitisha baada ya Waziri AWeso kupokea barua akamkabidhi Eng Rujomba na kumuonya akae mbali na Technical Manager Eng Humphray Mwiyombela Mwisho wa Siku wakamuondoa AUWSA

Kuna Mradi wa uondoaji Majitaka unaojengwa kwenda A to Z , Mheshimiwa Waziri Mkuu Serikali ilitoa kiasi cha Tzs 2.5bilion huu mradi ujengwe kwa Force Account maelekezo ayakufuatwa badala ya Kujengwa kwa Force account Mradi amepewa Tumaini Engineer bila Kufuata taratibu za Ununuzi na ni kinyume na agizo la Serikali ya Kazi hii ifanywe kwa kutumia mfumo wa Force account ,Pamoja na kupewa zabuni kinyume na taratibu Kampuni ya Tumaini Engineer imekuwa ikifanya kazi chini ya Kiwango width and Leng ya mtaro wa kulaza Bomba ni midogo ni tofauti na mchoro uliopo

Mkataba wa Tumaini Engineer na AUWSA aukupitishwa na Bodi ya zabuni ( Tender Board) ya AUWSA kinyume na Sheria ya Manunuzi PA, 2011 Section 35(1), (2) & 3 .Zabuni kutofuata Sheria ya Manunuzi The Public Procurement ammendment Regulation 2016- Section 91- Method of tendering for Non Consulting Services . Zabuni imeenda kinyume na Guideline’s for carrying out work under force account May 2020,15 .3, 15.5 & 15.1

Mheshimiwa waziri Mkuu kamati pia ichunguze Zabuni za Ununuzi wa Dira ( Mita) , Tender Board imepitisha Zabuni ya ununuzi Dira zenye thamani ya Tzs 880,000,000/= Dira zinazonunuliwa ni mbovu ni za Plastic zimewai kukataliwa na Evaluation team 2021 kwa kuwa zipo chini ya kiwango,Evaluation team ilizikataa 2021 kutokana na kudhiirisha kupunja Mamlaka, Mzabuni amepatiwa mkataba Januari mita ( Dira) zinatarajiwa kufika Mwezi wa tatu Mwaka huu TAKUKURU Majukumu yenu ni kupambana na Kuzuia Rushwa zuieni hii kuokoa Fedha za Umma msisubiri damages ndiyo Mjitokeze .

Mheshimiwa Waziri Mkuu Serikali ilitoa Tzs 520 bilion kwa ajili mradi Mkubwa wa Maji ambayo ilipaswa kukamilika Disemba 2020 cha kusikitisha Mradi bado aujakamilika upo Asilimia 70% na consultant anaongezewa Fedha za Malipo ya Usimamizi wa Mradi , Changamoto ni Eng Rujomba amevuta Pesa kwa consultant anashindwa kuwasimamia , akagui Miradi anaona aibu ameshavuta Pesa ..anasubiri ziara za Bodi, Ugeni wa Wizara ndiyo aende site muda wote yupo Dodoma , Dar , Moshi na Musoma .. Eng Rujomba aendi site anashinda Ofisini hata site meeting aendi anatuma wawakilishi yeye yuko busy kuchora michoro ya dili na kuwakarimu Viongozi wa Wizara, Tuma team ikague Mradi toka umeanza Kagua mikataba ya wakandarasi waliingia Mkataba wa Shilingi Ngapi na Wamelipwa kiasi gani hadi sasa… Wakandarasi wamelipwa zaidi ya Tzs 56 bilion za Ziada kuna Variation zinatengenezwa na Consultant za Kutisha.Na huu ni Mkopo ambao Mwisho wa Siku utalipwa na Serikali

Mheshimiwa Waziri Mkuu, Serikali ilipiga marufuku ulipaji Posho cha Kushangaza Menejimenti na Wasimamizi wa Mradi Mkubwa ya AUWSA ikifika disemba wanajilipa pesa za Sikukuu ya Noeli na Mwaka mpya kila Mjumbe Milion tatu hadi tano kufuatana na Cheo, huu ni ukiukwaji wa Maagizo ya Serikali.

Mheshimiwa Waziri Mkuu kuna Upotevu wa Maji Asilimia 54 kwa lugha nyingine AUWSA wanapoteza Maji mengi zaidi ya maji wanayouza kwa wateja kutokana na Upigaji wanadanganya kwenye Mahesabu Maji yanapotea kumbe ni Upigaji ,Na ni aibu AUWSA kupoteza Maji 54% na wamepatiwa na Serikali 520 bilion kusambaza maji na kudhibiti upotevu wa Maji.Kwa akili ya kawaida unapotezaje maji Asilimia 54% na
Kila mwisho wa Mwaka mnajilipa Milion tatu hadu tano za kusherekea Sikukuu

Mheshimiwa Waziri Mkuu Serikali ilipiga Marufuku Ununuzi wa Samani kwa wakuu wa Idara na Wakurugenzi, Wakuu wa Idara AUWSA na Eng Rujomba kila Baada ya Miaka Miwili wanajinunulia sofa zenye thamani ya 14 Milion kila Mmoja haya ni matumizi mabaya ya Fedha za Uma.

Mheshimiwa Waziri Mkuu Serikali ilitoa Maelekezo Magari ya Serikali yatengenezwe TAMESA na Siyo Garage bubu, Magari ya AUWSA yanatengenezwa garage bubu kwa Fundi John wametumia kiasi cha Tzs 465 Milion za Matengezo ya Magari garage bubu.. huu ni ukiukwaji wa maagizo ya Serikali

Mheshimiwa Waziri Mkuu kuna Tender ya Vifaa Pipe and Fiting ilifutwa mwezi Septemba 2021 na PPAA kutokana na ukiukwaji wa Taratibu wa ununuzi hii imesababisha Mamlaka kushindwa kuwaunganishia maji wateja wapya zaidi ya Elfu Kumi na Mbili ( 12000) tunajua na Ulimwengu unajua Eng Rujomba alivuta pesa Tzs 60 Milion akalazimisha mzabuni mwenye bei
Kubwa apatiwe zabuni , Swali la Msingi kwanini waziri na Bodi ya AUWSA awamwajibishi Eng Rujomba pamoja na PPAA kuthibitisha kulikuwa na Rushwa… Mzee KST ana Taarifa zote. Na Je? Eng Rujomba atawafidiaje Wakazi wa Jiji la Arusha ambao tayari wamelipa pesa za Maunganisho Mapya ya Maji awajaungnishwa? Na Je? Eng Rujomba Atafidiaje Maji yanayopotea kutokana na Uvujaji maana AUWSA awana mabomba ya kuziba Maji yanayomwagika wanachofanya ni kukunja bomba ? Na Je Rujomba atafidiaje wakazi wa Arusha ambao
Wanakosa maji kutokana na mabomba kukunjwa?


Kuna Mradi wa Uchumbaji visima 15 Vyenye thamani ya Tzs 4.5 bilion eneo wilaya ya Arumeru , Taarifa za tafiti za Kisayansi zinaonyesha Visima hivi vina Fluoride nyingi zaidi ya kiwango kinachotakiwa ambayo ni 0.5% visima hivi vina Fluoride 25% ni hatari kwa Afya ya Binadanu yanasababisha meno kuoza , Figo na matatizo ya akili.. Eng Rujomba alipewa pesa akasaini mkataba akijua maji ni hatari kwa afya ya binadanu…

Mhe waziri Mkuu Kuna Ufisadi katika Ununuzi wa Mashati, Mashati yaliyonunuliwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 bei iliongezwa kinyume na mapendekezo ya Evaluation team, Evaluatin team na Tender Board ilipendekeza Mashati mazuri kwa bei ya TZs 25,000/= kwa kila Shati cha kushangaza Eng Rujomba akaagiza bei iongezwe hadi Tzs 54,000/= bila kujali mapendekezo ya Evaluation team

Mhe Waziri Mkuu wafanyakazi wa AUWSA ambao ni wazalendo wanaopingana na Ufisadi wa Rujomba wananyanyasika na kushushwa Vyeo,

-Eng Mkama huyu alikuwa ni Msimamizi wa Mradi sehemu ya mtandao wa miundombinu majitaka.. huyu Mzalendo ameshushwa cheo na kuwa Engineer msaidizi kanda ya Ngaramtoni ameshushwa cheo baada ya kukataa kupokea mradi wa Pondi Mpya ya Majitaka iliyopo Terati iliyojengwa kwa Tzs 86 bilion kuwa kuwa hipo chini ya kiwango.. Hii pondi imejengwa chini ya kiwango Mkandarasi amekabidhi pondi disemba imeanza kubomoka na Majitaka yanaelea Juu .

- Eng Semba aligoma Tumaini Engineer kupatiwa Tender ya Mradi wa A to Z kutokana na Ukiukwaji wa Taratibu za Ununuzi,ananyanyasika kila kikao Cha Menejimenti anafokewa kuwa atekelezi Majukumu yake ipasavyo wakati Fedha za Upanuzi ( Extension) Shilingi 400 Milion za Majitaka amezichukua Eng Rujomba akapeleka kwenye mradi wa Longido ambao amechukua tender yeye kwa kutumia Mafundi na vibarua kutoka Moshi

-Afisa Ugavi Mija - Huyu mtumishi ni mzalendo alimgomea Eng Rujomba kuongeza bei Ununuzi wa Mashati , Evaluation team ilipendekeza Mashati yanunuliwe kwa Shilingi 25,000/= Eng Rujomba akalazimisha iongezwe hadi Tzs 54,000/= Baada ya Mija kugoma akaamishwa kwenda Pondi tena kwa kebei kuwa aende afaidi harufu ya Pondi

-Eng Tarimo huyu alikuwa Network Engineer wa Ngaramtoni- Ameshushwa cheo kwa Sababu aligoma maelekezo ya eng Rujomba ya kufaulisha Mabomba ameamishiwa Pondi mpya ya Terati

-Ibrahim Gagala alikuwa zonal incharges wa Ngaramtoni ameamishiwa Ofisi ya ukaguzi kwa Sababu alisambaza waraka wa ulioandikwa Jamiiforums ukielezea Ufisadi wa Eng Rujomba

-Surveyor Patric.. Alilazimishwa afanye kazi za Mkandarasi Tumaini Engineer ( Kazi ambayo hipo ndani ya Mkataba) akagoma kila Siku anatukanwa kwenye Vikao .


Mheshimiwa Waziri watanzania tuma imani kubwa sana na Mheshimiwa Rais Samia Hasan Suluhu pamoja na wewe ila kuna baadhi ya Mawaziri na Makatibu wakuu wanawaangusha wanayoongea wakiwa Jukwaani ni kinyume na wanyoyatenda

Tunaomba sana uunde kamati Maalum kuchunguza AUWSA kuokoa Fedha za Serikali, Waziri wa Maji Juma AWESO , Bodi ya AUWSA, PCCB wameshindwa kushugulikia huu ufisadi Pamoja na kuwa wana Taarifa zote.
 
Kale kawaziri aweso utasikia ukinizingua nami nakuzingua naona huko kamepigwa dole mgongo kanasikilizia utamu. Waziri Mkuu nenda kawasaidie hii mijitu ya mara ikikuongoza huwa ya mapumbavu sana. Hayana akili zaidi ya nguvu akili kisoda eti Rujomba yani jina kama dawa ya kienyeji
 
Kale kawaziri aweso utasikia ukinizingua nami nakuzingua naona huko kamepigwa dole mgongo kanasikilizia utamu. Waziri Mkuu nenda kawasaidie hii mijitu ya mara ikikuongoza huwa ya mapumbavu sana. Hayana akili zaidi ya nguvu akili kisoda eti Rujomba yani jina kama dawa ya kienyeji
Waziri mkuu hawezi kumgusa Aweso kale kajamaa kamemkamata maza vizuri kwa sasa.

PM mwenyewe anamalizia muda wake astaafu politiki ajiunge kwenye group moja na akina Pinda, Sumaye, Lowasa na Msuya . Anajikusanyia hela atulie mbele maana ndio baibai hiyo by 2025 atakuwa keshamaliza miaka 10 hapo nafasi inawindwa kweli .
 
Mtoa mada huyu Eng.Rujomba amekukosea nini...?...mbona huchokj kumuanika?
Ni Fisadi , Ameifanya AUWSA kuwa duka lake anachota anavyotaka, Wakazi wa Jiji la Arusha wanateseka kupata huduma bora ya maji kutokana na ufisadi wake.

Toka ameingia AUWSA akuna Project aliyosimamia ikafanikiwa mafanikio yaliyopo AUWSA ni Juhudi ya menejiment chini ya Mama Koya.. Iwe ni Tank ya Themi, Burka , Seed farm, Chekereni ,Pump station za Mbuguni , Mirerani na Visima 41 yote ni mafanikio ya Ruth Koya na iliyokuwa Menejinenti yake akisaidiwa kwa karibu na Eng Mkawe,CSM Edes Mushi ,PMU kitigwa , FM Kisanga na TM ENg Humphrey Mwiyombelwa..

Amebaki kudanganya makusanyo yameongezeka na Kufika 2 bilion wakati kuna zaidi ya Shilingi 400M ya malipo ya wateja kwa ajili ya maunganisho mapya..Na awaunganishiwa kwa wakati kutokana na AUWSA kutokuwa na mabomba

Eng Rujomba toka ameingia AUWSA ni upigaji tuu wa Fedha na kutukana wafanyakazi , miradi yote yaliyoanza toka kaingia AUWSA ni Failure .. Nenda Ngorongoro kuna Mradi wa Maji umesimama hakuna Mabomba, Nenda Namanga Mradi auishi , Nenda kakague visima 15 vinavyochimbwa Arumeru zina Fluoride zaidi ya kiwango kinachotakiwa ,Pamoja na Kuwa na Fluoride zaidi ya kiwango mradi ausogei.

Wageni wakitembelea AUWSA anawatembeza miradi iliyosimamiwa na Eng Ruth Koya miradi yake ni Jipu tupu athubutu kuwapelela wageni kutoka wizarani,
 
Ni Fisadi , Ameifanya AUWSA kuwa duka lake anachota anavyotaka, Wakazi wa Jiji la Arusha wanateseka kupata huduma bora ya maji kutokana na ufisadi wake.

Toka ameingia AUWSA akuna Project aliyosimamia ikafanikiwa mafanikio yaliyopo AUWSA ni Juhudi ya menejiment chini ya Mama Koya.. Iwe ni Tank ya Themi, Burka , Seed farm, Chekereni ,Pump station za Mbuguni , Mirerani na Visima 41 yote ni mafanikio ya Ruth Koya na iliyokuwa Menejinenti yake akisaidiwa kwa karibu na Eng Mkawe,CSM Edes Mushi ,PMU kitigwa , FM Kisanga na TM ENg Humphrey Mwiyombelwa..

Amebaki kudanganya makusanyo yameongezeka na Kufika 2 bilion wakati kuna zaidi ya Shilingi 400M ya malipo ya wateja kwa ajili ya maunganisho mapya..Na awaunganishiwa kwa wakati kutokana na AUWSA kutokuwa na mabomba

Eng Rujomba toka ameingia AUWSA ni upigaji tuu wa Fedha na kutukana wafanyakazi , miradi yote yaliyoanza toka kaingia AUWSA ni Failure .. Nenda Ngorongoro kuna Mradi wa Maji umesimama hakuna Mabomba, Nenda Namanga Mradi auishi , Nenda kakague visima 15 vinavyochimbwa Arumeru zina Fluoride zaidi ya kiwango kinachotakiwa ,Pamoja na Kuwa na Fluoride zaidi ya kiwango mradi ausogei.

Wageni wakitembelea AUWSA anawatembeza miradi iliyosimamiwa na Eng Ruth Koya miradi yake ni Jipu tupu athubutu kuwapelela wageni kutoka wizarani,
Kwani huwa hakuna ukaguzi unafanyika hapo?
 
Kwani huwa hakuna ukaguzi unafanyika hapo?
Kwani huwa hakuna ukaguzi unafanyika hapo?
Wakaguzi wanakuja kila Mwaka kuna wazee walikuwa TPA ndiyo wamepewa Jukumu la kukagua kwa
niaba ya Ofisi ya CAG Wanakagua vitu vidogo vidogo haya makubwa wanapewa Mshiko wanaondoa hoja… ni uhuni mtupu.

Mradi wa A to Z Ofisi ya CAG ilituma wakaguzi wakabaini kuna Ukiukwaji wa Taratibu za Ununuzi na Taarifa ilikabidhiwa bodi na Wizara ya maji hakuna hatua zilizochukuliwa

Bodi ya AUWSA iliunda kamati ya Uchunguzi mwenyekiti akawa ni Ndugu wa Aweso Ambaye ni Mjumbe wa bodi CPA Omari Sharif wameishia kulipana Posho za Shiling 34 Milion za Uchunguzi kwa Week Moja hakuna cha maana zaidi ya kulipana posho … upigaji juhu ya Upigaji.
 
Back
Top Bottom