Menejimenti ya AUWSA yakaidi agizo la Waziri Mkuu, Wametumia Milioni 216 kwenda kutalii Mwanza

Moshi town

Senior Member
Dec 7, 2021
171
120
Menejimenti ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha Chini ya Engineer Justin Rujomba imetumia Milioni Mia Mbili na Kumi na Sita ( 216 Milion) kwenda Mwanza kwenye Semina na Kutalii kwenye Mbuga ya Wanyama Serengeti kinyume na maagizo ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Kasim Majaliwa aliyoyatoa wakati akifunga Bunge la Bajeti 2022/2023.

Mheshimiwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa alipiga marufuku Taasisi za Umma kutumia Fedha za walipa kodi katika Semina , Warsha na Utalii na badala yake akatoa agizo semina na Warsha Zifanyike kwa Njia ya mitandao ili kuongeza kasi ya maendeleo.

Ziara hii imefanya Shuguli za Mamlaka ( Maunganisho Mapya , Makusanyo na Uzibaji wa Mivujo ) kusimama kutokana na Usafiri wa Mafundi kwa maana ya Magari 8 yameenda katika Ziara hiyo hivyo Kufanya Mafundi kushindwa kwenda sites kuhudumia Wakazi wa Jiji la Arusha.

Kaimu Mkurugenzi AUWSA ameachiwa Junior staff Arnord Kipanju ( Ambaye ni Mpwa wake MD Rujomba) kutokana na Menejiment yote ( MD, Wakuu wa Idara , Wakuu wa Sehemu na units) wote 28 wamesafiri .

Ziara hii inafanyika wakati Upotevu wa Maji AUWSA ukiwa ni 63% kwa Lugha Raisi ni kwamba AUWSA inauza Maji asilimia 37% tuu Asilimia 63 ya Maji yanapotea

Pamoja na Serikali kuu Kuvunja mkataba wa AUWSA na Mkandarasi wa Mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya Uhondoaji majitaka wa A to Z Kampuni ya Tumaini Engineer wahusika waliousika katika kuingia Mkataba huu wa kifisadi wapo huru na wanajisifu hakuna wa kuwakamata kwa maana wameiweka Wizara ya Maji, na TAKUKURU Arusha Mfukoni .

Haya yanatendeka ikiwa Tayari Serikali Imetoa Tzs 530 bilion kusambaza maji Jiji la Arusha lakini Maji ayaonekani yakiongezeka katika Jiji la Arusha Mgao wa Maji umeongezeka maradufu.
 
Jamii lazima ibadili mtazamo juu ya wanqoiba pesa za umma ila kama jamii itaendelea kuwaona watu waoiba pesa za umma ni watu waliotoboa na wanaolamba asali basi tutegemee msiba mkubwa zaidi kwenye pesa za umma.
Ni aibu kula pesa za walipa kodi ni aibu sana..
 
Hapa Bila katiba mpya ni kazi bure Tu hiyo nafasi hata nikipewa Mimi lazima nipige hela tu
Katiba ni maandishi tuu, kitu muhimu ni utekelezaji wa majukumu. Iwapo wanaopewa mamlaka wanaamua kufanya ufisadi katiba haitawazuia. Hata hivi tusemapo, kuna sheria kemkem za kupigana na ufisadi, lakini sie wananchi wenyewe ndio mafisadi na tunaushabikia ufisadi ndio maana unashamiri.
 
Wanafanya haya Kwa sababu wanajua kwamba hakuna hatua zitakazochukuliwa..

Hata hivyo unaweza Kuta hizo pesa ziko kwenye fungu lao la matumizi mengine na zilipitushwa na Bunge so kisheria wanakuwa wako sahihi maana hawajaingilia mafungu mengineyo.
 
Kuna wakati niliwahi kuwaambia baadhi ya watumishi wa umma, 'kesheni mkiomba bwana yule asije kuwa rais wa JMT; maana, mtalia na kusaga meno'. Ndani ya miezi sita wengi wenu mtakuwa mmekwisha fukuzwa kazi na baadhi yenu mtaishia koro koroni...
Wakaitikia Amina 😎
 
Hii imekaa kimbea zaidi.

Si kila jambo linaweza fundishwa kwa video, mambo mengine hadi ufike field ujionee, MWANZA nadhani ndio inaongoza kitaifa kwa kufanya vizuri upande wa makusanyo na udhibiti wa upotevu wa maji. Hivyo wengine kwenda kujifunza MWAUWASA imefanikiwa vipi si jambo la ajabu.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji ndio alikuwa Mwanza, performance ya MWAUWASA ndio ilimpandisha hadi kuwa katibu mkuu, wapo wengine wametolewa Mwanza kwenda kupewa vyeo sehemu nyingine ili kuokoa jahazi mamlaka nyingine.

Nadhani hujafurahishwa na safari ya wenzako Mwanza, sasa ukisikia uongozi umeenda Germany au Japan kujifunza si ndio utapagawa kabisa.

Kuwa mvumilivu tu, nawe utapanda ngazi, uanze lamba asali pia.
 
Mwanza hii hii ambayo maji ni ya mgao? Kweli serikalini kuna shida mahali.
 
Hii imekaa kimbea zaidi.

Si kila jambo linaweza fundishwa kwa video, mambo mengine hadi ufike field ujionee, MWANZA nadhani ndio inaongoza kitaifa kwa kufanya vizuri upande wa makusanyo na udhibiti wa upotevu wa maji. Hivyo wengine kwenda kujifunza MWAUWASA imefanikiwa vipi si jambo la ajabu.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji ndio alikuwa Mwanza, performance ya MWAUWASA ndio ilimpandisha hadi kuwa katibu mkuu, wapo wengine wametolewa Mwanza kwenda kupewa vyeo sehemu nyingine ili kuokoa jahazi mamlaka nyingine.

Nadhani hujafurahishwa na safari ya wenzako Mwanza, sasa ukisikia uongozi umeenda Germany au Japan kujifunza si ndio utapagawa kabisa.

Kuwa mvumilivu tu, nawe utapanda ngazi, uanze lamba asali pia.
Tumia akili usitumie Matako Kujibu hoja, Issue ni Matumizi mabaya ya Fedha ya Umma na kukaidi agizo la waziri Mkuu. Unataka kutuambia Waziri Mkuu ana Wivu kuzuhia Warsha na Utalii? Tshs 216M ni extension Kilomita ngapi za Majisafi?

Na kwa Taarifa yako Mamlaka yenye upotevu mdogo wa Maji ni Moshi ina below 25% Mwanza ina upotevu wa Maji above 38% . Ni akili kweli au tope kwenda kujifunza Mamlaka yenye upotevu wa Maji above 38%

Usimuhingize Eng Sanga Kwenye Upigaji wenu … Engineer Sanga ana heshima zake amejenga Carier yake kwa Miaka zaidi ya 20.

Tupatie na Jibu Mkataba wa AUWSA na Tumaini Engineer wa Ujenzi wa Mradi wa A to Z umevunjwa kwanini? Na Je wahusika waliongia Mkataba huu
Wa Kifisadi wa Tshs 2.8 billion wamechukuliwa hatua gani?
 
Shida ni pesa hiyo... Nyingi sana. Ila kutalii kiofisi sio mbaya. Wachunguzwe
 
Hii imekaa kimbea zaidi.

Si kila jambo linaweza fundishwa kwa video, mambo mengine hadi ufike field ujionee, MWANZA nadhani ndio inaongoza kitaifa kwa kufanya vizuri upande wa makusanyo na udhibiti wa upotevu wa maji. Hivyo wengine kwenda kujifunza MWAUWASA imefanikiwa vipi si jambo la ajabu.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji ndio alikuwa Mwanza, performance ya MWAUWASA ndio ilimpandisha hadi kuwa katibu mkuu, wapo wengine wametolewa Mwanza kwenda kupewa vyeo sehemu nyingine ili kuokoa jahazi mamlaka nyingine.

Nadhani hujafurahishwa na safari ya wenzako Mwanza, sasa ukisikia uongozi umeenda Germany au Japan kujifunza si ndio utapagawa kabisa.

Kuwa mvumilivu tu, nawe utapanda ngazi, uanze lamba asali pia.
Mumezoea kuhumiza Rahia na Nina Mashaka Kama unalipa kodi , Wiki iliyopita AUWSA wametumia Milion Kumi ( Ten Milion) ya kamati ya kwenda Dar kuhakiki Furniture za Ofisi zao Mpya zilizopo Kisongo… Ni Akili au tope kutumia 10 Milion na Magari 2 kwenda Dar kuhakiki Furniture? Kamati yenyewe imejaa washkaji wa Rujomba na Ndugu zake kutoka kanda ya ziwa..

Na cha kushangaza Eng Rujomba ameunda hii kamati kwa kuwaweka washlaji wake kutoka Moshi akiwemo hawara yake na Ndugu zake kutoka kanda ya ziwa.

Mamlaka ya AUWSA inachezewa sana
Imegeuzwa shamba la Bibi.
 
Back
Top Bottom